Wapinzani kutoka bungeni ni mkakati wa kimakosa

kalulukalunde

JF-Expert Member
May 27, 2016
1,056
1,083
KWENYE Jamhuri mengine hayawezekani kubadilishwa kwa wabunge kutoka tu kwenye vikao vya Bunge. Kuna wakati mbunge Tundu Lissu hakuonyesha kumtambua Rais. Ni hivi, kwenye Jamhuri Rais akishaapishwa ndio ameshakuwa Amiri Jeshi Mkuu. Hii ndio tafsiri halisi ya jambo hilo. Yawezekana, mwingine akaona, kuwa aliyeapishwa si Rais wake, nalo haliwezekani, kama Rais atakula kiapo kulitumikia Bunge la Jamhuri, basi, huyo ndiye rais pia kwa wabunge waliomo bungeni, ni kwa miaka mitano ijayo.

Maana, unaposema Jamhuri haina Rais una maana Jamhuri haina pia Amiri Jeshi Mkuu. Na kwenye Jamhuri ambapo unaweza kusimama na kusema hayo na kurudi nyumbani kwa amani na utulivu, basi, ujue Jamhuri hiyo ina Rais, na hivyo, mfumo wa kidola unaoheshimu haki za raia kujieleza kwa uhuru na hata kulindwa dhidi ya watakaochukizwa na kauli zao.

Tukaona wakati ule, kuwa Rais alihutubia Bunge, kuna wabunge wa upinzani wakaleta rabsha za hapa na pale, na kuna waliotulia kumsikiliza Rais wa Awamu ya Tano alipotoa mwelekeo kwa taifa.
Kilichopo sasa, wabunge wa upinzani wanatoka wakimsusia Bunge Naibu Spika, Dk. Ackson Tulia. Swali la kujiuliza; Unafanyaje na Naibu Spika aliyechaguliwa na wabunge wenyewe na kuapishwa?

Hakika swali hili lilipaswa wajiulize wabunge wa upinzani wenye kutoka bungeni kila baada ya dua ya asubuhi. Kwa kufuatilia kwangu siasa za nchi hii na dunia, na kwa kuyaangaalia mahitaji ya wananchi kwa sasa, naona mkakati huu wa wabunge wa upinzani ni wa kimakosa.

Ni mkakati utakaokuwa na gharama zaidi kwa wapinzani huko tunakokwenda kuliko Chama cha Mapinduzi chenye wabunge wengi bungeni. Unapopanga kulifanya jambo ni vema ukatafakari pia matokeo ya jambo husika. Kwa sababu za kibinadamu, ikiwamo kupandwa na jazba na mengineyo, wapinzani kutoka Bungeni siku ile ya kwanza baada ya mtafaruku kuanza ingeeleweka kwa wapiga kura.

Lakini, kwa kuendelea kwao kutoka kila asubuhi ya siku ya kazi za Bunge walizotumwa na wapiga kura kwenda kuzifanya inaanza kujenga hisia miongoni mwa Watanzania, mimi mmojawapo, kuwa huko ni kukosekana kwa umakini.

Niliangalia Bunge lilipoanza jana asubuhi na hakika nilisikitika moyoni. Naamini, siko peke yangu, maana, hayo si matarajio ya Watanzania kuwa na wabunge watakaokuwa wakichaguliwa na kufanya mambo kama yale.

Kama nchi, hakuna namna yeyote ya kuikimbia mifumo na kanuni tulizojiwekea. Haina mashiko, hoja ya kumkataa mtu katika nafasi yake na ambaye hajafanya lolote linalomtaka ang'atuke kwa mujibu wa kanuni, sheria na taratibu zetu kimfumo.

Kama mbunge hamtaki au hampendi Naibu Spika, hakuna anayemlazimisha, nje ya Bunge, kumwalika Naibu Spika kwenye kipaimara cha mwanawe au sherehe ya Maulid.

Na kimsingi, yanapotokea mapungufu ya kimfumo ndani ya kanuni, sheria na taratibu zetu mahali pekee kwa kuanzisha jitihada za kuyabadili hayo ni ndani ya Bunge au mahakamani. Si kwenye viwanja vya Bunge. Na kwa ilivyo sasa hakuna namna, Wabunge wanaotoka itafika siku itawalazimu wabaki tu ndani ya Bunge na Naibu Spika huyo huyo.

Tatizo hapa watakuwa wamepoteza muda mwingi nje ya Bunge badala ya kuwa ndani na kufanya kazi ya kuwatumikia wananchi kupitia Bunge.

Hii ni Nchi Yetu sote. Iko siku wapinzani ndio watakaounda serikali na Spika au Naibu Spika atatoka miongoni mwa wapinzani wa sasa. Kama wabunge wa CCM watafanya haya ya kutoka bungeni kwa vile tu hawatampenda au kumtaka Spika, basi, kwa namna hii hii, tutawashutumu wabunge hao wa CCM kwa wakati huo.

Raia Mweama
 
Good idea..

Swali:
Kwa nini wabunge UPINZANI wanatoka nje? Sababu zipi zinawafanya watoke nje ya bunge? Kwa nini wanamkataa Naibu spika? kwa nn asiwe Mwenyekiti au Spika?
 
Uamuzi wa kutoka nje ni mkakati ulioshindwa ndio sababu CCM wamekataa kufanya aina yoyote ya Mazungumzo na Ukawa kuhusu hilo kwa kuwa kwa CCM huo ni ushindi wa Mezani.
Umaarufu wa Chadema ulianzia Bungeni kuanzia 2007 kwny Richmond scandle, uamuzi wa kuamua kutoka kwny Budget session ni ahueni kubwa kwa CCM. Kwny Mpambano wa kisiasa unahitajika mpango madhubuti kwny lolote mlifanyalo. Usifanye jambo lolite ambalo ni ahueni kwa Mpinzani wako. Upinzani ukiamua kususa kwa kuwa hawamtaki Naibu Spika hapo CCM wanaitumia hiyo Golden chance kwa kuhakikisha mijadala yote muhimu na Makini wanamtumia huyo Naibu Spika na ndicho kinachofanyika.
 
Tulisema mapemaaaa kuwa hii style haina mana tukaitwa majina yote mabaya tukauliza mbona mwenyekiti hatumuoni akitoka au kujiziba makaratasi kwa kipindi chote majibu hakuna
 
Hata kipindi cha katiba mpya walitoka hivyohvyo na wakabezwa na kukejeliwa mno , lkn mwisho wa cku wale wale waliokuwa wanawabeza wabunge wa upinzani wakaja kugundua kuwa katiba mpya iliyotungwa chini ya wabunge wa ccm ina mapungufu na haijazingatia maoni ya wananchi walio wengi ...sasa Leo hii tunaona kabsa bajeti ikiwa ni kinyume na matalajio ya wananchi ...kila kitu kimepanda na mzunguko Wa pesa umekuwa mgumu mno ...wabunge Wa upinzani wameiita bajeti hewa , inaonekana wako sahihi kabsa
 
Kuna huyu mdau wa siasa amejaribu kutoa historia ya wabunge wa upinzani na ususiaji wa mijadala bungeni.

Kigeugeu Cha Wabunge wa upinzani tangu mwaka 1995 -(2) Tangu Bunge la vyama vingi lianze mwaka 1995 wabunge wa upinzani ambao ni wachache bungeni wamekuwa wanalalamikia kiti cha Spika na kutofautiana naye au kudai wanaburuzwa na wenzao wa CCM.
Mwaka 2003, Mbowe alitofautiana na Spika kwa kutangaza kuwa bungeni hakuna chochote kinachofanyika ni kama mchezo wa kuigiza, pia alimrushia lawama Spika wa Bunge wakati ule Pius Msekwa kuwa ni dikteta na analiburuza Bunge.
Kiongozi huyo alienda mbali kwa kusema kuwa Msekwa ametunga kanuni za kuendesha Bunge anavyotaka na kuwabana wapinzani.
Hoja hiyo aliizungumza kwenye majukwaa mbalimbali ya mikutano ya kisiasa hali iliyosababisha Spika wa Bunge kuiamuru Kamati ya Maadili na Hadhi ya Bunge kumhoji Mbowe.
Ajabu, Mbowe alifungua kesi kutaka Mahakama Kuu ya Tanzania kupinga kuhojiwa na Kamati ya Bunge hali hii ilileta mgongano katika hii mihimili miwili ya dola. Katika kipindi chote hicho upinzani uliendelea kudai kuwa Spika ni mbabe na analiburuza Bunge.
Kuanzia mwaka 2005 hadi 2010 Spika wa Bunge alikuwa Samweli Sita na Kiongozi wa Upinzani alikuwa Hamad Rashid, wakati huo akiwa mwanachama wa CUF.
Rashid alikuwa na busara ya aina yake, hakuwatumia wabunge wa upinzani kususa vikao vya Bunge, bali aliwaongoza kujenga hoja mbadala. Katika kipindi hicho pia, kulikuwa na malalamiko kwa baadhi ya wabunge wa upinzani hasa kutoka Chadema kulalamikia kutofuatwa kwa Kanuni huku CCM wakipitisha mambo mengi kutokana na wingi wao bungeni.

Kiongozi wa Upinzani Bungeni
Tangu mwaka 2010 hadi sasa Chadema kwa mara ya pili wametoa kiongozi wa Upinzani Bungeni, Mbowe na tumeshuhudia muda mwingi wapinzani wakilalamikia kiti cha Spika.
Kuanzia mwaka 2010 hadi 2015, Spika wa Bunge alikuwa Anna Makinda na Naibu Spika alikuwa Job Ndugai. Wapinzani walimlalamikia Spika wakimtuhumu kuwa anailinda Serikali na kuwa kiti kimemshinda. Sasa hivi kiti hicho kinakaliwa na Job Ndugai ambaye anaitwa ni ‘mbabe’.
Wote tunakumbuka jinsi ilivyokuwa vigumu kiti cha Spika kuongoza mjadala kutokana na wabunge wengi wa upinzani kuomba miongozo mbalimbali kiasi cha kulifanya Bunge lionekane linapoteza hadhi yake.
Kuna wakati wabunge walisimama huku wakipiga kelele na kulazimisha kuahirishwa vikao vya Bunge mara kwa mara.

Bunge Maalumu ya Katiba
Hali hii ilijitokeza hata kwenye Bunge Maalumu la Katiba (BMK) na ndiko Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) ulizaliwa rasmi. Wote tulishuhudia ilivyochukua muda mrefu kutengeneza kanuni.
Mtakumbuka ilivyochukua muda mrefu kujadili kuhusu kutumika kwa kura ya wazi au ya siri, lakini ilipokuja kuruhusiwa kikanuni kuwa kila mtu apige kura kwa hiari yake wale wale wabunge wa Ukawa waliokuwa wanapinga kwa nguvu zote kura ya wazi walipiga kura ya wazi kwa hiyo, tulichukua muda mwingi kubishana kwa jambo lililokuwa halina msingi wowote.
Wote mnakumbuka mjadala katika Bunge Maalumu la Katiba ulivyokuwa mgumu, Ukawa waking’ang’ania hoja wanataka kulazimisha iwekwe wakidai ni hoja ya wananachi. Mvutano ulipoendelea zaidi Ukawa wakatoa nje ya Bunge.
Spika wa Bunge Maalumu la Katiba, Samwel Sitta ambaye ndiye alikuwa chaguo la Ukawa, alipoanza kusimamia kanuni walimgeuka na kuonekana hafai na anatumika na Serikali na chama cha CCM.

Sakata la Naibu Spika
Imeanzishwa propaganda inayoenezwa ya kutaka kumng’oa Naibu Spika, Dk Tulia Ackson kwa madai ametumwa na Rais John Magufuli kuminya uhuru na demokrasia ndani ya Bunge.
Kama nilivyoeleza, hii siyo mara ya kwanza kwa Kambi ya Rasmi ya Upinzani kulalamikia Kiti cha Spika.
Pia, siyo mara ya kwanza kwa upinzani kususa na kutoka nje ya Bunge, pia, siyo mara ya kwanza wabunge wa upinzani kukorofishana na kiti cha Spika.
Tatizo la Kambi ya upinzani ni pale Spika anaposimamia Kanuni. Kanuni zipo wazi kama hujaridhika na uamuzi wa kiti cha Spika unaruhusiwa kukata rufaa na hoja ikajadiliwa, sasa wabunge wa kambi rasmi ya upinzani sijui ni kwanini hawataki kufuata utaratibu huu, ambao ni wa Kikanuni. Wao wanataka kumng’oa spika.

Kufanya siasa bungeni
Kambi ya Upinzani imeacha kufanya kazi yake ya kujenga hoja mbadala imekuwa inalitumia Bunge kama uwanja wa kutaka kujijenga kisiasa na baadhi ya wabunge kujitafutia umaarufu na matokeo yake, badala ya kujadili hoja tumekuwa tunasikia vijembe, mipasho, kashfa na malumbano yasiyo na msingi wowote ndani ya Bunge.
Kwa hiyo, Bunge limegeuka jukwaa la malumbano ya kisiasa na baadhi ya wanasiasa kujipatia umaarufu badala ya kumtetea mwananchi mnyonge.
Baadhi ya wabunge wa upinzani hawasomi kanuni. sina maana kwamba ni ‘vilaza’, hapana ila ni lazima watambue na kuzielewa kanuni zinazoongoza Bunge kuwa ni kanuni zilizotungwa na kupitishwa na wabunge wenyewe.
Ni utaratibu wa mahali popote kwamba kila taasisi ina kanuni na miongozo yake, lakini muhimu kutambua kuwa juu ya kanuni kuna sheria na juu yake kuna katiba.
Vitu vyote hivi vinatakiwa kusimamiwa na kiti cha Spika na kinapokosea upo utaratibu wa kikanuni unaoelekeza kitu cha kufanya na siyo kufanya vurugu na kuzomeazomea.
Katiba inatambua kuwa kuna Naibu Spika, kanuni za Bunge zinaelekeza utendaji wa kila siku bungeni, lazima kuna kuwa na kiongozi wa kuongoza iwe ni Spika mwenyewe au Naibu Spika au wenyeviti.
Kinachoshuhuhudiwa bungeni hivi sasa ni vurugu za miongozo na kuhusu utaratibu, kwa hiyo kama hali hii haitadhibitiwa na kiti cha Spika basi Bunge kazi yake kubwa itakuwa ni kujadili miongozo na utaratibu na kuweka kando mambo ya msingi ya kumsaidia mwananchi mnyonge.

Kudhalilisha wanawake
Mkakati wa upinzani bungeni kumwondoa Naibu Spika katika madaraka yake, ni mwendelezo wa wazi wa udhalilishaji dhidi ya wanawake kuwa hawana uwezo wa kuongoza.
Ukichunguza kwa umakini utagundua kosa la Naibu Spika ni kutaka kulifanya Bunge liwe chombo chenye heshima na kinachofanya shughuli zake kwa umakini kwa kufuata kanuni ilizojiwekea.
Huko nyuma wote tulishudia jinsi Makinda alivyokuwa anazomewa na wabunge wetu wa upinzani, kudhalilishwa na kuambiwa kiti kimemshinda na anatumika kuilinda Serikali. Hii yote ni kuudhalilisha utu wa mwanamke.
Sasa hivi tunaye mwanamama mwingine msomi, Dk Tulia hadi sasa hatuelezwi ni kanuni ipi Naibu Spika amekiuka au sheria ipi na kifungu kipi cha Katiba amekivunja, tunachoona ni madai yasiyo na uthibitisho.
Hii propaganda chafu inafaa kupigwa vita na wadau wote kwa sababu hivi sasa Tanzania ni moja ya nchi inayopigania usawa wa kijinsia na tunaelekea kwenye asilimia hamsini kwa hamsini.

Dalili zilianza mapema
Dalili za kukataliwa kwa Naibu Spika zilionekana tangu mwanzo kwani wabunge wa upinzani walimkataa hata kabla ya kuanza kazi kwa madai kuwa ametumwa na Ikulu na tulishuhudia hata siku ya kujieleza alivyokuwa anazomewa.
Tabia hii ambayo hata wanafunzi wa shule za msingi hawawezi kufanya ndiyo ilionyeshwa wa wabunge wa Kambi rasmi ya Upinzani kwa Naibu Spika. Hata hivyo, kiongozi huyo alivumilia kwa sababu yupo kwa ajili ya kuwatumikia Watanzania wote.

Mwandishi ni Mwenyekiti wa Chama Cha Kijamii (CCK), anapatikana kwa barua pepe: luhanyaakitanda@yahoo.com na maoni@mwananchi.co.tz.
 
Tulisema mapemaaaa kuwa hii style haina mana tukaitwa majina yote mabaya tukauliza mbona mwenyekiti hatumuoni akitoka au kujiziba makaratasi kwa kipindi chote majibu hakuna
Mboe alikurupupuka. Hii imewaharibia sana Sema Hawa jamaa ni wagumu kutoka hadharani kukiri mpango huu ulikua dhaifu. Lakini jamii tumetambua ujinga wao.

Sasa hivi imebaki nitoke vipi kwa kutumia magazeti.
Pia mboe aache kuendesha chama kama mali binafsi, akubali maoni ya wadau. Na hii tabia ya kuzira kila jambo ni nonsense, kwani haijawa na matokeo chanya toka waanze.
 
Kuna huyu mdau wa siasa amejaribu kutoa historia ya wabunge wa upinzani na ususiaji wa mijadala bungeni.

Kigeugeu Cha Wabunge wa upinzani tangu mwaka 1995 -(2) Tangu Bunge la vyama vingi lianze mwaka 1995 wabunge wa upinzani ambao ni wachache bungeni wamekuwa wanalalamikia kiti cha Spika na kutofautiana naye au kudai wanaburuzwa na wenzao wa CCM.
Mwaka 2003, Mbowe alitofautiana na Spika kwa kutangaza kuwa bungeni hakuna chochote kinachofanyika ni kama mchezo wa kuigiza, pia alimrushia lawama Spika wa Bunge wakati ule Pius Msekwa kuwa ni dikteta na analiburuza Bunge.
Kiongozi huyo alienda mbali kwa kusema kuwa Msekwa ametunga kanuni za kuendesha Bunge anavyotaka na kuwabana wapinzani.
Hoja hiyo aliizungumza kwenye majukwaa mbalimbali ya mikutano ya kisiasa hali iliyosababisha Spika wa Bunge kuiamuru Kamati ya Maadili na Hadhi ya Bunge kumhoji Mbowe.
Ajabu, Mbowe alifungua kesi kutaka Mahakama Kuu ya Tanzania kupinga kuhojiwa na Kamati ya Bunge hali hii ilileta mgongano katika hii mihimili miwili ya dola. Katika kipindi chote hicho upinzani uliendelea kudai kuwa Spika ni mbabe na analiburuza Bunge.
Kuanzia mwaka 2005 hadi 2010 Spika wa Bunge alikuwa Samweli Sita na Kiongozi wa Upinzani alikuwa Hamad Rashid, wakati huo akiwa mwanachama wa CUF.
Rashid alikuwa na busara ya aina yake, hakuwatumia wabunge wa upinzani kususa vikao vya Bunge, bali aliwaongoza kujenga hoja mbadala. Katika kipindi hicho pia, kulikuwa na malalamiko kwa baadhi ya wabunge wa upinzani hasa kutoka Chadema kulalamikia kutofuatwa kwa Kanuni huku CCM wakipitisha mambo mengi kutokana na wingi wao bungeni.

Kiongozi wa Upinzani Bungeni
Tangu mwaka 2010 hadi sasa Chadema kwa mara ya pili wametoa kiongozi wa Upinzani Bungeni, Mbowe na tumeshuhudia muda mwingi wapinzani wakilalamikia kiti cha Spika.
Kuanzia mwaka 2010 hadi 2015, Spika wa Bunge alikuwa Anna Makinda na Naibu Spika alikuwa Job Ndugai. Wapinzani walimlalamikia Spika wakimtuhumu kuwa anailinda Serikali na kuwa kiti kimemshinda. Sasa hivi kiti hicho kinakaliwa na Job Ndugai ambaye anaitwa ni ‘mbabe’.
Wote tunakumbuka jinsi ilivyokuwa vigumu kiti cha Spika kuongoza mjadala kutokana na wabunge wengi wa upinzani kuomba miongozo mbalimbali kiasi cha kulifanya Bunge lionekane linapoteza hadhi yake.
Kuna wakati wabunge walisimama huku wakipiga kelele na kulazimisha kuahirishwa vikao vya Bunge mara kwa mara.

Bunge Maalumu ya Katiba
Hali hii ilijitokeza hata kwenye Bunge Maalumu la Katiba (BMK) na ndiko Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) ulizaliwa rasmi. Wote tulishuhudia ilivyochukua muda mrefu kutengeneza kanuni.
Mtakumbuka ilivyochukua muda mrefu kujadili kuhusu kutumika kwa kura ya wazi au ya siri, lakini ilipokuja kuruhusiwa kikanuni kuwa kila mtu apige kura kwa hiari yake wale wale wabunge wa Ukawa waliokuwa wanapinga kwa nguvu zote kura ya wazi walipiga kura ya wazi kwa hiyo, tulichukua muda mwingi kubishana kwa jambo lililokuwa halina msingi wowote.
Wote mnakumbuka mjadala katika Bunge Maalumu la Katiba ulivyokuwa mgumu, Ukawa waking’ang’ania hoja wanataka kulazimisha iwekwe wakidai ni hoja ya wananachi. Mvutano ulipoendelea zaidi Ukawa wakatoa nje ya Bunge.
Spika wa Bunge Maalumu la Katiba, Samwel Sitta ambaye ndiye alikuwa chaguo la Ukawa, alipoanza kusimamia kanuni walimgeuka na kuonekana hafai na anatumika na Serikali na chama cha CCM.

Sakata la Naibu Spika
Imeanzishwa propaganda inayoenezwa ya kutaka kumng’oa Naibu Spika, Dk Tulia Ackson kwa madai ametumwa na Rais John Magufuli kuminya uhuru na demokrasia ndani ya Bunge.
Kama nilivyoeleza, hii siyo mara ya kwanza kwa Kambi ya Rasmi ya Upinzani kulalamikia Kiti cha Spika.
Pia, siyo mara ya kwanza kwa upinzani kususa na kutoka nje ya Bunge, pia, siyo mara ya kwanza wabunge wa upinzani kukorofishana na kiti cha Spika.
Tatizo la Kambi ya upinzani ni pale Spika anaposimamia Kanuni. Kanuni zipo wazi kama hujaridhika na uamuzi wa kiti cha Spika unaruhusiwa kukata rufaa na hoja ikajadiliwa, sasa wabunge wa kambi rasmi ya upinzani sijui ni kwanini hawataki kufuata utaratibu huu, ambao ni wa Kikanuni. Wao wanataka kumng’oa spika.

