Wapinzani mbona mmekuwa kimya? Tupatieni taswira ya kisiasa kwa sasa ikoje?

Kuna mwaka niliwahi kukutana na mzee mmoja alikuwa akisoma gazeti la Mwanahalisi, kipindi lipo hot kuibua ufisadi na madudu ya awamu ya nne.

Mimi kama mtu mdadisi nilimuuliza swali moja, mzee samahani, sikujui lakini samahani hawa jamaa wa Mwanahalisi wanapata wapi hizi tips na kulipua haya madudu. Madudu ambayo ni ukweli mtupu! Yule mzee alinijibu jibu moja tu kuwa hawa Mwanahalisi wanatoa picha ya jinsi nchi ilivyo.

Wapinzani mbona mpo kimya au bado mnatafakari jinsi Uchaguzi ulivyowatupa kombo?

Tupeni picha ya nchi,kuna ufisadi? Je kuna ubadhirifu?

Jamani kukosa wabunge isiwe sababu ya kukaa kimya. Kama kuna uozo mtuambie.
Magufuli hataki kabisa kukosolewa. Amehakikisha anakwibavkura ili wabunge woooote wanaomkosoaga wasirudi bungeni. Magazeticmengi yamefutwa kabisa, na yaliyopo yanapigwacfaini kubwavna maonyo makali kila uchao. Mbowe kaongea sana tu, ona walivyoripoti kwa woga. Tundu Lissu ndio usiseme. Usijali hata hivyo, nondo zitakuja tu. Ulionavjinsi Mbowe alivyotupia za usoni? Yajayo yanafurahisha. Vuta subira
 
Kila kitu kinaendelea vizuri ajira za kumwaga, vifaa vya ujenzi bei chini ili kuwasaidia wanyonge wajenge,bei za mazao ni rafiki kwa mkulima, upatikanaji wa pembe jeo nchi nzima, Uhuru wa kujieleza upo na utawala wa sheria upo
Huyo utapoteza bure muda wako ukijaribu kumwelimisha. Chama kama siyo chama basi ukabila umemshikia akili, hawezi kuelewa.
 
Back
Top Bottom