mdesi
JF-Expert Member
- Jul 18, 2013
- 1,347
- 2,081
Mimi si mwandishi mzuri sana lakini nadhani mtapata mawazo yangu.
Hakika Wapinzani mkijipanga vizuri na kumuweka mtu makini anayeuzika katika kampeni za uraisi 2020 njia ni nyeupe sana kuingia mjengoni.Kura za makundi yote mnazo.
1.Kundi la waajiriwa wote: mkigusa kubadili sheria ya mifuko ya Jamii juu ya fao la kujitoa tuu; kura zao zoote mnazo, hakuna muajiriwa yeyote alifurahishwa na hii sheria mpya ya mafao uzeeni pamoja na kuunganisha mifuko yote na kubaki miwili na hivyo kupunguza ushindani na kulazimisha wafanyakazi kujiunga mifuko wasio itaka.
2. Elimu na afya, kuboresha elimu kwa kuwa ajiri walimu waliosota mtaani kwa mda mrefu (haikuzoeleka), afya ajiri madaktari, manesi waliosota mtaani kwa mda mrefu ilihali hospitali zinauhaba wa wataalamu wa afya, kuongeza madawa, miundombinu na vitendea kazi.
3. Fungua wigo wa ajira sekta binafsi kwa kuweka mazingira rafiki ya uwekezaji, kwa wageni na wazawa. Hapo soko la bidhaa litaongezeka automatically.
4. Uhuru wa kutoa mawazo, bila kuitwa mchochezi, Uhuru wa kujipatia habari mf.bunge live, kui challenge serikali iliyoko madarakani, ili kujiletea mabadiriko chanya.
5. Wakulima, kupanua soko la bidhaa kwa kufanya utafiti wa Masoko ya ndani na nje ya nchi, kuhakikisha pembejeo zinapatikana kiurahisi,kuongeza wataalamu wa kilimo ili kuongeza ubora wa mazao yenye ushindani ktk soko la kimataifa.
6. Maji safi, umeme na miundo mbinu mwingine.
Nyingine mtaongeza na kuziboresha. Hapo vyuma vimekaza ni byebye, wakulima bei za mazao zitapanda, wafanyakazi mishahara itapanda na kila mtu atafanya kazi kwa bidii.