John Mnyika
JF-Expert Member
- Jun 16, 2006
- 712
- 1,240
Mnyika,,,
Kama unavyofahamu mimi sio pendera fuata upepo,,,sikubali mambo kirahisi rahisi. Hebu naomba definition ya tume huru!!!
NB:
Remember Zanzibar walitafsiri tume huru kwa namna yao,,, Bunge la Jamhuri likatafsiri kwa namna nyingine,,,
Kilitime:
Tume Huru ni dhana pana. Ni zaidi ya kuwa na wapinzani katika Tume ya Uchaguzi. Nimeshawahi kuandika kuhusu suala hili- ukitaka kujua mtazamo wangu bonyeza hapa: http://www.chadema.net/habari/misc/misc_10.html
JJ
Maoni yangu ni pamoja na-
Tume ya uchaguzi si huru: Kwa nini?
Kwa mara ya tatu chini ya mfumo wa vyama vingi; Tume ya Uchaguzi ilisimamia na kuratibu uchaguzi mwaka 2005 kwa kutumia uzoefu ilioupata katika chaguzi za mwaka 1995 na mwaka 2000. Kwa ujumla Tume ya Uchaguzi iliendesha vizuri zaidi uchaguzi uliopita ukilinganisha na chaguzi zilizotangulia lakini bado mchakato wa uchaguzi haukukidhi vigezo vyote vya uchaguzi huru na haki.
i. Mifumo ya kisheria na kiuchaguzi kwa ajili ya uchaguzi na Muundo wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi
Pamoja na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania sheria mbalimbali zimekuwa zikisimamia uchaguzi hususani: Sheria ya Uchaguzi na. 1 ya mwaka 1985; Sheria ya Vyama vya siasa na. 5 ya mwaka 1992 na Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambazo zimetoa mamlaka kwa tume kusimamia na kuratibu uchaguzi ikiwemo kutoa maelekezo na taratibu mbalimbali.
Muundo wa Tume ulichukua mfumo ule ule ambao ulitumika katika uchaguzi mkuu 2005 unatokana na Katiba Kifungu 74(1) kama ilivyofanyiwa marekebisho na Sheria na. 4 ya 1992 na Sheria na. 7 ya mwaka 1993; Tume inateuliwa na Rais(Katiba na Sheria husika zimeeleza sifa za wanaoweza kuteuliwa). Mkurugenzi wa Uchaguzi naye anateuliwa na Rais kwa mapendekezo ya Tume. Katiba kifungu 74 imebainisha majukumu ya Tume ya Uchaguzi. Vyama vya siasa viliendelea kudai tume huru ya uchaguzi wakati wa marekebisho ya 14 ya katiba yaliyofanyika karibu na uchaguzi mkuu. Hata hivyo suala la muundo wa tume huru ya uchaguzi halikujadiliwa wala kuingizwa kama sehemu ya marekebisho hayo. Matokeo yake maandalizi ya uchaguzi yalifanywa na tume ile ile ambayo ilisemwa kipindi chote kwamba haiko huru. Kamati mbalimbali ziliundwa na kufanya kazi kipindi cha uchaguzi pekee.
Nini kifanyike ili pawe na Tume huru:
Pawepo na Sheria ya Tume ya Uchaguzi ili kuipa uhuru na mamlaka zaidi tume ya uchaguzi kama ilivyo katika nchi kadhaa za Kusini mwa Afrika.(Pendekezo hili limetolewa pia na Tume ya Uchaguzi na Vyombo mbalimbali vya Ufuatiliaji/Uangalizi wa uchaguzi)
Kamati za Tume ziwe ni za kudumu; ziendelee na kazi hata baada ya uchaguzi. Vitengo vya TEKNOHAMA (ICT) na Elimu ya Uraia view sehemu ya vitengo vya kudumu vya Tume.
Katiba na Sheria vifanyiwe mabadiliko/marekebisho ili kutoa uhuru na mamlaka ya Tume ya Uchaguzi wa Kuzingatia vigezo vya Kanuni/Matamko na Misingi mbalimbali ya Uchaguzi ya Kimataifa ambayo taifa letu limeridhia. Baadhi ya masuala mahususi ni pamoja na: Tume iwe nje ya mfumo wa kiutendaji wa kiserikali(Watendaji wa Serikali kama Wakurugenzi na Watendaji wa Kata wasiwe watumishi wa Tume ya uchaguzi hata wakati wa uchaguzi); Wajumbe wa Tume wachaguliwe kwa mashauriano na Wadau wengine vikiwemo vyama vya siasa na baadaye wathibitishwe na Bunge; Utumishi wa Wajumbe waandamizi wa Tume wa ulindwe(durability and security of tenure) kisheria na kikatiba kama walivyo majaji; Uwakilishi wa Tume uzingatie jinsia, uwakilishi wa kijamii na makundi rika; Tume ya Uchaguzi iwajibike kwa Bunge badala ya Kuwajibika kwa Serikali; Tume ya Uchaguzi iwe na Bajeti inayojitegemea itakayopitishwa moja kwa moja na Bunge.
ii. Rasilimali kwa ajili ya usimamizi wa uchaguzi na Usimamizi wa Uchaguzi
Tofauti na chaguzi za 1995 na 2000, katika uchaguzi mkuu 2005 fedha za uchaguzi kwa ajili ya shughuli za uendeshaji wa Tume ya Uchaguzi zilitolewa katika wakati mwafaka na sehumu kubwa zilitolewa na serikali. Kupungua kwa utegemezi kwa wahisani katika kutoa fedha za kusimamia uchaguzi pamoja na kutoa fedha mapema vilisaidia kuboresha uendweshwaji wa uchaguzi.
Uhusiano katika ya vyama vya siasa na Tume ya Uchaguzi katika ngazi ya Taifa ulikuwa mzuri; vyama vilialikwa katika vikao mbalimbali na vilikuwa na wajumbe katika kamati mbalimbali za tume ya Uchaguzi. Hata hivyo, malalamiko yametolewa baadhi ya maeneo hususani yale yaliyokuwa na upinzani mkali kwamba vyama havikushirikishwa ipasavyo na watendaji wa tume ya taifa ya uchaguzi ngazi ya wilaya, majimbo na kata. Wakati wa kampeni watendaji hawa wameonekana kuegemea chama tawala. Hali hii iliendelea katika maeneo mengi hata katika hatua za kuhesabu kura, kujumlisha kura na kutangaza matokeo hususani katika ngazi za majimbo. Katika mfumo wa tume hakuna utenganisho kati ya usimamizi na utekelezaji katika muundo wa tume ngazi za chini ya makao makuu ya tume. Uteuzi wa watendaji wa chini ulifanywa na wasimamizi wa uchaguzi ambao ni watekelezaji(ambao walikuwa ni watumishi wa serikali) badala ya chombo huru cha kusimamia uchaguzi hivyo walitumiwa na dola kupika ama kuchezea matokeo.
Tume ya Uchaguzi iwe na watendaji wa Kudumu katika ngazi mbalimbali; utaratibu wa kuwatumia maofisa wa serikali kama wasimamizi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi usitishwe.