Wapinzani kuhamia CCM vs kumuunga mkono Rais wakiwa katika vyama vyao

MUSIGAJI

JF-Expert Member
Dec 26, 2014
2,186
2,455
Wakuu poleni na ujenzi wa Taifa.Naomba niingie kwenye mada moja kwa moja.
Takribani mwaka mmmoja sasa kumekuwepo na wimbi kubwa la wapinzani kuhamia Chama cha Mapinduzi ( CCM),Wengi wa wanaohama wanatoa sababu ya msingi ambayo ni kwenda kumuunga mkono Rais katika juhudi alizozionyesha za kuifikia Tanzania yenye uchumi wa viwanda,Tanzania itakayomkomboa Mtanzani yule wa chini kabisa.

Kumekuwa na dhana ya kwamba watu hawa hasa wabunge wananunuliwa na hoja ya wanaosema hii ni kwamba,Ikiwa wabunge hawa wanataka kumuunga mkono Mh Rais Magufuri kwanini wasifanye hivyo wakiwa katika vyama vyao?.Kwa nini waliingize Taifa katika gharama mpya za uchaguzi?Katika kuitazama dhana hii ebu tuangalie ugumu uliopo kwa Mbunge kwa upinzani kumuunga mkono Mh Rais akiwa katika chama chake katika njanja zifuatazo.

I)Mbunge wa upinzani kuunga mkono Bajeti ya serikali waziwazi.Wabunge wa upinzani hasa CHADEMA kuunga mkono bajeti ya serikali wazi wazi ni marufuku.Ikiwa Mbunge wa upinzani akijiridhisha kuwa bajeti ya wizara fulani iko sawa ni marufuku kuiunga mkono hadharani,Mbunge huyu kwa vyovyote atalazimika kuhama ili akapate fursa ya kusaidiana na Mh Rais.

II)Kuambatana na Mh Rais katika ziara mbalimbali ndani ya majimbo ya uchaguzi.Ikitokea Rais akawa na ziara katika jimbo ambalo Mbunge anatoka CHADEMA na Mbunge huyu akaambatana na Mh Rais,Mbunge huyu anaanza kuitwa msaliti na huanza kutengwa katika masuala muhimu ya chama.Katika mazingira haya inakua ngumu kusema Mbunge huyu amuunge mkono Rais akiwa katika chama chake.

iii)Kuunga mkono Sera na maamuzi mbalimbali ya serikali.Ndani ya upinzani ni dhambi na ni usaliti kwa Mbunge wa upinzani kuunga mkono hatua mbalimbali za serikali za kiuchumi.Mfano suala la ununuzi wa ndege ni marufuku Mbunge wa upinzani kutamka waziwazi kuwa suala hili ni muhimu katika kufufua shirika letu la ndege.Hata katika mapokezi ya ndege zetu walipigwa marufuku kuhudhuria.

Demokrasia inagharama,tusiziogope gharama hizi.Rais Magufuri ameonesha nia katika kutupeleka katika uchumi wa viwanda.Tufungue milango watu waje wamusaidie.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kweli ukiwa lichama lile akili inawekwa maaataakoni

don't invest in a woman
 
Upo kijiji gani? Maana Uzi wako nmeufungua nikapiga chafya kwa harufu ya utumbo uliandika!!!!
 
Wanaotaka maendeleo ya nchi watahama ili kusaidia ukuaji wa taifa letu,huwezi kukaa na watu kama zitto ukawaza positive upon your nation
 
Back
Top Bottom