Kitila Mkumbo
JF-Expert Member
- Feb 25, 2006
- 3,354
- 1,944
CCM yashinda viti vingi vya madiwani wapinzani watamba mijini
Na Waandishi wetu
CHAMA ha Mapinduzi (CCM) kimepata viti vingi vya udiwani kati ya vivyokuwa vinagombewa katika uchanguzi mdogo uliofanyika nchini juzi, huku wapinzani wakitamba kwenye kata za mijini. Mpaka sasa CCM imepata viti vitano na wapinzani viti vinne.
Kutoka Arusha Mussa Juma, anaripoti kuwa Umoja wa Wapinzani, umeibwaga Chama CCM katika uchaguzi mdogo wa udiwani Kata ya Sombetini ambao nusura uvurugwe na polisi kufuatia kupiga mabomu ya machozi kuwatawanya watu waliokuwa na jazba wakisubiri matokeo.
Uchaguzi huo uliofanyika baada ya kiti cha udiwani wa kata hiyo kuwa wazi baada
ya aliyekuwa diwani wa kata hiyo, Mussa Mkanga (CCM) 'kuenguliwa' kwa madai ya
kuhusika na ugawaji wa kiwanja cha wazi kilichopo eneo la kilombero kwa kampuni
ya EMOIL Marketing Ltd kinyemela mapema mwaka huu.
Katika uchaguzi huo mgombea wa TLP, Alphonce Mawazo Chemu aliibuka mshindi kwa kupata kura 1515 wakati mgombea wa CCM, Fabian Gabriel Mhindi aliambulia kura 1473.
Kabla ya Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi huo ambaye ni Afisa Mtendaji wa kata hiyo,
Juma Kitumbo kutangaza matokeo hayo, wafuasi wa vyama vya upinzani walishinikiza
kutangazwa kwa matokeo hayo hasa kutokana na kujua kuwa wameshinda lakini
msimamizi huyo mara zote alikuwa akihaha kutoa majibu huku akipokea simu mbali
mbali.
Hali hiyo ilisababisha kuibuka kwa vurugu zilizosababisha askari polisi kitengo
cha Kuzuia Ghasia (FFU) kutinga katika Ofisi ya Mtendaji eneo la Mbauda, majira ya
saa 12.30 jioni wakiwa na silaha za moto tayari kukabiliana na hali hiyo.
Hata hivyo giza lilivyozidi kutanda, wafuasi hao wakionekana kuwa na furaha
iliyochanganyika na wasiwasi wa kuporwa kura zao, wakiwa nje ya ofisi hiyo
waliendelea kuimba nyimbo za kumshinikiza msimamizi wa uchaguzi wa kata hiyo
kutangaza matokeo hayo, huku viongozi wa vyama vya upinzani wakilinda masanduku ya
kura.
?Hakuna kulala?tunataka matokeo?msije kupora kura zetu kama ilivyokawaida
yenu,? hizo ni sehemu za nyimbo walizokuwa wakiimba wafuasi huo huku mashabiki wa
CCM akionekana kujikusanya vikundi, vikundi wengine wakiwa nje ya Ofisi ya chama
hicho iliyoko karibu na Ofisi ya Kata.
Umati wa wafuasi hao ulizidi kuongezeka kadri saa zilivyozidi na ilipofika saa 1
usiku askari hao walianza kuvurumisha mabomu ya machozi ovyo hali iliyosababisha
watu kukimbia huku na kule kusaka maji ya kuosha macho yao ambapo walilazimika
kunawa miferejini.
Hali hiyo ilidumu kwa saa tatu hadi saa 4.30 licha ya msimamizi wa uchaguzi huo
kutangaza matokeo majira ya saa 2.45 usiku, ambapo viongozi mbalimbali wa vyama
hivyo wakishuhudia akiwemo Msimamizi wa Uchaguzi wilaya, Job Laizer ambaye pia ni
Mkurugenzi wa Manispaa ya Arusha.
Wafuasi hao wa vyama vya upinzani, walitawanyika na kuendelea na shamrashamara za
ushindi huo, ambapo jana mchana walitarajiwa kufanya sherehe katika viwanja vya
Ngusero kushehekea ushindi huo.
Naye Jospeh Senga anaripoti kutoka Songea anaripoti kuwa, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeshinda kwa kishido katika Kata ya Majengo katika uchaguzi mdogo uliofanyika jana katika Kata hiyo iliyoko katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea, Mkoa wa Ruvuma.
Mgombea kwa tiketi ya Chadema Idd Ibrahim aiyekuwa akiungwa mkono na vyama
vya TLP, NCCR-Mageuzi na CUF alipata kura 1,015 kati ya kura halisi 1,569
zilizopigwa na Halfan Kigwenembe wa CCM alipata kura 554. Jumla ya kura
zilizopigwa ni 1,581 na zilizoharibika ni 12.
Kwa matokeo hayo Msimamizi wa uchaguzi huo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Manispaa
ya Songea, Edigar Berege alimtangaza Idd Ibrahim kuwa mshindi.
