Wapinzani Chukue Viti vya Ubunge kwanza....

Pope

Senior Member
Dec 3, 2007
117
0
kimtazamo naona wapinzani waachane na kumaliza nguvu kwenye kiti ch uraisi badala yake waongeze nguvu kwenye Ubunge.

Naimani kuwa kama hivi vichwa vyote vya Upinzani CUF, NCCR, CHADEMA n.k vikiwa bungeni basi bunge litakuwa la changamoto na kuibana serikali kwa hoja na sio maneno nje ya Bunge, mabyo wakati mwingine ni ya maana lakini yanachukuliwa kama kelele za kisiasa. Najaribu kupata picha kama hawa wangeungana na Ndesamburo, Slaa, Kabwe na wengine sijui pangekuwaje huko!!!

Pili:
Ili kuishinda CCM ni lazima kuwe na umoja, sauti ya Umoja, tukubaliane katika suala la uraisi akisimamishwa mmoja kunakuwa na nguvu na mgawanyo wa kura unakuwa kati ya chama tawala na huyo mgombea aliyesimama, Vyama viachiane majimbo wasimamishe watu wanaokubalika na kuwe na collecive power itakayopelekwa hapo na vyama vyote huku wakifanyiana Kampeni kwa zamu kwa mtaji huu kutakuwa na uhakika wa viti vingi vya uwakilishi wa Upinzani Bungeni...

Naomba kuwakilisha
 
Nimevutiwa na hii post nikaamua nijiandikishe.
Nakubaliana na Mheshimiwa sana hapo, ni kweli kuna kila haja kwa kambi ya Wanasiasa wa Upinzania kulifanyia kzi hili.
Ila nakuwa na wasiwasi hasa kwa suala moja ambalo kwangu nahisi ni kikwazo kwa Wapinzani. Suala lenyewe ni kuhusu RUZUKU,
Ruzuku inachangia sana kuvuruga umoja wa wapinzania kwani kuna walioingia kwenye sisa kwa njaa na hawa ndio wanaofanya safari yetu kuwa fupi na tusifike tunakotaka kwenda, naimani kama tutaamua kuangalia maslahi ya kitaifa tunaweza kujenga umoja wa kweli na kuishinda CCM katika chaguzi zijazo.

Shime watanzania kwa pamoja tunaweza kama elimu ya Uraia itawafikia walio mbali ambao wanahisi kuchagua Upinzani ni dhambi.

otherwise naipenda kazi yenu na ni msomaji mzuri wa hii Forum kila siku ila leo nimeamua kujiandikisha rasmi.
 
Rai yako sio mbaya inaonyesha ni jinsi gani ulivyochoshwa na utawala huu na hivyo ni hatua moja ya kuanzia, lakini kama WTZ tunataka mabadiliko ya kweli na kuingoa CCM madarakani ni kudai Katiba Mpya - hili litatuondolea kasoro nyingi katika uendeshaji wa nchi, juhudi tungazielekeza huko kwani hapo ndio penye chimbuko la matatizo yote chini mwetu, Tupasue jipu kwa kuondoa na mzizi wake otherwise kesho litaota tena.Nafikiri wana JF kudai Katiba mpya iwe ndio dira yetu kulikpo chochote kile.
 
Ndugu Pope na Bikirembwe,

Katika kuwaunga mkono kwa hoja zenu napenda pia niwapongeze kwa kutuletea fikra zenu.

Naamini kwamba mikakati hiyo itasaidia sana katika kuleta changamoto yenye ushindani wa kisiasa utakaosukuma nchi yetu kwenye maendeleo ya kweli yanayoweza kutujengea matumaini ya kupambana na ujinga, umasikini, maradhi, rushwa na ufisadi.

Nionavyo mimi ushindani wa kweli wa kisiasa, ungeanzia kwenye ngazi ya shina, kuelekea kwenye kata, wilaya, mkoa na nchi nzima.
Hii ngazi ya shina ni muhimu sana na inaonekana kupuuzwa na vyama vya ushindani. Hapo ndipo penye ngome ya CCM. Wizi wa kura unaanzia hapo katika kuandikisha wapiga kura.

Mjumbe wa nyumba kumi na Sheha kule Unguja na Pemba ndie anayejua nani CCM na nani mshindani wake. Nani aandikishwe na nani apigwe ngwara na mizengwe.

Ili kuing'oa CCM madarakani ni muhimu sana kushika serikali za mitaani na mitaa; kata na vijiji; miji na wilaya na mikoa na nchi. In that order. Ukitaka kuung'oa mti sharti ung'oe na mizizi yake. Kwa hiyo kila penye mjumbe wa nyumba kumi wa CCM ni lazima awekewe mwenzake wa ushindani katika kupigania serikali za mitaa. Ushindani unaanzia hapa.

Hali hii itaipa ushindani nafsi nzuri zaidi na kwa karibu zaidi ya kujua nini kinaendelea katika uandikishwaji wa wapiga kura na mizengwe ya upigaji kura yenyewe na uhesabuji wa kura na uwakilishi wa mawakala na matokeo halisi ya vituo vya kura.

Makatibu kata na wenyeviti katika sehemu hizo wana mkono wenye nguvu sana katika uibaji wa kura kwa upande wa CCM. Ushindani nao unahitajika kuwa na nguvu katika eneo hili wa kudhibiti shughuli hizi haramu.

Ili lengo la kuupatia ushindani angalau Wabunge wengi zaidi panahitajika KATIBA MPYA. Hii itasaidia kuweka kiwanja sawa cha ushindani wa kisiasa kwa kuzingatia kupunguza madaraka ya Rais (ambaye siku zote ni Mwenyekiti wa CCM).

Pia KATIBA MPYA italenga upatikanaji wa TUME ya TAIFA ya UCHAGUZI isiyomwogopa na kumpendelea MTEUZI wake (Rais na Mwenyekiti wa CCM) na kumnyima MTEUZI huyo nafasi ya uwezo wa kuwafukuza/kuwaondoa wajumbe wa TUME ya UCHAGUZI baada ya kuwateua. Itamnyima MTEUZI uwezo wa kuchagua watu kiholela kama atakavyo yeye kwa kumwekea maeneo ya UTEUZI wake.

KATIBA mpya itamwondolea Rais uwezo wa kukitetemesha kitengo cha JUDICIARY (sheria mama) na kile cha PARLIAMENTARY (Bunge ambalo ndio sauti ya ummah ndani ya serikali yao). KATIBA MPYA pia italipa Bunge nguvu na uwezo wa kumhoji Rais badala ya hii ambayo inatoa nguvu na uwezo kwa Rais wa kulihoji Bunge. KATIBA MPYA yenye kumnyima Rais uwezo wa kutumia vyombo vya dola kwa faida yake binafsi na kwa faida ya chama chake cha siasa.

Kwa kuwa CCM na serikali yao wanakataa katakata kusikia hilo neno la KATIBA MPYA (ambayo wanajua itawaondolea uhondo) ni vyema ushindani ukashika uongozi wa shina na mitaa kisha uka-mobilize madai ya KATIBA MPYA kutokana na wananchi at large badala ya kutokana na vyama vyao vya ushindani.

Malengo ya kushika shina(serikali za mitaa); kupata wabunge wengi na kudai KATIBA MPYA na utekelezaji wake ni lazima viende kwa wakati mmoja. Ni kazi ngumu inayohitaji umoja wa dhati, kujitolea na kujiamini. Hakuna kizuri kipatikanacho kwa bei rahisi.
 
Naunga mkono hoja kabisa, inafaa wapinzani waanzie chini kabisa, kwani hata mtoto huanza kwa kulala kisha akakaa kisha akatambaa kisha akasimama dede kisha akatembea kisha akakimbia kisha akasoma kisha akahitimu kisha akakalia kiti ch enzi kama Mwenyeezi mungu kamjaalia. Na si kukurupuka tu. Haiingii akilini.
 
Mawazom yenu wote ni mazuri sana kasoro ya mmoja wa kuunga uunga tu bila kusema anaunga kivipi wengine wote nakubaliana nanyi.
napenda tuliangalie hili nalo kwa makini .Nia ya Chama chochote cha siasa ni kutwaa dola .Kutaka madaraka ya Nchi .Sasa ili kuanza kupigania Ubunge pekee inatakiwa busara za hali ya juu kwa makubaliano ya vyama hivi .Kwamba kama watamweka Mgombea mmoja wamuunge mkono basi wenyeviti wa Vyama vingine warudi majimboni kuutafuta Ubunge .

Nguvu ya watu kama Mrema wakiwa Bungeni itasikika na huu ndiyo ukweli .Vita ni vita lazima wajifunze kwa CCM kwamba walifikai mahali pa Msekwa na Makamba kuumwa na Mbu huko Kiteto na hawakuja hata kumuona Bush .CCM pamoja na kuwa a viti vingi na kuto kubalilka lakini they have been fighting and they will fight .

Kurudi kwenye shina is very essential .Kuna fitina sana vijijini na za kijinga kuna watendaji wa mitaa kule hata sijui kama wana akili nzuri .

Katiba ni jibu pekee kwa kila kitu japokuwa naona Wapinzani huligusa na kuliacha mara kwa mara lakini Katiba itawapa access kweney Tume.
 
Lakini kuwashauri wapinzani bila kujitambulisha ni kufanya makosa.

Wewe huko upande gani wa siasa? Ukiwa unasema kama mwanaCCM, nadhani wapinzani wamepata ujumbe wako.

Lakini mimi niliye huru (nisiye na chama) nawaambia wapinzani msiweke mayai kwenye kapu moja. Kila ngazi ya uchaguzi ina-visibility yake.
 
Ni kweli lakini hapa tunaongea kwa maslahi ya Utaifa zaidi bila kuwa na Chama, Binafsi kiongozi mwenye dira na anayetekeleza Dira za chama chake ndiye namuunga Mkono kwani Hata katika CCM wapo waadilifu na katika Upinzani wapo Wenye Umimi na Tamaa pia.

