Wapinzani Chukueni Tahadhari, Njama Walizopanga CCM Kuelekea Uchaguzi wa Serikali Za Mitaa 2019

Chief Kabikula

JF-Expert Member
Jan 1, 2019
7,559
2,000
Chama cha mapinduzi kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa mwezi huu, kimepanga yafuatayo baada ya mipango ya awali kufeli, mipango iliyohusisha maelekezo kwa Watendaji wa kata, makatibu tawala wa wilaya, maafisa usalama wa taifa wa wilaya na waziri waziri mwenye dhamana wa Tamisemi.

Sina haja kurudia walichopanga maana vyote vimeshuhudiwa na watanzania wote. Mapya waliyoyapanga ni yafuatayo, kwa kuwa vyama vikuu Chadema na Act Wazalendo vimejitoa kushiriki uchaguzi huu, CCM wamevielekeza vyama mamluki vyenye mapandikizi yao navyo vijitoe ndio maana baada ya Act Wazalendo kujitoa msululu wa vyama kujitoa uliongezeka mara dufu, wewe hushangai mpaka Lipumba kibaraka wao mkuu.

Pamoja na kujitoa vyama hivyo pandikizi wamepewa maelekezo kuwa uchaguzi utakapokaribia vianze vyote kurudi kushiriki uchaguzi huu haramu ili kudhoofisha nguvu ya Chadema na Act Wazalendo, vilevile kudanganya wafadhili, nchi wahisani kuwa vyama vyote vimeshiriki Chadema na Act Wazalendo ni wakorofi tu. Haya wapinzani taarifa hiyo ifanyieni kazi msiseme hatukuwaambia, time will tell.
 

Bwana PGO

JF-Expert Member
Mar 17, 2008
45,372
2,000
Huyu Dogo kachanganyikiwa aiseeee.....au labda kama wamemnukuu vibaya
Screenshot_20191113-235304.jpeg
 

Jimbi

JF-Expert Member
Aug 16, 2010
3,571
2,000
Mkuu ahsante sana kwa taarifa hizo za huko JIKONI. Nina amini Vyama husika watazifanyia kazi, ili hawa MABEBERU WA AFRIKA waendelee kudhibitiwa ipasavyo.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom