Wapinzani Serikalini wasimamishwa kazi - Kujihisisha na siasa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wapinzani Serikalini wasimamishwa kazi - Kujihisisha na siasa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Jun 1, 2011.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Jun 1, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Watumishi watano wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete wamesimamishwa kazi wakidaiwa kujihusisha na masuala ya siasa kinyume na kanuni za kudumu za utumishi wa umma. Watendaji hao ni kutoka idara ya mipango, idara ya maji na watendaji watatu, wakiwemo wawili wa kata na mmoja kutoka ngazi ya kijiji. Watumishi hao kwa pamoja, wakiwa kila mmoja katika eneo lake la kazi, wanatuhumiwa kufanya shughuli za kisiasa wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka jana.

  Kufuatia tuhuma hizo, Halmashauri ya Wilaya ya Makete imewasimamisha kazi na kuwapa nafasi ya siku 14 za kujieleza kwa maandishi kuthibitisha kama madai hayo yana ukweli au la. Uchunguzi wa NIPASHE uliofanyika wilayani hapa, umebaini kuwa waliokumbwa na kadhia hiyo ni pamoja na mtumishi wa idara ya mipango Barton Sinene, Naumu Tweve kutoka idara ya maji na Clemence Sanga ambaye ni Ofisa Mtendaji Kata (WEO) ya Bulongwa. Wengine ni Yusti Konga, Ofisa Mtendaji (WEO) wa Kata ya Mlondwe na Happy Mahenge ambaye ni Ofisa Mtendaji wa Kijiji (VEO). Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Imelda Ishuza alipotafutwa na NIPASHE kutoa ufafanuzi kuhusiana na sakata hilo, alikiri kuwa watumishi hao watano wamesimamishwa kazi na kupewa siku 14 za kujieleza kwa maandishi.

  “Ni kweli tuliwapa barua za kuwasimamisha na kuwataka wajieleze kimaandishi ndani ya siku 14 ambazo hata hivyo bado hazijaisha…Hawa wanatuhumiwa kujihusisha na mambo ya siasa kinyume na kanuni za kudumu za utumishi wa umma,”alisema Mkurugenzi huyo. “Sisi tunafanya uchunguzi wetu na kwakweli hatuna tatizo na wao ila tukibaini hawakufanya hivyo watarejea kazini kuendelea na majukumu yao,”alisema mkurugenzi huyo.

  Kutokana na hali hiyo, NIPASHE ilitaka kujiridhisha kuhusiana na sakata hilo na kufanya mahojiano na Ofisa Utumishi wa Halmashauri hiyo, Pius Gerace ambaye alikiri kuwa watumishi hao wamesimamishwa kazi kwa mujibu wa kifungu cha 21 (f) cha sheria ya mwaka 2009 ya kanuni za kudumu za utumishi wa umma.“Hii sheria tuliyotumia kuwapa mapumziko wakati ambapo Halmashauri inafanya uchunguzi wa kina kuhusiana na tuhuma hizo inaitwa Standing Order for Public Service,”alisema Gerace.

  Nipashe
   
 2. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #2
  Jun 1, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Hivi walikuwa wakiisaidia ccm au?:mod:
   
 3. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #3
  Jun 1, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Waliowasimamisha kazi ni wale waliowekwa na CCM, kwa hali ilivyo baada ya kupita Dr. kule na kuonekana wanamwunga mkono wamezuliwa ya uchaguzi wa mwakajana. Mbona wakuu wa mikoa na wilaya walioliwa wanapigia debe CCM hawajasimamishwa?
  Mwanasheria Mkuu wa Serikali alipigia debe kwa nguvu zote wakati wa Uchaguzi kutetea Kikwete, mbona hawamsimamishi?
   
 4. k

  kiloni JF-Expert Member

  #4
  Jun 1, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 575
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kama wangeisaidia ccm wangepewa UDC
   
 5. p

  politiki JF-Expert Member

  #5
  Jun 1, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  hivi mawaziri siyo viongozi wa serikali na mkuu wa hizo halmashauri si waziri ambaye naye anajishulisha na siasa au vipi? wafanyakazi wote wa seriakli walio na kadi za vyama mbalimbali vya siasa na pia si wanajishugulish na siasa au vipi? Rais wa nchi ambaye ni kiongozi mkuu wa hiyo serikali ni mwenyekiti wa chama cha siasa au vipi?? unawezaje kutenganisha siasa na serikali
   
 6. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #6
  Jun 1, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,709
  Trophy Points: 280
  Dah, democrasia bongo bado, na wale walogombea kwa ccm wakapigwa chini itakuwaje?
   
 7. t

  tweve JF-Expert Member

  #7
  Jun 1, 2011
  Joined: Jan 23, 2011
  Messages: 696
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  wamewaonea sana hawa wafanyakazi.mbona mkurugenzi wa wilaya ndiye alikuwa anafanya kampeni za kuinadi ccm wakt wa kazi ?sheria ya kazi inasemaje ?inakataza kushabikia vyama vya upinzani ama kushabikia vyama vyote muda wa kazi?ccm wanatapatapa .mwisho wao unakuja si muda mrefu.naamini Mungu wa haki atawapigania wote waliokumbwa na kadhia hii ya uonezi watapata haki zao na kurudi kazini.
   
 8. B

  Blessing JF-Expert Member

  #8
  Jun 1, 2011
  Joined: Apr 21, 2009
  Messages: 271
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi nauliza ingekuwa wafanyakazi wa ccm ingekuaje ??? Unajua ccm anakunyua nakupaka wenyewe --- ili iweje ????

  Nasema kunasiku na inakuja wataiona kitemaukuni hawa wanao wachisha kazi wandugu zetu.
   
 9. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #9
  Jun 1, 2011
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Kwani ma Dc sio wafanyakazi wa serikali mbona walikua kuutwa wakizunguka na wagombea wa ccm. Huyo DED *** **** nini. ? Mimi nafikiri taifa hili hadi tuchapane makofi ndio kuna karunguyeye watatia akili.!
   
 10. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #10
  Jun 1, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mie nalia na Lt Gen Shinbo na Bwana Twndwa mbona hawajasimamishwa na kutakiwa kujieleza
   
 11. p

  plawala JF-Expert Member

  #11
  Jun 1, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 627
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ukisaidia ccm ni sahihi,hata cheo unaweza kuongezewa,ukifanyia kampeni chama kingine ndiyo sheria inakula kwako
   
 12. SG8

  SG8 JF-Expert Member

  #12
  Jun 1, 2011
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 3,204
  Likes Received: 264
  Trophy Points: 180
  kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma za mwaka 2009 zinaruhusu mfanyakazi kujiunga na Chama cha Siasa ila haziruhusu kusimama jukwaani kuipinga serikali iliyopo madarakani. Watumishi pia hawaruhusiwi kufanyia siasa maeneo na wakati wa kazi, kuvaa sare za vyama vyao wakati wa kazi na kutoa huduma kwa kuwabagua watu kulinganan na itikadi zao. Aidha hairuhuisiwi kushika wadhifa wowote katika ofisi za Chama cha Siasa chochote. Kanuni za Utumishi serikalini za mwaka 2003 pia zinasisitiza jambo hilo.
  Kama watumishi hao walifanya kati ya hayo yanayokatazwa hapo juu basi wanawajibika bila kujali ni kupitia CCM. Kufanya siasa nje ya muda wa kazi sio kosa kisheria
   
 13. MWEEN

  MWEEN JF-Expert Member

  #13
  Jun 2, 2011
  Joined: Feb 6, 2010
  Messages: 472
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  Mbona kuna watumishi wa mashirika ya umma ambao ni madiwani? Kipindi kilichopita kulikuwa na Meya ambaye ni Profesa na hakuachia kazi yake chuoni! Je, hii ni sawa? Maomba mwongozo
   
 14. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #14
  Jun 2, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Mbona kuna watumishi umma kibao ni washabiki wa CCM. Na wengine ni viongozi wa chama na wanajulikana. Hebu watajeni?:mod:
   
 15. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #15
  Jun 3, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Nape anazunguka huku na huko kwa ajili ya CCM ameshautema uDC?
   
 16. Omuregi Wasu

  Omuregi Wasu JF-Expert Member

  #16
  Jun 3, 2011
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 753
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Achani kuonea watu!!
   
 17. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #17
  Jun 3, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,167
  Likes Received: 1,251
  Trophy Points: 280
  Mbona Nape ni Katibu Mwenezi CCM na anapita kila kona kubwabwaja hajasimamishwa ukuu wa Wilaya????

  Anyway Sumaye alisema " Anayetumia Kalamu kuchafua wenzake akiingia ikulu atatumia mtutu wa bunduki ama dola kuwanyamazisha wapinzani wake"
   
 18. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #18
  Jun 3, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,903
  Likes Received: 5,365
  Trophy Points: 280
  mimi ofisini magazeti yangu ni mwanahalisi,tz daima,mwananchi,na kuna baadhi ya watu washaanza kuniulizauliza,nasubiri barua ya kusimamishwa kazi ingawa sijawahi kufanya siasa ofisini,..i won't waiver,..
   
 19. tanga kwetu

  tanga kwetu JF-Expert Member

  #19
  Jun 3, 2011
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 2,165
  Likes Received: 1,125
  Trophy Points: 280
  wakuu ipo wazi kwamba, sheria hiyo ipo applicable ukishabikia CDM tu (sio CUF, sio NCCR-Mageuzi, sio CCM, sio TLP wala sio DP). ipo haja ya mtumishi mmoja kusaidiwa kisheria afungue kesi once wakimfukuza.
   
Loading...