Jackal
JF-Expert Member
- Apr 10, 2012
- 9,553
- 12,665
Kitu cha msingi ,Je umemuelewa?Ukiambiwa kuwa kilikuja na meli usiwe unganisha ndugu, siyo kwamba tunakuchukia, Tumia tu Kiswahili achana na lugha zilizovuka maji
Kitu cha msingi ,Je umemuelewa?Ukiambiwa kuwa kilikuja na meli usiwe unganisha ndugu, siyo kwamba tunakuchukia, Tumia tu Kiswahili achana na lugha zilizovuka maji
Haya ndio aliyosema Mkapa kwamba ukiwa rais watu wanachukulia wanakumiliki,hivi ni kiwango gani cha kuumwa ambacho wananchi tunatakiwa kujua? Au hata kama anaumwa na jino?
Sina tatizo na hilo, ila ndio nimeuliza ni kwa kiwango gani cha kuumwa ambacho wananchi tunatakiwa kuambiwa? maana inawezekana anaumwa ila ndio kama alivyoeleza Makamu wa rais hivyo si tatizo la kulazimika kutangaza kuwa rais mgonjwa ila huku ndio tukawa tunatumia hisia kuona rais ni mgonjwa kiasi saaana kiasi cha kuhitajika wananchi kutangaziwa.Maswala ya kuumwa yako kwenye katiba hivyo tusitumie hisia binafsi. Kama hatupendi basi tubadilishe katiba maana tusikofuata katiba ni dharau kwa wananchi wote. Ndiyo maana kuna raisi mmoja kama hutaki kuweka mambo sawa unaweza kutafuta kazi nyingine.
Magufuli anajulikana ni jeuli sio wa kupelekeshwa na ndio maana akaona alichoeleza Waziri mkuu na Makamu wa rais kinatosha...nadhani anatakiwa ajitokeze wananchi wake wamuone.
..kwani kitu gani kinamzuia asijitokeze?
Sina tatizo na hilo, ila ndio nimeuliza ni kwa kiwango gani cha kuumwa ambacho wananchi tunatakiwa kuambiwa? maana inawezekana anaumwa ila ndio kama alivyoeleza Makamu wa rais hivyo si tatizo la kulazimika kutangaza kuwa rais mgonjwa ila huku ndio tukawa tunatumia hisia kuona rais ni mgonjwa kiasi saaana kiasi cha kuhitajika wananchi kutangaziwa.
COVID 19/SARS 2?!Tungesikia wamepiga hodi Chamwino alafu tukapata habari tungesema ni upendo kweli
Lugha ina changamoto za upumuaji?Niwie radhi Lugha hii kidogo umeandika ikiwa na changamoto nyingi.
Andika Kwa Kiswahili tukuelewe kwa uhakika huenda unahoja nzuri inayochafuliwa na lugha.
Sasa hapo ndio tunarudi kwa Waziri mkuu na Makamu wa rais,maana waziri mkuu alisema ameongea nae rais hadi akamwambia ratiba yake hivyo rais anajielewa na kuweza kufanya maamuzi. Kinachosumbua ni uzushi wa kwamba sijui yupo Kenya mara India.Kiwango ni kuumwa kiasi cha kushidwa kufanya maamuzi. Baraza la mawaziri linatakiwa limwambie Jaji mkuu halafu wateuliwe wataalamu madaktari watatu kumchunguza. Mfano kama unaumwa umwa corona upo kwenye mashine tukavamiwa nani anatakiwa kufanya maamuzi ya kupeleka jeshi? VP hawezi kufanya maamuzi kama hayapo kisheria. Badala yake kuna watu wanajiona ndiye wenye nchi na wengine ni wajinga hivyo wamesema No kwa katiba!
Sasa hapo ndio tunarudi kwa Waziri mkuu na Makamu wa rais,maana waziri mkuu alisema ameongea nae rais hadi akamwambia ratiba yake hivyo rais anajielewa na kuweza kufanya maamuzi. Kinachosumbua ni uzushi wa kwamba sijui yupo Kenya mara India.
Una uhakika kama anajua huku nje waziri mkuu na makamu wa raisi wameeleza nini?Magufuli anajulikana ni jeuli sio wa kupelekeshwa na ndio maana akaona alichoeleza Waziri mkuu na Makamu wa rais kinatosha.
Ccm wangekuwa wamewekeza kwenye ajenda za msingi tusingeona wakigeuka kuwa majizi ya kura, na kutegemea udhaifu wa katiba na vyombo vya dola ili kujitangaza washindi kwenye uchaguzi.Kuna mambo mengi yanaweza kufanya wapinzani hapa nchini mpaka kujenga upya imani kwa wananchi. Hili la kushadidia mkuu wa dola anaumwa au haonekani halina mantiki....
Ukishamuona au wakikwambia unapata nini?Hakuna mtu ana mwamini waziri mkuu wana utamaduni wa kudanganya. Pili Makamu alisema ni kawaida mtu kwenda kutengenezwa alikuwa na maana gani? Tatu kama yupo poa kuna ugumu gani wa kuonekana hata Ikulu tu.
Ndiyo maana tunasema Watanzania tunajijua huwezi kutudanganya kirahisi. Kuumwa ni kitu cha kawaida. Tatizo mmoja tu ni kutokutufanya sisi wajinga kama uongo ule wa Corona, uchaguzi yaani serikali ni ya kitapeli kwelikweli
Unataka wawekeze kwenye ajenda gani labda wewe ulidhike?Ccm wangekuwa wamewekeza kwenye ajenda za msingi tusingeona wakigeuka kuwa majizi ya kura, na kutegemea udhaifu wa katiba na vyombo vya dola ili kujitangaza washindi kwenye uchaguzi.
Ungemuuliza huyo kiazi mwenzio alitaka wapinzani wawekeze kwenye ajenda gani ili yeye aridhike. Kama wapinzani wangekuwa hawana ajenda tusingekuwa tunaona uhayawani, ushenzi na upuuzi wa hali ya juu kwenye chaguzi zetu toka Magu ameingia madarakani.Unataka wawekeze kwenye ajenda gani labda wewe ulidhike?
Muwe mnakubali kushindwa kura mpigiwe na nani hasa na kwa kipi mlichonacho kichwani?
Mmekalia majungu tu hamna lolote kila Rais wa CCM akiingia madarakani hamkosi kasoro,Ungemuuliza huyo kiazi mwenzio alitaka wapinzani wawekeze kwenye ajenda gani ili yeye aridhike. Kama wapinzani wangekuwa hawana ajenda tusingekuwa tunaona uhayawani, ushenzi na upuuzi wa hali ya juu kwenye chaguzi zetu toka Magu ameingia madarakani.
Sie wote humu na yote tunayoongea hapa hakuna mwenye uhakika hata mmoja,na ndio maana wengine wanasema yupo Kenya mara India mara keshafariki hakuna mwenye uhakika.Una uhakika kama anajua huku nje waziri mkuu na makamu wa raisi wameeleza nini?