Kufanya siasa bungeni
Kambi ya Upinzani imeacha kufanya kazi yake ya kujenga hoja mbadala imekuwa inalitumia Bunge kama uwanja wa kutaka kujijenga kisiasa na baadhi ya wabunge kujitafutia umaarufu na matokeo yake, badala ya kujadili hoja tumekuwa tunasikia vijembe, mipasho, kashfa na malumbano yasiyo na msingi wowote ndani ya Bunge.
Kwa hiyo, Bunge limegeuka jukwaa la malumbano ya kisiasa na baadhi ya wanasiasa kujipatia umaarufu badala ya kumtetea mwananchi mnyonge.
Baadhi ya wabunge wa upinzani hawasomi kanuni. sina maana kwamba ni ‘******’, hapana ila ni lazima watambue na kuzielewa kanuni zinazoongoza Bunge kuwa ni kanuni zilizotungwa na kupitishwa na wabunge wenyewe.
Ni utaratibu wa mahali popote kwamba kila taasisi ina kanuni na miongozo yake, lakini muhimu kutambua kuwa juu ya kanuni kuna sheria na juu yake kuna katiba.
Vitu vyote hivi vinatakiwa kusimamiwa na kiti cha Spika na kinapokosea upo utaratibu wa kikanuni unaoelekeza kitu cha kufanya na siyo kufanya vurugu na kuzomeazomea.
Katiba inatambua kuwa kuna Naibu Spika, kanuni za Bunge zinaelekeza utendaji wa kila siku bungeni, lazima kuna kuwa na kiongozi wa kuongoza iwe ni Spika mwenyewe au Naibu Spika au wenyeviti.
Kinachoshuhuhudiwa bungeni hivi sasa ni vurugu za miongozo na kuhusu utaratibu, kwa hiyo kama hali hii haitadhibitiwa na kiti cha Spika basi Bunge kazi yake kubwa itakuwa ni kujadili miongozo na utaratibu na kuweka kando mambo ya msingi ya kumsaidia mwananchi mnyonge.

Kudhalilisha wanawake
Mkakati wa upinzani bungeni kumwondoa Naibu Spika katika madaraka yake, ni mwendelezo wa wazi wa udhalilishaji dhidi ya wanawake kuwa hawana uwezo wa kuongoza.
Ukichunguza kwa umakini utagundua kosa la Naibu Spika ni kutaka kulifanya Bunge liwe chombo chenye heshima na kinachofanya shughuli zake kwa umakini kwa kufuata kanuni ilizojiwekea.
Huko nyuma wote tulishudia jinsi Makinda alivyokuwa anazomewa na wabunge wetu wa upinzani, kudhalilishwa na kuambiwa kiti kimemshinda na anatumika kuilinda Serikali. Hii yote ni kuudhalilisha utu wa mwanamke.
Sasa hivi tunaye mwanamama mwingine msomi, Dk Tulia hadi sasa hatuelezwi ni kanuni ipi Naibu Spika amekiuka au sheria ipi na kifungu kipi cha Katiba amekivunja, tunachoona ni madai yasiyo na uthibitisho.
Hii propaganda chafu inafaa kupigwa vita na wadau wote kwa sababu hivi sasa Tanzania ni moja ya nchi inayopigania usawa wa kijinsia na tunaelekea kwenye asilimia hamsini kwa hamsini.

Dalili zilianza mapema
Dalili za kukataliwa kwa Naibu Spika zilionekana tangu mwanzo kwani wabunge wa upinzani walimkataa hata kabla ya kuanza kazi kwa madai kuwa ametumwa na Ikulu na tulishuhudia hata siku ya kujieleza alivyokuwa anazomewa.
Tabia hii ambayo hata wanafunzi wa shule za msingi hawawezi kufanya ndiyo ilionyeshwa wa wabunge wa Kambi rasmi ya Upinzani kwa Naibu Spika. Hata hivyo, kiongozi huyo alivumilia kwa sababu yupo kwa ajili ya kuwatumikia Watanzania wote.

Mwandishi ni Mwenyekiti wa Chama Cha Kijamii (CCK), anapatikana kwa barua pepe: luhanyaakitanda@yahoo.com na maoni@mwananchi.co.tz.
Huu ndo ukweli halisi kwa asie penda kujitoa ufahamu, najua kwa wenzetu ni ngumu kumeza
 
Uamuzi wa kutoka nje ni mkakati ulioshindwa ndio sababu CCM wamekataa kufanya aina yoyote ya Mazungumzo na Ukawa kuhusu hilo kwa kuwa kwa CCM huo ni ushindi wa Mezani.
Umaarufu wa Chadema ulianzia Bungeni kuanzia 2007 kwny Richmond scandle, uamuzi wa kuamua kutoka kwny Budget session ni ahueni kubwa kwa CCM. Kwny Mpambano wa kisiasa unahitajika mpango madhubuti kwny lolote mlifanyalo. Usifanye jambo lolite ambalo ni ahueni kwa Mpinzani wako. Upinzani ukiamua kususa kwa kuwa hawamtaki Naibu Spika hapo CCM wanaitumia hiyo Golden chance kwa kuhakikisha mijadala yote muhimu na Makini wanamtumia huyo Naibu Spika na ndicho kinachofanyika.
Wakitumia mwanya huo kumuweka naibu spika kwenye mijadala yote,je,ni faida au hasara kwa nchi?
 
Good idea..

Swali:
Kwa nini wabunge UPINZANI wanatoka nje? Sababu zipi zinawafanya watoke nje ya bunge? Kwa nini wanamkataa Naibu spika? kwa nn asiwe Mwenyekiti au Spika?
NS kaamua kufata sheria harisi. Ni bunge la hapa kazi tu, utoto na vibweka na kujikweza hatuvitaki tena
 
Hapo bwana mwenyekiti umeanza vizuri lakini kwa mawazo yangu naona kuhusianisha mgongano wa Tulia na wapinzani kwamba nikwasababu naibu spika huyo ni mwanamke na lengo lao nikumkandamiza mwanamke sio kweli iwezayo kuthibitishwa kwa asilimia kubwabali ni hoja mufilisi
Ninasema hivyo kwa sababu umesema walisema Ndugai ni mbabe je kwani nimwanamke huyo?
Wapinzani pia wanampinga Chenge je mwanamke?
Umethibitisha kwamba wamemgomea Sitta je nae alikua mwanamke?
Hoja yako ni nzuri ila umeihitimisha vibaya mwenyekiti

Kamakweli ni mwenyekiti wa chama ujue kwamba unaaminiwa na baadhi ya watu na kwakujitambulisha kama mwenyekiti wa chama fulani inatoa picha kwamba huo ndio msimamo wa chama.Siamini kama chama wanaweza kuwa na hoja mufilisi ya kuhusianisha umwanamke wa naibu spika na mgongano uliopo.
NAKUSHAURI KISEMEE CHAMA VIZURI VINGINEVYO TOA MAWAZO YAKO USIINGIZE CHEO UTASHANGAZA WALIOWENGI
 
Uamuzi wa kutoka nje ni mkakati ulioshindwa ndio sababu CCM wamekataa kufanya aina yoyote ya Mazungumzo na Ukawa kuhusu hilo kwa kuwa kwa CCM huo ni ushindi wa Mezani.
Umaarufu wa Chadema ulianzia Bungeni kuanzia 2007 kwny Richmond scandle, uamuzi wa kuamua kutoka kwny Budget session ni ahueni kubwa kwa CCM. Kwny Mpambano wa kisiasa unahitajika mpango madhubuti kwny lolote mlifanyalo. Usifanye jambo lolite ambalo ni ahueni kwa Mpinzani wako. Upinzani ukiamua kususa kwa kuwa hawamtaki Naibu Spika hapo CCM wanaitumia hiyo Golden chance kwa kuhakikisha mijadala yote muhimu na Makini wanamtumia huyo Naibu Spika na ndicho kinachofanyika.
Wanapata faida gani?ona bajeti iliyopitishwa unafikiri upinzani ungekuwepo hali ingekuwaje
 
Bajeti za Miaka 10 zilipitishwa wakati wa Jk na Wapinzani walikuwepo na Mwishowe wakazunguka Nchi nzima wakati wa Kampeni kusema Jakaya hajafanya kitu. Bora tuonje ladha tofauti.
 
Back
Top Bottom