Wapinzani Tokeni Bungeni Waacheni CCM Wajibishane/Kulindana

Kuntakint

JF-Expert Member
Sep 26, 2011
1,768
2,000
Iliniuma sana jana nilipokuwa nasikiliza bunge. Hasa wapinzani nao wakiwa pamoja kujadiliana na watuhumiwa katika kupendekeza namna ya kuwaadhibu. Jamani Lisu mwanasheria ukushituka kuwa huu ni mchezo. Kweli inaingia akilini kujadiliana na Chenge mnamwachia nafasi aongee namna ya kujihukumu?

Au mlilishwa dawa? tangu lini Lukuvi, Makinda wakawaita na kuwaambia mkae mjadiliane zaidi ya kuwazomea na kusema watoke wamezoea hao na kejeli nyingi. Ninachowaambia ndg zangu wabunge wa upinzani hili swala Escrow.CCM wanalijua na wamejipanga kuwamaliza kisiasa ili mmbariki mpango wao wa kutowajibisha wahusika. Kamati ya PAC ndio bunge, na katika uchunguzi wamefuatilia uchunguzi kutoka kwa CAG na TAKUKURU ambazo zote ni vyombo vya serikali. Sasa kuna uchunguzi gani tena inayotakiwa ifanyike???

Taarifa ya PAC mmeisoma kuna sehemu gani imeingilia mahakama?? Kwasababu haya mapendekezo yanaenda kwa serikali hayaendi mahakamani. Mifano hai zipo na mnazijua leo bado mnaambiwa kamati zikae mpaka saa nane na nyie mnakubali. Wanachotaka CCM ionekane kwa wananchi,mataifa za nje (wahisani) kuwa hata vyama vya upinzani vilishiriki yani muonekane wote ni walewale. Serikali inayowajibika ukipatikana na kosa hata la kuhisi tu unajiuzulu au unakaa nje kwa uchunguzi.

USHAURI
Mwambieni spika mapendekezo yabaki kama yalivyopendekezwa na PAC. Yapelekwe kwa serikali, Serikali ndio wataamua kuwaajibisha waliotajwa na wao ndio watafanya uchunguzi wao na kuona kuwa watuhumiwa wanastahili kuwaadhibiwa kazi sasa ni la serikali. Uchunguzi wa bunge limefanyika ndio hayo makabrasha mliyokuwa mnajadili. Watuhumiwa ambao bunge linaweza kuwaajibisha wawajibishwe kama kamati (PAC) ilivyopendekeza. Spika akikataa tokeni bungeni kama mnavyofanya siku zote. Muwaache CCM Wawajibishane wenyewe. Mrudi saa nane na azimio hilo. Swali la kujiuliza Je mumeona kama kuna barua kutoka mahakamani au ni danganya toto.

Haya maamuzi mlikuwa mchukue tangu jana mapema kabla ya saa nne wala msingekuwa Dodoma leo. Manapoteza muda maazimio CCM Walishapanga tangu Jumatatu.

Naomba usiliunganishe na Taarifa zingine hii ni ushauri mpya wa leo kuwashauri upinzani. Pls Pls
 

Ileje

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
5,835
2,000
Hatoki mtu bungeni!

Kama wabunge wa magamba wataendelea kuwatetea wezi na mafisadi, Wabunge wa UKAWA watasimama kama jana na kuimba kwa nguvu zote wa kuhamasisha mapambano ndani ya bunge!
 

Osaka

JF-Expert Member
Jun 21, 2011
1,762
1,225
Ina maana unataka kusema ule mchezo wa jana utaendelea tena leo na mwafaka hautafikiwa?
 

Kuntakint

JF-Expert Member
Sep 26, 2011
1,768
2,000
Ina maana unataka kusema ule mchezo wa jana utaendelea tena leo na mwafaka hautafikiwa?

Mchezo imepangwa ivyo sakata lipo kama jana. Kikubwa wapinzani wakitoka CCM wataona aibu kwa raia na mataifa wahisani ivyo watuhumiwa wataondolewa
 

Ileje

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
5,835
2,000
Ina maana unataka kusema ule mchezo wa jana utaendelea tena leo na mwafaka hautafikiwa?
Ile ndiyo mbinu pekee ya kukabiliana na Bibi Kiroboto na ujanja wa serikali kutaka kuwa- frustrate UKAWA ili wasusie bunge na CCM wabaki wanapitisha maazimio ya kuwalinda mafisadi!
 

Osaka

JF-Expert Member
Jun 21, 2011
1,762
1,225
Ile ndiyo mbinu pekee ya kukabiliana na Bibi Kiroboto na ujanja wa serikali kutaka kuwa- frustrate UKAWA ili wasusie bunge na CCM wabaki wanapitisha maazimio ya kuwalinda mafisadi!
Nimekupata vizuri mkuu Ileje.
Kumbe lilikuwa ni suala la kuvuta muda tu hadi leo lakini maamuzi anayo Anna pamoja na timu yake.
 
Last edited by a moderator:

instagramboy

JF-Expert Member
Oct 16, 2014
1,523
0
CCM.OYEEEEE TEEEEHHHH jv hiki chama kinakufa lini?? maana kimechokaa hafi wabunge wao wengi vilaza
 

afwe

JF-Expert Member
Oct 29, 2010
4,085
2,000
Hatoki mtu bungeni!

Kama wabunge wa magamba wataendelea kuwatetea wezi na mafisadi, Wabunge wa UKAWA watasimama kama jana na kuimba kwa nguvu zote wa kuhamasisha mapambano ndani ya bunge!
Na hii ndio nmna sahihi ever!
 

LESIRIAMU

JF-Expert Member
Feb 12, 2008
6,142
2,000
Unajua Ccm wanafanya utani na hili jambo. Jana nilikuwa na wazungu kama watano mahali hawajui kiswahili wakaniuliza hivi bungeni wanaendeleaje? Nikawapa brief jinsi wabunge wa Ccm wanavyo tetea ujinga na kuwaambia kuna hujuma hata umemme pia wamekata ili watu wasione.

Mara kijana mmoja kaja na simu yenye radio anasikiliza bunge huwezi amini walimzunguka na kuniomba niwatafsirie maongezi ya bungeni. Hii ni aibu kwa taifa. Ccm kuweni makini. Tamaa zinaliqweka Taifa uchji.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom