Wapinzani, kabla hamjafikiria kupeleka malalamiko Tume ya Uchaguzi, jiulizeni swali hili

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
42,495
2,000
Ikiwa ni miezi kadhaa sasa tangu Meya Boniface Jacob apeleke mashitaka kwenye Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma juu ya uhalali wa jina la RC Makonda,Tume mpaka leo imetoa mrejesho gani?

Pia mjiulize uchaguzi wa marudia (kama utakuwepo) wasimamizi wa uchaguzi watakuwa ni kina nani kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi iliyopo?

Nawashauri msijisumbue kwenda Tume wala kufungua kesi mahakamani na zaidi hata uchaguzi wa wabunge kwa majimbo yaliyo wazi msishiriki kabisa.

Nawasisitizia msishiriki chaguzi zozote zijazo chini ya Tume hii na sheria ya sasa ya uchaguzi na badala yake muwaache wajitekenye na kucheka wenyewe.

Hata hivyo,ili kuondoa dhana kuwa wapinzani wanalalamika tu bila kuchua hatua,nawashauri wabunge wa upinzani mmoja wenu apeleke hoja binafsi kutaka mabadiliko ya katiba yatakayoruhusu kuundwa kwa Tume Huru ya Uchaguzi au hata hoja ya kutaka sheria ya uchaguzi ibadilishwe kwa lengo la kuwaondoa wakurugenzi wa Halmashuri na watendaji wa kata kama maafisa wa Tume ya Uchaguzi kwa maana ya sheria ya uchaguzi kutoendelea kuwatambua kana wasimamizi wa uchaguzi katika majimbo na kata za uchaguzi.

Wakikataa hoja zenu watawapa uhalali wa kutoshiriki uchaguzi na zaidi uhalali wa kutowabeza na kujisifu kushinda uchaguzi.
 
kiloriti

JF-Expert Member
May 12, 2016
486
1,000
Mleta mada uko sahihi sana.hapa kinachotakiwa ni katiba mpya tu ndo suluhisho wa haya yote.wapende wasipende hilo ndo mzizi wa fitina tu
 
Black fire

JF-Expert Member
Oct 8, 2014
751
1,000
Chadema mtalalamika mpk lini? Unashirikije uchaguzi wa kihuni namna hii?

Na nyie ccm mtabebwa mpk lini?

IPO SIKU YAJA. HATA MUGABE HAKUJUA
 
MSAGA SUMU

JF-Expert Member
May 25, 2015
5,388
2,000
Hilo la kususia uchaguzi ni wazo zuri wasiwasi wangu Mbowe atakubali kweli? Maana idadi ya wabunge ni directly proportional na ruzuku
 
UGORO87

JF-Expert Member
Mar 7, 2014
819
500
Kama nasari alipeleka ushahidi takukuru wa madiwani kuhongwa na haikufanyiwa kazi je hayo malalamiko je itafanyiwa kazi?
 
domokaya

JF-Expert Member
Apr 22, 2010
3,538
2,000
Mleta mada uko sahihi sana.hapa kinachotakiwa ni katiba mpya tu ndo suluhisho wa haya yote.wapende wasipende hilo ndo mzizi wa fitina tu

Wakishindwa tu, katiba mpya inakumbukwa.
Katika kampeni utasikia 'lazima tuwanyooshe' hiyo toka 1995. Eti wapinzani. Uchaguzi ukiambatanishwa na kaposho tu hao mbio kama nyumbu wako kwenye heat wanakimbilia msimu wa kupandwa!
 
dalaber

JF-Expert Member
Aug 6, 2014
1,815
2,000
Kwa yaliyotokea jana 2020 hakuna mpinzani atakayerudi bungeni wala kwenye kata
 
Kingdom_man

JF-Expert Member
May 19, 2010
405
500
Kama Mbowe angekuwa MPINZANI kwelikweli na sio pandikizi hakika tungekuwa na Mapinduzi

Nobody is really serious
 
FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
23,715
2,000
Huwezi pata haki yako ukiwa unekunja nne; ni kuingia vitani ama kuachana na siasa; CDM you have ONLY two option.

La kuanza nalo sasa ni Tume huru ya uchaguzi; hili hulipati kwa kutumia diplomasia. Diplomasia ilikwisha siku Lissu alivyotwangwa risasi as if yeye ni gaidi.

No any other option; twende kazi ana tumwage manyanga ili CCM watawale watakavyo.
 
kipara kipya

JF-Expert Member
May 2, 2016
9,631
2,000
Ikiwa ni miezi kadhaa sasa tangu Meya Boniface Jacob apeleke mashitaka kwenye Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma juu ya uhalali wa jina la RC Makonda,Tume mpaka leo imetoa mrejesho gani?

Pia mjiulize uchaguzi wa marudia (kama utakuwepo) wasimamizi wa uchaguzi watakuwa ni kina nani kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi iliyopo?

Nawashauri msijisumbue kwenda Tume wala kufungua kesi mahakamani na zaidi hata uchaguzi wa wabunge kwa majimbo yaliyo wazi msishiriki kabisa.

Nawasisitizia msishiriki chaguzi zozote zijazo chini ya Tume hii na sheria ya sasa ya uchaguzi na badala yake muwaache wajitekenye na kucheka wenyewe.
Hasira za mkizi......
 
Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
89,723
2,000
Ikiwa ni miezi kadhaa sasa tangu Meya Boniface Jacob apeleke mashitaka kwenye Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma juu ya uhalali wa jina la RC Makonda,Tume mpaka leo imetoa mrejesho gani?

Pia mjiulize uchaguzi wa marudia (kama utakuwepo) wasimamizi wa uchaguzi watakuwa ni kina nani kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi iliyopo?

Nawashauri msijisumbue kwenda Tume wala kufungua kesi mahakamani na zaidi hata uchaguzi wa wabunge kwa majimbo yaliyo wazi msishiriki kabisa.

Nawasisitizia msishiriki chaguzi zozote zijazo chini ya Tume hii na sheria ya sasa ya uchaguzi na badala yake muwaache wajitekenye na kucheka wenyewe.

Ndo Mange alivyowaambia hivyo?
 
domokaya

JF-Expert Member
Apr 22, 2010
3,538
2,000
Chadema mtalalamika mpk lini? Unashirikije uchaguzi wa kihuni namna hii?

Na nyie ccm mtabebwa mpk lini?

IPO SIKU YAJA. HATA MUGABE HAKUJUA

Sio CCM, CCM imemtengeneza Mugabe na CCM hiyo hiyo imeenda kumsaidia asiadhirike.

Ilimuweka madarakani 1980, juzi kaondoka CCM ipo.

CCM imekitengeneza CHADEMA, ukitoka CCM unaenda chadema halafu eti huko chadema ushinde.

Sio leo wala kesho, mzee Mtei hawezi kukubali kuitoa CCM madarakani. Tusubiri aondoke Mtei, mkwe wake na kizazi chake, hapo labda!
 
juvenile davis

JF-Expert Member
Apr 13, 2015
4,637
2,000
Tanzania wapinzani ni wajinga tangia 1992,,waliotaka vyama vingi ni 20% waliotaka chama kimoja ni 80% ila 20% ndio walioshinda..ujinga kamili wa mpinzani ulianza 1995 alipokubali kufanya uchaguzi chini ya katiba yenye muundo wa chama kimoja(CCM). Hadi leo hii ujinga huo unaendelea,,upinzani kwa hapa Tanzania ni bado sana aisee.
 
Mpanda nyangobe

JF-Expert Member
Apr 30, 2015
455
1,000
Mbona kenya katiba imeboreshwa lakini uhuni wa watawala upo pale pale?. Kuna kitu cha kufikiri zaidi ya hizo the so called katiba..
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom