Wapinzani ondokeni Bungeni rudini majimboni kwenu

GJHariohay

JF-Expert Member
Oct 24, 2013
1,026
2,000
Wanajamvi habarini.

Haya ni maoni yangu binfsi.

Awali ya yote naomba kuwa muwazi kwamba mimi ni miongoni mwa wasiopendezwa na jinsi nchi inavyoongozwa kwa sasa. Sikubali utawala huu kwa mambo mengi sana.

Kubwa zaidi ni mtawala kukataa katiba mpya ya wananchi ambayo yeye alikuwa mmojawapo wakati mchakato wake ulipoanza, lakini pia katiba inayotumika kama ni nguo imechakaa, ina viraka vingi sana. Jambo hili si la mzaha hata kidogo, kama ingekuwa gari basi katiba ingekuwa engine ya gari.

Hali ya maisha kuwa mbaya zaidi ni tatizo lingine, utawala umeshindwa kuzalisha ajira, uchumi umekuwa mbaya zaidi, gharama za maisha imepanda zaidi kiasi kwamba watu wamebaki kutafuta chakula cha tumbo tu badala ya kufanya maendeleo, uhusiano na mataifa mengine umekuwa mbaya, uhuru wa kuongea umekufa kabisa n.k n.k n.k.

Hayo ni machache kati ya mengi, lakini sasa naomba niende kwenye point.

Naomba kuwataka wabunge wote wa upinzani kuondoka bungeni moja kwa moja kama namna ya kushinikiza kupatikana kwa KATIBA MPYA.

Kuendelea kushiriki kwao bungeni itakuwa ni kubariki udhalimu wa serikali hii.

Nawaasa kurudi majimboni kwao, wapige story na wapiga kura wao, washirikiane ugumu wa maisha.

Ni hayo tu. Maoni binafsi.
 

cocochanel

JF-Expert Member
Oct 6, 2007
24,452
2,000
Tueleweshe wengine na sie juu ya katiba basi..

Akiikubali ni badaliko gani tutayaona? Na itakuwaje kwa sisi wananchi na nchi.

Mini napenda kujua lipi tunalikosa kwa sasa kwa sababu Raisi wa awamu hii hajakubali hiyo katiba ianze. Na awamu iliyopita kwanini haikuanza? Ilikuwaje?

Wabunge wao wanawezaje kuisukuma ikawepo.. yaani nani mwenye neno la mwisho kwamba hiyo katiba pendekezwa ianze kutumika? Na itaanzaje kwa tamko tu au?

Hao wapinzani wakitoka kuna faida gani kwa watu waliowapigia kura? Na unaona watatoka na kukosa pesa kulisha familia?

Nimeona umeandika kwa uchungu sana.. hivyo inaelekea unayajua sana kuindani.. nijuze nijue.
 
Top Bottom