Wapinzani, Si kila anayekosana na Magufuli ni mtu mwema au wa kutetewa

GuDume

JF-Expert Member
Jan 18, 2015
6,651
14,318
nimeona hii tabia inayotaka kuzuka ya kuamua kuwa wapinzani uchwara. yaani sasa ni kumtetea kila ambaye serikali ya magufuli itamshughulikia. haya mambo yanakua kwa kiwango cha juu sana. leo hii yusuf manji anaonekana ni mtu mwema kabisa anaonewa. kweli? leo hii andrew chenge anaonekana ni mtu mzuri kabisa wa kumshabikia. leo hii wema sepetu anaonekana ni mtu mwema kabisa katika jamii.

upinzani huu ni upinzani uchwara. haya mambo ya kusema ifuatwe sheria mbona miaka ile ya nyuma ilitajwa list ya mafisadi mwembe chai na tukawahukumu moja kwa moja hao watu? zilipofuatwa sheria kuwa upatikane ushahidi yakinifu ikaonekana kuwa kulikuwa na kigugumizi au woga katika kuwashughulikia.

leo tunataka mtu ikithibitika nusu kuwa anahusika na madawa ya kulevya awekwe ndani kwanza tayar kwa uchunguzi watu wanaana kutetea waovu. leo hii kukamatwa passports zaidi ya 100 kwa mtu flan inaonekana kuwa anaonewa sababu kesi ya kwanza ilikuwa ni madawa ya kulevya. wangapi tuliosoma zamani tunakumbuka ilikuwa ukiitwa ofis ya walimu kwa kosa la kupiga kelele ukifika kule watakuangalia na ikigundulika hukuchomekea utadhibiwa tena, ukigundulika umevaa kandambili utachapwa,ukigundulika kuna siku ulitoroka utachapwa na makosa hayo tena. nani amesahau? hii ilitufanya tunapoenda ofisi ya walimu hata kwa jambo jema tujikague mara kadhaa kabla ya kwenda.

wapinzani tusibadilike na kupinga kila kitu... kuna watu hawatakiwi kuonewa huruma kwa namna walivyolinyonya taifa hili. leo hii huyu zile pesa zilizokamatwa pamoja na mtumishi toka quality group akiwa nazo dodoma tayari kwa kugawa zisingekamatwa tungekuwa na moja ya marais Hopeless kabisa duniani. na huyu angekuwa amewekwa na aliyezituma pesa hizo. ni nani alizituma?hatujui ila mfanyakaz wa kutoka quality group mwenye asili ya kiasia ndiye aliyehusika kuzibeba pesa hizo.
 
sijui uchaguzi ujao watakuja na ajenda gani maana zoooote zipo kwao,
kumbukeni kuweka akiba ya maneno
 
Hivi wewe mpinzani kwako ni nani? Kila mtu anayekosoa serikali au viongozi wa serikali ni wapinzani?

Jamii gani katika dunia yenye watu wanaofanana mawazo, mitazamo, vipaumbele na hata uwezo wa kuelewa? Kwa hiyo kwa makamasi yako unayotumia unadhani wanaokosoa serikali pale inapofanya vibaya wote ni lazima wawe wapinzani, na wanaosifu pale panapokuwa na mema wote ni ccmm?

Tabia za kununua vyeo na madaraka hizo ni za ccm. Na ndiyo matokeo yake haya unayoyaona.

Sina tatzizo na Magufuli kwa sababu ni biandamu kama wengine na naomba na yeye asije akajiondoa kwenye kundi la binadamu kwa kuwa atakosa mahala pa kusimama. Hawezi kuwa kitukingine zaidi ya binadamu.

Tatizo langu ni Ccm na mifumo yake ya kijingae. Hamuwezi kulazimisha utawala wakati mlishashindwa miaka mingi na wananchi ahwawataki, halafu mlazimishe kutenda mema ambayo ni mwiko kwenu, mkijidai kusafisha nchi huku mkijua ninyi ndio mliochafua na wachafuzi ndio wanaowangoza.