Tofauti na chaguzi zingine ambapo wanawake wanakuwa wengi, katika uchaguzi huo idadi kubwa ya wanaume na vijana walijitokeza wingi kupiga kura.
Ulinzi mkali ulikuwepo katika uchaguzi huo,Kamanda wa polosi wa Mkoa wa Ruvuma,Falhum Mshana na Mkuu wake wa polisi wa Wilaya ya Songea walikuwepo kutokana uchaguzi huo kuvuta hisia za watu wengi.
Baada ya kura kuhesabiwa na matokeo kubandikwa kwenye vituo vya kupigia kura
wafuasi wa vyama vya upizani walianza kushabgilia
Kutoka Muheza, Tanga, Steven William anaripoti kuwa,? CCM imeibuka kidedea baada ya kushinda kwa kishindo katika? uchaguzi mdogo wa udiwani katika Kata ya Masuguru baada ya mgombea wake, Dorothi Kihampa kupata kura nyingi.
?
Uchaguzi huo mdogo ulihusisha?wagombea wa?vyama vitano ambavyo ni CCM, CUF, Chadema, UDP na TLP.
?
Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo majira ya saa mbili usiku katika Shule ya Msingi Masuguru ambako kura zilihesabiwa, Msimamizi wa uchaguzi huo ambaye ni ?Mkurugenzi wa Halmashauri ya Muheza, Ephireem Kalimawendo, alimtangaza Kihapa wa CCM kuwa mshindi kwa kupata kura 720 akifuatiwa na Awadhi Mjenga wa CUF, alipata kura 363,Chombo Ahamedi (Chadema) kura 9, Yusuphu Salimu (UDP) kura saba na Maiko Muhina waTLP aliyeambulia kura 2.
?
Baada ya matokeo hayo kutangazwa na Mkurugenzi huyo sherehe za maandamano ya CCM zilianza kutoka katika Shule ya Msingi Masuguru hadi Ofisi ya CCM Wilaya ya Muheza ambapo kulikuwa na sherehe.
Naye Abdallah Nsabi kutoka Maswa anaripoti kuwa, CCM imeibwaga CUF katika kinyanganyiro cha udiwani wa Kata ya Nguliguli kwa kunyakua kiti hicho.
Akitangaza matokeo hayo Msimamizi wa Uchaguzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halimashauri ya Wilaya ya Maswa, Gabriel Fuime, alimtangaza mgombea wa CCM Petro Mashara kuwa mshindi baada ya kupata kura 2,222 dhidi ya mgombea wa CUF Jibusa Karaja aliyepata kura 828.
Amesema kuwa uchaguzi ulifanyika kwa kufata taratibu zote za uchaguzi na idadi ya
wapiga kura 3117 walijitokeza kupiga kura na kura 67 ziliharibika na kwamba hakuna malalamiko yoyote yaliyojitokeza katika uchaguzi huo na kila chama kilikubaliana na matokeo hayo.
Akizungumzia matokeo hayo, Mwenyekiti wa CCM, Hamis Mgeja alisema ushindi uliopatikana umetokana na mshikamano uliokuwepo kati ya wanachama na viongozi wa achama hicho na kisha kuwapongeza wapinzani wao CUF kukubali matokeo.
Kutoka Sumbawanga mwandishi wetu anaripoti kuwa, aliyekuwa Diwani wa Kata ya Katazi, Wilaya ya Sumbawanga, mkoani Rukwa kwa tiketi ya Chadema, Anselmo Mzatula ambaye alihamia CCM amechaguliwa tena kushika wadhifa huo kwa tiketi ya chama hicho.
Ushindi huo wa CCM umetokana na kata ya Katazi kuorodheshwa kati ya kata tatu za
mkoa wa Rukwa kushiriki kwenye uchaguzi mdogo wa madiwani ambazo ziliachwa wa baada ya madiwan wake kufariki dunia.
Mzatula ambaye alijiuzulu uwanachama wa Chadema na kujiunga na CCM mapema mwaka huu ameibuka mshindi kwa kupata kura 1,295 dhidi ya mpinzani wake Aloyce Sokoni wa
Chadema aliyepata kura 324.
Taarifa kutoka wilayani Nkasi zimeeleza kuwa madiwani wa vyama vya upinzani wamepoteza kata moja kati ya mbili zilizokuwa zinaongozwa na madiwani wa vyama hivyo kabla ya uchaguzi huo.
Msimamizi wa jimbo hilo Bi Christina Midelo alisema kuwa Sospeter Kasawanga wa CCM
alishinda uchaguzi huo kwa kupata kura 2,310 dhidi ya mpinzani wake Pius Mwanisawa aliyepata kura 1, 837.
Alisema katika Kata ya Kabwe, mgombea wa Chadema, Asante Libinsha alipata kura 1,953 na kumshinda mgombea wa CCM, Juma Milumba aliyepata kura 1,713, na kura 84 ziliharibika