MADOTTO
Senior Member
- Dec 15, 2012
- 125
- 181
Nimekuwa nikifuatilia mwenendo wake bunge kwa jinsi linavyoendeshwa katika awamu hii.
Kwanza nakiri kuwa lugha zinazotumika wakati mwingine si lugha nzuri au niseme sio lugha za staha na kwa kweli si jambo jema hata kidogo.
Nikisema bila kupindisha maneno jambo hili kwa kiasi kikubwa linachangiwa na kiti HASA spika mwenyewe anapokuwa anaongoza kwa sababu zifuatazo:
1:Utakuta Mbunge wa CCM anatoa lugha ya kejeli, matusi na kashifa kwa upande wa upinzani na hata anapoombwa mwongozo au kupewa taarifa na wapinzani kuhusiana na kinachoongewa HUWANYIMA wapinzani nafasi hiyo na badala yake pindi mbunge huyo atapomaliza changia spika uanza chombeza kwa kumsifia mtoa matusi katika kuzidi wadhihaki wapinzani, hii si sawa kwani si mfano wa kiongozi bora na matokeo yake utakuta upinzani wanamua jibu mapigo na hapo kiti ndo uona kuna kosa limetendeka toka upinzani.
2:Upinzani pale wanapotoa hoja zao za msingi lakini spika anaziminya bila sababu ya msingi tofauti na jinsi CCM anavyowapa upendeleo, kwa namna yoyote vile wabunge wa upinzani inabidi wadai haki yao ambapo unakuta wananyimwa na matokeo yake unakuta Lugha zisizofaa zinatokea.
3:Spika mwenyewe kuwa mwanzo wa Lugha zisizofaa, mfano alipo mwambia Halima kikalishe uko, au pale unaona kabisha wagombea wa upinzani ni wanaume kisha unauliza tuambieni hapo nani ni mwanamke hapo.
Hakika pindi Spika utakapo jifunza kutotoa lugha kama hizo si rahisi kuitwa FALA.
4:Spika asipokuwa mbabe na kupindisha taratibu kwa ajiri ya kukibeba chama chake na kutoa haki sawa kwa wote HATOSKIA matusi,lugha za kuuzi au dharau juu yake.
Mzazi usitegemee mtoto akuheshimu kama wewe mwenyewe ujiheshimu na kumheshimu mtoto wako.
5:Akisimama mnadhimu wa Serikali wakati wowote lazima asikilizwe na taarifa yake au mwongozo atakaoomba utafanyiwa kazi mara moja ili pindi mnadhimu wa upinzani atakapo simama inakuwa mashaka matupu mara anyimwe nafasi mara ubabe, hapo ni vipi pasitokee kutoelewana.
Haki siku zote ujenga, bila haki na ubabe tegemea malipo yakudharauliwa na hao unaowataka wakuheshimu.
Kiti pindi kikitenda haki hakika nakuambieni Heshima kitapata bila kulazimisha, vinginevyo tutazidi waona wabunge wa upinzani wakinyanyaswa, dhihakiwa kama vile maadui kwelikweli.