Wapinzani msitufokee, watanzania sio wasahaulifu kiasi hicho

Amani Msumari

JF-Expert Member
Aug 21, 2016
1,830
976
Wanajamvi,

Kumbukumbu zangu zimenichukua mpaka kwenye miaka 5 ya mwisho ya utawala wa Mzee Kikwete, yaani 2010 - 2015. Nimejaribu kupitia vyanzo mbalimbali pamoja na kumbukumbu zangu binafsi kuhusu zipi hasa zilikuwa ajenda za wapinzani.

Wapinzani walipigia kelele sana suala la rushwa (ufisadi), Kukuza uchumi kwa kuhakikisha wanaimarisha shirika la ndege, reli, bandari n.k
Waliongea pia kuhusu madini na jinsi watakavyofumua mikataba ya madini
Hawakuishia hapo, waliahidi elimu bure mpaka chuo kikuu.

Uchaguzi ukafika 2015 na watanzania wakaamua Dr. John Magufuli ndio awe nahodha. Tangu hapo, Rais. Magufuli ametekeleza kwa ufasaha ilani ya uchaguzi ya CCM ya 2015 - 2020 na akaenda mbali kutekeleza Yale yote wapinzani waliyoahidi. Ukiacha elimu bure mpaka chuo kikuu, ni kipi hajafanya? Hata Hilo la elimu bure mpaka chuo kikuu limefanyika kwa mtindo mwingine. Unapomkopesha mtoto wa masikini ili asome, maana yake umemuwezeshea kufikia ndoto zake na hapohapo kulisaidia taifa kwa kuhakikisha linapata wataalamu wa kutosha.

Rais Dr. Magufuli aliweka bayana, mpaka 2020 Upinzani utakuwa umekufa Tanzania, wasioelewa walitafsiri watakavyo ila kifo hicho kilitabiriwa kutokana na ukweli kuwa alijipanga, na amefanikiwa kutekeleza kile watanzania walio CCM na Upinzani walichotaka. Je, hapo kutakuwa na Upinzani tena?

Hebu niambieni, wapinzani wanna ajenda gani ya maana mwaka huu? Mnawasikia Tena wqkiongelea ajenda ya ufisadi?

Nataka niwakumbushe wapinzani kuwa watanzania tunakumbuka kuwa waliiacha ajenda ya ufisadi tangu balozi Dkt. Slaa alipowachomoka pyuuu. Sasa hawana nyimbo.

Mgombea wao alikubali kula matapishi yake kwa kumpokea mtu aliyewaaminisha watanzania kuwa ni fisadi. Alikaa kimyaaaaa, mbona hakuonesha hayo makeke. Duru zinaarifu kuwa ukiacha balozi Dkt. Slaa ambaye alipinga hadharani, Mnyika inaaminika kuwa alikwazwa sana.

Hatujasahau kuwa ni yeye mgombea wao aliyeshadadia Mwami afukuzwe chamani kwa kutamani kiti. Demokrasia anayoihubiri iko wapi? Kama alishindwa kutuonesha hivyo tangu awali, tutamuaminije sasa?

2020 kura yangu ni kwa John.
 
Wanasema kwenye shimo la nyoka,mwagia mafuta na nyoka mpaka wadogo wa siku moja wote watatoka. Lissu hajaawasha gari la kampeni,mataga mnakurupuka,je muziki munene full wa Zitto,Lissu,Mdee,Mbowe,Msigwa,Heche,Mnyika na wengineo mtakuwa na hali gani?
Ushauri wa bure,tembeeni na pain killers na vidonge vya kushusha pressure.
 
Kwa kujitoa akili hamjambo, eti wapinzani wameacha agenda ya ufisadi!! Hukawasikia na madai ya trilioni 1.5 iliyfukuzisha kazi CAG Asad?
 
Wapinzani hawakuahidi kuteka, watu kuokotwa kwenye viroba, kupotea 1.5 trl, wala kutopandishwa madaraja na kuboreshwa kwa maslahi ya watumishi umma. Sasa wewe unasema vipi awamu imefanya yale wapinzani waliyoahidi.
Huna hoja
 
...milioni 50 kila kijiji
Zimetoka zaidi ya hizo kupitia TASAF, benki ya maendeleo ya Kilimo na mikopo kwa vikundi mbalimbali
Mkuu unaishi nchi gani? Hayo yote ni usanii tu, hakuna hata moja limetekelezwa, rushwa imejaa mpaka inakera, watia nia wao wote wa mwaka huu wametoa rushwa ili kununua wajumbe, milioni hamsini za kila kijiji na laptop za walimu ziliota mbawa, awamu hii ni ya kisanii zaidiView attachment 1534412😭😭
Unaposema wote unamaanisha nini?
 
Tuliona jinsi Balozi Dkt. Silaa alivyoonesha msimamo wake na kukataa kula matapishi yake. Mgombea wenu alisimamia wapi ili tuone kweli ana msimamo?
 
Zimetoka zaidi ya hizo kupitia TASAF, benki ya maendeleo ya Kilimo na mikopo kwa vikundi mbalimbali
Ilitamkwa milioni 50 kila kijiji, wala haikutamkwa zitapitia TASAF, benko ya maendeleo nk. Au unadhani kila mwanakijiji ana sifa za kunufaika na TASAF? Hatujasahau...!
 
Ilitamkwa milioni 50 kila kijiji, wala haikutamkwa zitapitia TASAF, benko ya maendeleo nk. Au unadhani kila mwanakijiji ana sifa za kunufaika na TASAF? Hatujasahau...!
Ulifikiri zitaendwa kumwagwa Kama pipi? Hapana, wamepewa wale wenye uhitaji na bado kazi inaendelea
 
Back
Top Bottom