Masuala ya kitaifa yasifanywe agenda za kisiasa kwa sababu athari zake hazibagui watu kwa vyama!.
 
Hatuangalii ubaya aliowahi tenda
mtu, maadam katoka kwa shetani(ccm)
Kaja kwenye ufalme wa Mungu(chadema)
Sisi humsamehe na kuanza upya.
Na hapo huwa mchapa kazi zaidi ya yule aliekaa zaidi katika ufalme.
 
Mawazo na itikadi kama hizi ndio ujinga tunaoukemea, kwa hiyo mnataka wauza madawa ya kulevya waachwe bila kushughulikiwa, ama kweli ubatizo wa nyumbu huondoa utashi na kupandikiza falsafa za kijinga.
 
Hongera mleta Uzi mwenye akili ameelewa na asiyeelewa basi ana lake jmbo na kuhusu upinza nadhani Mwenyezi Mungu akipenda akitufkisha 2020 na washauri wtafute shughuli nyingine ykufnya Sio siasa itawawiya ngumu sana
 
Kila jambo linalotokea ni ishara ya jambo linalofuata.....au jambo lililopitia.......

Mimi binafsi sina imani na watu tunaowaita wapinzani katika taifa hili.....ingawaje utawala uchwara wa CCM umeshatuchosha kama sio kutukinaisha........

Haikuhitaji kuwa na kiwango kikubwa cha akili kuweza kugundua hilo zaidi kutumia vyema kilichomo kichwani mwako.....na kujitoa kwenye mapenzi........

Kusema ukweli heka heka za upinzani kupaza sauti za utetezi hata kwa watu ambao awali walikuwa wamewapa kila aina ya majina mabaya ya ubadhilifu huwa kinanishangaza sana...........na kusikitika kuwa Tanzania kama nchi nchini ya CCM imeshapoteza dira....lakini watu wanaotubembeleza kuwa wanaweza kuwapokea CCM kijiti......ndio wanatuvunja moyo zaidi kutokana na matendo yao..........

Bado nina kumbu kumbu mbaya za wao kutuletea mgombea uraisi ambao wao wenyewe kwa kauli zao na kwa ushahidi wao usio na shaka....walituthibitishia kuwa hafai.......huwa nawaza kuwa ilitumika akili gani kwenye kulifany lile na sipati jibu zaidi ya kucheka......nawahurumia zaidi nionapo vijana wasiotumia akili zao vyema wakiandamana na kuunga mkono jambo hilo........

Kwa kifupi ni kwamba tupo chini ya utawala mbovu wa CCM.....ambao hauna dira wala maono.....lakini cha kusikitisha tuna upinzani wa ajabu ambao hauna dira wala maoni......ambao unakupa maswali mengi kuwa wakipata utawala watakuwa ni watawala wa aina gani.......

MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
Upinzani wamegeuka watetezi wa mafisadi, wakwepa kodi, wabadhilifu wa mali za uma, wauza unga, mashoga...inatia aibu shekhe
Wajanja wa siasa wamewaweka kwenye hiyo position ya kutetea waovu bila wao kujua. Kwa lugha ya mtaani, wamelishwa matango pori lakini wao wanajiona wanapambana. Niliuliza, utakuta topic ina wachangiaji 200 lakini viewers 5000, hujiulizi hao silent 5000 wanamtazamo upi kwenye huu utetezi unaondelea!
 
Waende nchi za magharibi waone jinsi polisi wanavyofanya kazi. Unaweza kukamatwa na kosa la kuendesha gari lakini wakakuchunguza Mambo mengine mengi tu
Mkuu unafurahisha, Naona hollywood movies zinakuchanganya..Kumbe kuendesha gari nalo ni kosa..Hebu tusaidie ni nchi gani ya magharibi ambapo askari huwa wanajazana barabarani kukamata magari?
 
Back
Top Bottom