Wapinzani mbona mmekuwa kimya? Tupatieni taswira ya kisiasa kwa sasa ikoje?

Chagu wa Malunde

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
8,708
5,711
Kuna mwaka niliwahi kukutana na mzee mmoja alikuwa akisoma gazeti la Mwanahalisi, kipindi lipo hot kuibua ufisadi na madudu ya awamu ya nne.

Mimi kama mtu mdadisi nilimuuliza swali moja, mzee samahani, sikujui lakini samahani hawa jamaa wa Mwanahalisi wanapata wapi hizi tips na kulipua haya madudu. Madudu ambayo ni ukweli mtupu! Yule mzee alinijibu jibu moja tu kuwa hawa Mwanahalisi wanatoa picha ya jinsi nchi ilivyo.

Wapinzani mbona mpo kimya au bado mnatafakari jinsi Uchaguzi ulivyowatupa kombo?

Tupeni picha ya nchi,kuna ufisadi? Je kuna ubadhirifu?

Jamani kukosa wabunge isiwe sababu ya kukaa kimya. Kama kuna uozo mtuambie.
 
Kuna mwaka niliwahi kukutana na mzee mmoja alikuwa akisoma gazeti la Mwanahalisi,kipindi lipo hot kuibua ufisadi na madudu ya awamu ya nne...
Utasubiri sana wapinzani wanaendelea na maisha yao Watanzania wanatakiwa kuamka wenyewe. Kila mtu anatakiwa kufanya jitihada walishawaambia hawana shida mkabisha sasa wameona na wenyewe wawe na maisha na Watanzania waamke wenyewe kwa maumivu.
 
Wako shocked na kinachoendelea kwa wale wa ng'ambo ya magharibi wanaodai wanawaunga mkono kumbe wanawachora tu!!! Ona kinachoendelea huko!

 
Ahaaa ahaaaa nimecheka kwa nguvu vibaya sana. Wapinzani watoe tathmini gani ya kisiasa, ili muwabambikie kesi? Wapinzani ilikuwa kama taa, saa hii shetani katumia madaraka yake kuzima taa, ngoja tukae kwanza gizani, siku taa ikiwaka tena tuhesabu hasara. Kiki zote sasa hivi zinabuma, maana watu hawaangalii kwa sana TV wala kusoma magazeti...
Sasa hivi TRA wanaanza kuvizia watu wanaoingia madukani!Ukitoka kununua Tshirt na huna risiti,faini milion!Chanzo kipya cha mapato!
Malofa kweli hawa jamaa,wameua biashara sasa wanataka kuforce mapato!

Mapato ya DPP bado hayajatosha!
 
Sasa hivi TRA wanaanza kuvizia watu wanaoingia madukani!Ukitoka kununua Tshirt na huna risiti,faini milion!Chanzo kipya cha mapato!
Malofa kweli hawa jamaa,wameua biashara sasa wanataka kuforce mapato!
Mapato ya DPP bado hayajatosha!
Na tunawaambia hao jamaa kuwa hatuendi kufanya shoppings.
 
Kuna mwaka niliwahi kukutana na mzee mmoja alikuwa akisoma gazeti la Mwanahalisi,kipindi lipo hot kuibua ufisadi na madudu ya awamu ya nne...
Nimeona mahali Zitto anataka afukue jambo lakini wapinzani wengi bado wana ile hoja ya Muafaka Zanzibar vichwani mwao. Walimkatisha tamaa.

Wamesahau ya kuwa hata kinywa cha mpumbavu kuna wakati hunena hekima.
 
Kwani kuchambua mapungufu ya serikali iliyopo mpaka uwe na wabunge?
Jiwe alishasema tena akarudia mara tatu kusisitiza kuwa uchaguzi umekwisha, muda wa siasa umekwisha, tujenge nchi.. Lissu alikuwa mwiba bungeni na jiwe akamwambia speaker we mtoe nje alafu mimi nitamshugurikia. 🙈

Hauna kinga nje huku we jifanye kimbelembele...😆

By the way jamaa ameongelea issue kubwa za ufisadi wadhani utaziongelea nje huku na kupata backups?

Chagu wa malunde think hard bro
 
Ahaaa ahaaaa nimecheka kwa nguvu vibaya sana. Wapinzani watoe tathmini gani ya kisiasa, ili muwabambikie kesi? Wapinzani ilikuwa kama taa, saa hii shetani katumia madaraka yake kuzima taa, ngoja tukae kwanza gizani, siku taa ikiwaka tena tuhesabu hasara...
Huna imani na TRA, mahakama na kila idara ya serikali. Kumbuka TRA kukusanya kodi ni wajibu wa kisheria.

Kama kuna maovu yanafanywa na serikali na wapinzani wakayaibua na kukosoa hakuna wa kubambikiwa kesi.

Unatakiwa ukubali ukweli kuwa wapinzani hawana cha kukosoa kwa sasa.
 
Serikali inachapa kazi zake hadi wapinzani wameunga juhudi za serikali mkono.
Ile 16% hawana cha kukosoa😂😂😂
 
Back
Top Bottom