wapinzani na CCM acheni kutuzingua kwny katiba mpya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

wapinzani na CCM acheni kutuzingua kwny katiba mpya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by eliesikia, Nov 13, 2011.

 1. eliesikia

  eliesikia JF-Expert Member

  #1
  Nov 13, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 423
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 45
  sijaona nia ya kweli ya kupata katiba halisi ya mwananchi zaidi ya wanasiasa uchwara wa kitanzania kutetea maslahi yao.. wao ni tume huru na mamlaka ya raisi kutwa nzima.. kamwe wananchi wanyonge tusikubali kupewa kiini macho wakatimiza kiu yao ya madaraka.

  naomba kwa pamoja tuungane na kudai:
  pensheni kwa kila mfanyakazi eg. madereva na wakulima. madereva kama wa daladala hawana mshahara lakini kwa nini wamiliki wasitoe hela kipande hata cha siku moja kwenda kwenye pensheni ya huyu dereva ili akistaafu aweze kujikimu?

  tuweke ukomo wa mwananchi mmoja kumiliki ardhi kubwa peke yake. tukubaliane kuwa kila mwananchi atakuwa na kiwango cha juu cha ardhi eg. eka 20 ili kila mtu apate na si matajiri peke yao. katiba itoe mamlaka ya ardhi kwa mamlaka ya kijiji ili wawekezaji uchwara wasipewe ardhi mpaka baraza la kijiji litakapoidhinisha

  mimi najua mambo haya ni machungu kwa ccm na wapinzani kwa kuwa wao ndio matajiri mitaani ardhi na daladala na magari ya biashara kama safaris na hotel ni zao... wananchi tuungane tuwalazimishe hawa wanasiasa watengeneze ratiba ya kwetu wanyonge na si vinginevyo...
   
 2. simplemind

  simplemind JF-Expert Member

  #2
  Nov 13, 2011
  Joined: Apr 10, 2009
  Messages: 11,800
  Likes Received: 2,571
  Trophy Points: 280
  Zipo ishara serikali inayo nia ya kufanya mchakato wa katiba mradi wake. Nia hasa ni kulinda masilahi ya wachache . Nia ya serikali kubaka uundwaji wa katiba mpya ni lazima upingwe kwa nguvu zote na ikibidi kuazishwe mchakato mbadala(people driven parallel constitituion review process ) ambao utahusika moja kwa moja kukusanya maoni ya wananchi. Kuburuzwa basi !
   
Loading...