Wapinzani ni washauri sahihi wa serikali, walimshauri Rais avunje baraza tukawapinga; naamini wanatonywa mengi

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
539
3,507
Wapinzani walipomwambia Rais avunje Baraza ateue na kuapisha upya niliikuwa mmoja wa waliodhani ni ushauri batili.

Wapinzani wakasema kuna watu walitaka Mhe. Rais asiapishwe nikawapuuza nakudhani wanataka kumtisha Mhe. Rais akose utulivu

Wakasambaza taarifa za sukuma Gang nikaona wanaanza kutuhubirisha ukabila.

Leo kwa kauli ya Rais nimeamini kwamba Hawa wanaoitwa wapinzani may be siyo wapinzani Bali ni washauri wa serikali. Wanayonena yanatimia,wanayotabiri yanadhihiri.

Natamani Mhe. Rais apunguze maadui Kwa kuwaachia wafungwa wote wa kisiasa waliopo ndani kwa sasa. Wapo waliowekwa mwaka 2020 na wapo waliowekwa yeye akiwa Rais, msamaha kwa watu Hawa utaimarisha Imani ya washauri wake( wapinzani) na Kila watakapotonywa na kubwabwaja yeye ataelewa Nchi IPO wapo. Leo hii baadhi ya washauri( wapinzani) hata wakiwa na taarifa muhimu wanaweza ingiwa na roho ya kusema acha yatokee.

Asipambane na maadui wawili Kwa wakati mmoja, yawezekana hao hao wanaotaka Ikulu 2025 ndio haohao walioweka watu ndani Ili Mhe. Rais aonekane KATILI na asiyemjua Mungu. Tupunguze maadui Vita hii Haina macho
 
Akivunja balaza na yeye ajivunje maana nae ni zao la hao mawaziri waliopo.
 
Back
Top Bottom