Uchaguzi 2020 Wapinzani kubalini matokeo, Mliingia kwenye Uchaguzi kwa kuiamini NEC hii hii: Tumuache Magufuli achape kazi na tujipange 2025

Alex Fredrick

JF-Expert Member
Jun 21, 2016
573
1,000
Uchaguzi umeisha baada Watanzania waliojiandikisha kutumia haki yao ya msingi tarehe 28 October 2020 kuchagua Viongozi kupitia sanduku la kura.

Tayari matokeo ya Ubunge,Udiwani na Rais yameenza kutolewa Nchini na Chama cha mapinduzi (CCM) kikiwa kinaongoza kwa ushindi wa kishindo.

Sishangai matokeo haya maana ndani ya miaka mitano Rais Dkt. John Pombe Magufuli ametekeleza kwa vitendo yale aliyowaaidi Watanzania na zaidi kufanya mambo makubwa ambayo sie wengine hatukutegemea kabisa.

Tayari kuna baadhi ya Viongozi wa vyama vya siasa wameanza kutoa kauli ambazo sio afya kwa ustawi wa Taifa letu.

Uchaguzi umeisha na niwasihi viongozi wote wa Upinzani kukubali matokeo maana wakati mnaingia kwenye Uchaguzi mliiiamini Tume ya hii ya Uchaguzi.

Na kila Chama kilikubali kuweka mawakala wake kwaajili ya kulinda na kusimamia kura za mgombea wake husika.

Tuache visingizio ambavyo havina mashiko baada ya kuona mmeshindwa kihalali kabisa.

Tumuache Rais Mh DR John Pombe Magufuli amalize ngwe yake na kutekeleza yale yote ambayo aliwaidi Watanzania kwenye campeni zake.

Ewe Mtanzania popote ulipo hasa kijana popote ulipo jiepushe kufanya vurugu au kushawishiwa kufanya maandamano au vurugu yoyote ile.

Busara ni kujipanga upya na kusubiri tena Uchaguzi ujao mwaka 2025 maana subra ni ibada.

#JPM KIOO TUELEKEACHO


Alex Fredrick
 

radika

JF-Expert Member
Jul 15, 2014
19,852
2,000
Korea kaskazini mpya
IMG_0271.jpg
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom