Uchaguzi 2020 Wapinzani msimuamini sana Membe kwa yoyote atakayosema na kuyatenda kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu baadae mwaka huu

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,011
144,371
Mwanasiasa ambae anaweza kujiamini kusema na kufanya lolote kwa lengo la kukosoa watawala waliopo madarakani bila hofu ya kushitakiwa,mali zake kutaifishwa au kunyang'anywa,n.k ni yule tu ambae wakati alipokuwa kwenye system, hakuwahi kutuhumiwa kufanya ufisadi,wizi,kujihusisha na rushwa,kujilimbikizia mali na vitendo vingine ambavyo ni kinyume na sheria za nchi.

Binafsi naamini Nyerer tu ndie aliekuwa na sifa hii na ndio maana aliweza kuwakosoa watawala bila hofu ya kuumbuliwa au kufanyiwa mizengwe ila kwa waliobaki, sijui kama yuko mwenye sifa ya aina hii au walau ya kufanana na sifa alizokuwa nazo Baba wa Taifa.

Kwa msingi huu,kama Membe ni mmojawapo ya watu wenye sifa kama za Mwalimu Nyerere,basi mnaweza kumuamini, vinginevyo, kuweni makini nae sana na mjiulize sana ujasiri huu anaouonyesha ni wa kweli au kuna kilicho nyuma yake kabla ya kufikiria kumpa nafasi yoyote katika vyama vyenu na hasa ya kuwa mgombea katika uchaguzi wa baadae mwaka huu iwapo ataonyesha ni ya kutaka kuhamia katika vyama vyenu.

Sometimes in life, it worth to be curious when others are satisfied,and to be dissatisfied, when other are curios.
 
Naunga mkono hoja, ni heri mkashindwa kwenye uchaguzi kwa sababu zingine za wazi au kuonewa kuliko tuje kuambiwa alikuwa pandikizi.
UPINZANI UTAFIA HAPO
Wanaweza kabisa kumuacha aongee au atende atakavyo ili muamini kweli ni mwenzenu kumbe wana agenda zao, hivyo wapinzani wafanye kazi ya ziada kujua ukweli kuhusu Membe na misimamo yake kabla ya kumuamini kwa asilimia 100.
 
Mkuu, hakuna sababu ya kumwogopa Membe, au yeyote atakayejitoa CCM na kutaka kusaidia juhudi za kukiangusha chama hicho.

Nina hakika watu hawa wapo wengi tu kwa sasa hivi.

Kinachotakiwa ni kwa upinzani kuwapa majukumu na malengo ya kazi zao za kuiangusha CCM bila ya kuwapa nafasi za uongozi ndani ya vyama vyao.

Malipo ni baada ya kazi, na sio kabla.

Yeyote atakayekubaliana na hili akaribishwe kwa mikono miwili na awezeshwe kufanya kazi zake kwa ufanisi.

Utakataaje msaada kama huo?
 
Simuoni kama ana nafasi mbele ya Lissu, Lissu is the best.
Mkuu 'denoo J', Membe anao msaada sana CHADEMA wakimtaka, na nawashawishi wamtake.

Kwani Lissu hawezi hata kumteua awe waziri baada ya kazi kubwa atakayokuwa ameifanya kwenye kampeni?

CHADEMA wakati huu ni wa kuwakaribisha kwa wingi, wote walioko ndani ya CCM wakiwa hawana furaha kutokana na chama chao kubinafsishwa na mtu mmoja. Waende CHADEMA wakafanye kazi, na uteuzi watapewa, kwani nafasi zitakuwepo nyingi zitakazohitaji kujazwa.
 
One of the biggest problem ya Membe ni kwamba huyu ni TISS na kwa nchi yetu hii huwezi kamwe kuitenga TISS na CCM...
Lingine ni kwamba TISS ni kazi ya kudumu hasa kwa level ya Membe... Anaweza kuwa nawe kwa muda tuu lakini mambo yakienda mrama si mwenzako tena.. Atarudi kwenye asili yake

Zaidi Membe yuko kisiasa zaidi kuliko kiutendaji.. Anaongea sana na ni mwepesi wa kufunguka huku akiwa hawezi kuficha hisia zake... Hawezi kabisa kubaki kwenye neutral point ili kuficha misimamo yake kwenye baadhi ya mambo

Jr
 
ukichagua kumuamini mwana siasa. .ni sawa na kumuoa kahaba huku ukiweka imani kwamba atakua muaminifu katika ndoa yenu
 
Sioni sababu ya kutomuamini kabisa.

Ila kutomuamini sana ni sahihi. Maana yake ni kwamba wamuamini 'kidogo' na kuwe na mpango mkakati na mathubuti wa kumuamini huko.

Kiwango hicho 'kidogo' cha kumuamini ni vyema kishabihiane na nafasi ambayo atakuwa amekabidhiwa ndani ya chama ili kusiwe ama kusilete madhara makubwa hapo baadaye.
 
Back
Top Bottom