Wapinzani Tanzania hawajui matatizo ya watanzania - Mwigulu Nchemba

Kuchasoni Kuchawangu

JF-Expert Member
Aug 21, 2012
603
340
Akihutubia mkutano wa hadhara maeneo ya wilaya ya Igunga Mwigulu Nchemba amesema,Viongozi wa upinzani mpaka leo hii hawajui tatizo linaloikabili nchi yetu, wameshaanza na kuwashawishi na wengine wasijue tatizo linaloikabili nchi yetu.

Wanasema wanapigania uhuru,uhuru upi alihoji Nchemba.wanasema wanafanya mipango ya ukombozi,ukombozi upi?. Nchi ilishakombolewa tangu 1961 na tatizo la watanzania leo hii sio uhuru.(akamtaja Freeman m/kiti CHADEMA akiitwa anaitika eti anataka uhuru) Ni taabu sana kuwa na upinzani haujui tatizo la watanzania.

Nchemba alisema, Tatizo la watanzania ni mambo ya uchumi, mambo ya kipato, na kinachotakiwa ni kufanya mapinduzi ya kiuchumi ili watu wapate ajira waendeshe shughuli zao.

Wanasema nchi ina mabonde mengi mbona hatuna chakula, eti mabonde siku hizi yanaliwa aliuliza. Tuna dhahabu hapa kwenu kuna soko la dhahabu? Ukichimba utaila? Wazungu tuliowategemea hawaji tena uchumi wao umeyumba uero imeyumba. Mjadala uko wazi kwa hotuba hii.

Naambatanisha na Audio yake.

[JFMP3]www.jamiiforums.com/attachment.php?attachmentid=72461&stc=1&d=1353873727[/JFMP3]
 

Attachments

  • mwigulu.mp3
    2.8 MB · Views: 50
Mwigulu ni First Class-Failure, Boss wake JK hajui kwa nini TZ ni maskini, hivi maswali huwa hayaruhusiwi kwenye mikutano, angeulizwa huyu ''kyalu''
 
kanena vyema...mnataka ukombozi....ukombozi upi....?? matatizo ya watanzania sio flani ni fisadi na flani anatembelea bajaji...matatizo ya mtanzania ni kupata ajira za uhakika..kupata kipato cha uwakika na huduma bora na si vinginevyo
 
Kumbe JK na PINDA ndiyo wapinzani wa nchi hii, maana kumbukumbu ndiyo zinaonyesha wao kuwa hawajui kwanini nchi hii ni MASKINI. Nafikiri Mwigulu alikuwa hana la kufanya Igunga maana hakujua hata anachokiongea, labda kuna kitu kingine amekifuatilia huko.
 
Hivi huyu nae ni mwanasisa.Kama anayajua matatizo wa watanzania kachukua hatua zipi.
 
Sijui ni kwa nini mtu kama huyu Nchemba haji humu jamiiforums na kumwaga pumba kama hizi!!!,sipati picha angetokea mlango gani.

Watanzania waliokuwa wakihutubiwa na Mchemba wengi wao(baadhi) wana njaa/matatizo kibao/elimu mbovu kichwani mwao na hapo hapo wameshaahidiwa pilau huku wakiwa wameshagaiwa kofi/kanga/tishirt na vitambaa hivyo vichache tu kwa watu wa jamii hiyo hata wakitukanwa watamshangilia sioni ajabu,ila ninaamini wapo pia wenye fikra nzuri watampuuzia kwa maneno yake mbofu mbofu.
 
ile ilikuwa political freedom...........watu tunaongelea freedom of mind, awareness, being, consciousness nk....kweli first class nyingine za kudesa taabu kwelikweli....
 
Mhhhhhhhh yupo Igunga mida hii, ngoja nimpigie kaka yangu awe makini na yule mke wake mzuri asionwe na jamaa ikaja kuwa kilio!
 
INAPOELEZWA kwamba chama tawala cha CCM kimepoteza mwelekeo, wapo wanasiasa nguli wa chama hicho wanaojifanya hamnazo na kuona kama hizo ni kelele za mfamaji au za debe tupu ambalo haliachi kutika
 
kanena vyema...mnataka ukombozi....ukombozi upi....?? matatizo ya watanzania sio flani ni fisadi na flani anatembelea bajaji...matatizo ya mtanzania ni kupata ajira za uhakika..kupata kipato cha uwakika na huduma bora na si vinginevyo

ukombozi wa fikra....
 
Duuuh Burn karudi kaanza kutekeleza maazimio ya cc ya ccmweli.
 
Kiukweli kama haya ndio maneno yake jamaa ni LOSSER hata hiyo 1st class nina wasiwasi nayo.

Nimesikiliza sana CDM kwenye kampeni wamekuwa wakiongelea kuwa wakipewa NCHI watafufua viwanda ili vijana wapate kazi hii nilisikia kwa Zitto aliposem kuwa hata mashamba ya mikonge yanatakiwa yarudi kwa waanchi maana walio nayo hawayafanyii kazi.

Dr Slaa alisema kama angeshinda angeutilize resources na kukusanya kodi ipasavyo ili vitu kama Elimu ipatikane BURE hii hata Lowassa kaisema jana.

Pia Dr Slaa alisema atashusha bei ya vifaa vya ujenzi ili watanzania waweze miliki nyumba hii Kinana kaiongelea pia.

Hadi hapo wapinzani wanafahamu matatizo ya watanzania.
 
Enhe! kuna wanasiasa TZ ila huyu ni kiboko, sawa kama yeye na wenzie wanayajua matatizo ya watanzania, wamefanya nini kuyatatua kwa miaka 50 na waliyokaa madarakani? huo mkutano haukuwa na fursa ya maswali watu wamuulize?
 
ukombozi wa fikra....

ukombozi wa fikra ni juu yako mwenyewe kujitambua wewe ni nani mpaka sasa unafanya nini na ili iweje.
kiukweli alichokisema mh.mwigulu tatizo kubwa la watz ni uchumi tu,mengine yanafuata maana watu wakiwa na uchumi ulio bora sidhani kama kuna atayelalamika ama kujihusisha na siasa.Yule anayepinga hili haiyumkini uchumi wake ni mzuri ama anawapumbuza watu kiuchumi ili aendelee kuwatawala kifikra.Siku zote ukombozi wa kifikra ni elimu,kwa hali ilivyo sasa bila ya pesa (uchumi) kuipata elimu ni vigumu sana labda uwe na uwezo ama kujitambua mapema ili kutia juhudi.
 
HUYU BWANA LEO NIMEMUONA NA GARI KUBWA V8 T203 .... Ndio naona anayajua matatizo ya Watanzania
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom