Wapinzani na wanaharakati, andaeni maandamano ya amani kutaka uwazi wa mikataba ukiwemo wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo

Kuweka wazi mkataba siyo jambo rahisi kwa sababu za kibiashara muhimu kamati ya bunge ya miundo mbinu inaweza kuupitia kwa niaba yetu na pengine washirikishe jopo la wanasheria maarufu wakiwemo viongozi wa dini waangalie maslahi ya nchi.
unaongea kuhusu bunge gani? bunge 100% ni ccm , wengi wao hata la 7 hawakumaliza
 
Huu mraddi wa bandari ya Bagamayo siyo mradi wa kuingia kichwa kichwa. Kama serikali haitakuwa makini Huu utaturudisha utumwani, watakao uidhinisha huu mkataba wanatakiwa wafahamike kwa majina ili majina yao yaingie kwenye historia ya nchi yetu.
 
Lowasa alikuwa waziri mkuu na akasema katika kipindi cha kampeni kupitia UKAWA ya wakati huo kabla haijaharibiwa na akina amstwrdm kwamba akiwa rais huo mradi agavunja mkataba wake maana hauna maslahi kwa nchi.

Magufuli akiwa rais akisema amesitisha huo mradi kwa sababu kuna vipengele ni mzigo kwa taifa na akavitaja.

Wote hao ni viongozi wa kitaifa na walipinga huo mradi!

Wewe mbugilambugila una kipi cha kusaport huo mradi zaidi ya chuki zako za kijinga ukifikiri unamkomoa Magufuli?
huu mradi wa bagamoyo ni wizi mtupu, sidhani kaa mama samia anauelewa sawa, hii mradi ni hatari kwa taifa letu, ukome mara moja, uangaliwe umpya, mkataba uandikwe upya na uwekwe wazi kabla ya kutiwa sign
 
..kwanini mataga msiandamane kupinga mradi wa bagamoyo?

..kila jambo baya mnasubiri lipingwe na vyama vya upinzani?

..naona ktk hili mnakimbia wajibu wenu.
Hao wanasubiri "kupozwa" wafunge midomo, midomo yao ni strategy.
 
Kuweka wazi mkataba siyo jambo rahisi kwa sababu za kibiashara muhimu kamati ya bunge ya miundo mbinu inaweza kuupitia kwa niaba yetu na pengine washirikishe jopo la wanasheria maarufu wakiwemo viongozi wa dini waangalie maslahi ya nchi.
Sisi tunaiga nchi zilizotutangulia, hakuna nchi inayofanya hivyo hapa duniani/Afrika?

Kamati ipi ya bunge? Kwa wabunge wapi? Hawa waliopitisha mikataba ya gesi usiku kwa usiku? Hawa wanaoshangaa sheria kandamizi zilizopitishwa na bunge? Hawa walipitisha kodi za kizalendo zisizowagusa wao? Hawa walioukataa mradi wa bandari ya bagamoyo jana na leo wanautaka?

Viongozi wa dini wapi hao? Wale waliopokea zawadi ya Rugemalira? Au hawa waliopo bungeni leo?

Wanasheria wapi? Wakina Chenge wa vijisenti?

Waweke tu hadharani, wote tujue, kama inaliwa wote tujue inaliwa na hatuna cha kufanya baaaasi, tuendelee kuwa mazoba hivi hivi.
 
Wakati magufuli anaukataa hadharani alianisha japo kwa mdomo,mapungufu yaliyopo mule.

Sijui ni nani alitafuta mwekezaji yule,na kwa lengo gani!

Trillion 21 tsh ni pesa nyingi sana mtu kuwekeza halafu asiweke mazingira ya hiyo pesa kurudi.

Magufuli ali sound logically zaidi.

Bado ukweli wa uwekezaji huo una maswali mengi sana.
Jiwe ni muongo na lagahi kama shetani, usimuamini kwa lolote
 
Naomba nitoe wito kwa wanasiasa upinzani pamoja na wanaharakati, waombe kibali cha kufanya maandamano ya amani kushinikiza uwazi wa mikataba ukiwemo mkataba wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo.

Mradi huu ni mkubwa sana na kwa maana hiyo, unaweza kuleta matokeo makubwa kwa nchi yetu ambayo yanawe kuwa ni chanya( positive) au hasi(negative) kwa nchi yetu9 hivyo hatupawi kukaa kimya.

Mradi huu ukiwa na matokeo chanya, utafaidisha mpaka vitukuu wetu, na ukiwa na matokeo hasi, basi utaathiri mpaka vitukuu wetu pia kwahiyo ni lazima sisi wananchi tushirikishwe.

Tungekuwa na Bunge imara, tungeshirikishwa kupitia wawakilisha wetu (wabunge) , ila kwakuwa hatuna Bunge la aina hiyo(kwa mtazamo wangu), basi mkataba uwekwe wazi kwa umma na wananchi tutoe maoni yetu kama mradi huo uanze au vinginevyo.

Kamwe tusiwaachie wanasiasa waaamue peke yao jambo kubwa na nyeti kama hili hasa ukizingatia wanasiasa wetu wmekosa msimamo katika mambo nyeti kama haya. Zaidi wao huangalia watawala wameegemea upande gani na wao huunga mkono mawazo yao.

Kujadili huu mradi pasipo kujua nini hasa kimo katika huo mkataba huku wengine wakiupinga na wengine wakiutetea,ni uwendawazimu na ujinga mtupu na zaidi ni kupotezeana muda.

Bila shinikizo, tutajadili wee halafu tutachojadili hakitabadilisha kitu chochote, na mwisho wa siku, wataingia makubaliano wanayoyajua wao huku sisi tukibaki kuomba Mungu mkataba uwe fair kwa pande zote( kelele zote hizi zitakuwa ni sawa na kelele za chura ambazo hazimzui Tembo Kunywa maji).

Hivyo, natoa wito wa kufanyika maandamano ya amani kutaka uwazi juu ya mkataba huu vinginevyo tukubali matokeo hapo baadae.

Kumbukeni ya gesi ya Mtwara na maneno mazuri ya watawala wakati ule- Tanzania ya uchumi wa gesi.
We nae hujulikani unataka nini, pole Sanaa mkuu
 
Kile kipengele cha mchina kumiliki ardhi miaka 99 alichosema JPM kinatisha.mchina akifanikiwa tuu basi kwingine utakapo kopa utaambiwa nao wnataka ardhi kama ulivyompatia mchina au hatukupi mkopo je tutaishia wapi? sasa ni wangapi ambao tutakao kopa na kuwapa ardhi miliki miaka 99? je mwisho wa siku watoto wetu watamiliki kipande gani cha ardhi? hii ni lazima iwekwe wazi tujue mkataba huo utatuletea keki au bange?
 
We endelea kutetea CCM iliyotufikisha hapa.
Salary slip huyu mama anawapa chadema rushwa ndogo ndogo ,ili mkae kimya.Mara Mbowe arudishiwe pesa zake.Mara Lissu alipwe pesa zake.Kumbe anataka kutengeneza mikataba ya kifisadi kama JK.Niwaulize.Tanzania inaongoza kwa uzalishaji wa gesi.Je,mtwara na Lindi wanafaidika chochote.?Kwa sababu ya JK .
 
Kuna maswali mengi sana ya kujiuliza au kuuliza wanaoandaa kuuangalia upya mkataba wa ujenzi wa bandari ya Bagamoyo.
1. Je hii siyo furahisha Kikwete?
2. Je tunashindana kimikoa?
3. Wanaoungalia upya ni wepi? walioshiriki kuunda kipindi cha Kiwete au walioshiriki kuusimamisha kipindi cha JPM?
4. Kama ni wapya wametokea wapi na wana sifa gani?
5. Je vetting ilifanyika?
6. Kamati za Bunge zitahusishwa?
7. Vyuo vikuu vitahusishwa?
8. Mabalozi wetu kwenye nchi jirani zilizoingia mikataba kama hiyo ambayo leo hii inawatesa wanashiriki kutoa ushauri? Je wanafahamu lolote? Wamepewa kazi ya kutafuta undani wa mikataba iliyoshindikana?
9. Wastaafu serikalini wamepewa nafasi ya kutoa ushauri?
10. Watakao upitisha huu mradi wapo tayari kuweka majina yao wazi wananchi wawafahamu?
11. Kama viongozi wanaamini ni wenye manufaa kwa Taifa, Je serikali iko tayari kuuweka wazi mkataba wananchi watoe maoni yao?
12. Mkataba sensitive namna hii unaotishia kuturudisha utumwani, viongozi wako tayari kukubali pindi watokapo madarakani na ikathibitika kwamba mkataba hauna manufaa kwa nchi watakuwa tayari kuondolewa kinga zao na kukubali kufunguliwa mashtaka?
13. ....Je itafanyika tathmini makini ya kuonyesha itakavyoathiri bandari za Tanga, Dar, Mtwara? Kuonyesha kwanini si bora kuzipanua hizo zilizopo badala yake kupendekeza kuingia mkataba huu hatari?
14.......

Endelea
 
Ni kweli kabisa, ila kwa sasa kupata kibali itakua ngumu sababu tushatangaza uwepo wa wimbi la tatu la Covid -19
 
Back
Top Bottom