Naimani kuwa Mashina ni nguzo muafaka pia ila kwa Level walizonazo akina Lipumba, Zito, Mbowe, Mbatia huwezi kuwarudisha kwenye vikao vya kata wanatakiwa wakawahutubie huko na kuimarisha Chama kwenye Kata na MAshina wakiwa nai Viongozi na wawakilishi wa Majimbo.

Ninaposema hivi namaanisha kunakuwa na Sauti ya nguvu akienda kama Mbunge kama alivyokwenda Mheshimiwa Zitto kupiga tough kule Kiteto mliona impact yake.

Kuing'oa CCM kunahitaji mikakati na si kukurupuka kwa mwendo wa sasa na chaguzi zilizopita tutaisindikiza milele.
 
Labda unataka wapinzani waende msituni. Sababu kubwa ya kushindwa kwa wapinzani sio mbinu zao bali ufinyu wa mawazo ya wapiga kura wenyewe. Na sio kazi ya wapinzani kwenda kuwafundisha watu ABC.
 
Labda unataka wapinzani waende msituni. Sababu kubwa ya kushindwa kwa wapinzani sio mbinu zao bali ufinyu wa mawazo ya wapiga kura wenyewe. Na sio kazi ya wapinzani kwenda kuwafundisha watu ABC.

fikiria kabla hujasema Mkubwa... Naimani elimu ya Uraia ni ukombozi wa Siasa na mafanikio ya Chama cha siasa, watu hawana Elimu ya Uraia bado wanashabikia Chama na si mtu!! naimani kwenye elimu ya Uraia na umakini wa Upinzani CCM huwa inapata taabu, si kila anayehutubia anakipaji cha kukusanya watu na si watu wakikusanyika wanakuja kukusikiliza wewe kuna point mbili ambazo zinatofautiana kukusanya watu na kuwafanya uliowakusanya wakuelewe!! Tulishuhuda Mtikila na Mrema wakisukumwa toka Jangwani hadi makwao, Mrema alikuwa akifungua mdomo esho ne Lead Story leo kiko wapi akiongea habari utaikuta page 5 kama si 7 pembeni ya matangazo ya Vifo hujiulizi ni kwanini? tunapaswa kuwafanya watu wetu waamini tunayoyahutubia majukwaani.

Kwa sasa Chadema wanaweza kuja kuisumbua sana CCM ni kwa sababu wameonyesha vitendo vya maneno yao!! Wako kwa maslahi ya Taifa na si kwa maslahi ya chama chao.

Ninachotaka kusema ni kwamba Watu wanaelimishwa na Kauli zetu ndio zinakujenga au Kukubomoa hujui msemo usemao.... "ULIMI ULIPONZA KICHWA..."

Wabillah Tawfiq
 
Nadhani nimekuamini na kukubaliana na wewe mkuu
 
Ni kweli lakini hapa tunaongea kwa maslahi ya Utaifa zaidi bila kuwa na Chama, Binafsi kiongozi mwenye dira na anayetekeleza Dira za chama chake ndiye namuunga Mkono kwani Hata katika CCM wapo waadilifu na katika Upinzani wapo Wenye Umimi na Tamaa pia.

Naimani kuwa Mashina ni nguzo muafaka pia ila kwa Level walizonazo akina Lipumba, Zito, Mbowe, Mbatia huwezi kuwarudisha kwenye vikao vya kata wanatakiwa wakawahutubie huko na kuimarisha Chama kwenye Kata na MAshina wakiwa nai Viongozi na wawakilishi wa Majimbo.

Ninaposema hivi namaanisha kunakuwa na Sauti ya nguvu akienda kama Mbunge kama alivyokwenda Mheshimiwa Zitto kupiga tough kule Kiteto mliona impact yake.

Kuing'oa CCM kunahitaji mikakati na si kukurupuka kwa mwendo wa sasa na chaguzi zilizopita tutaisindikiza milele.[/QUOTE]

Mbinu za kuing'oa SISIEMU zipo tayari na zinatumika kwa nguvu zote.
Tatizo ni pale SISIEMU ikibaini imeshindwa inatumia Polisi FFU na Fedha za walipa Kodi na Vitisho visivyo vya lazima, kama kuwaeleza wananchi kwamba machafuko yatatokea endapo upinzani utachukua kiti.

Vyama vya Upinzania vikitaka kuchukua hatua kamili kuikabiri SISIEMu katika ununda wake maana yake ni kuanzisha vita. Kwa sababu vyama vya upinzani havina jeshi ni wazi vita ikizuka ni kukimbilia msituni tu.

Aina za siasa kama hii ya kudai haki(sheria) kwa nguvu ni common sana barani Afrika. Ni wazi vyama vya upinzani vinajua madhara ya kutumia nguvu badala ya hoja katika kutwaa madaraka ndiyo maana hata pale SISIEMU ikibebwa na FFU vyama vya upinzani vinaendeleza kauri na hoja za nguvu bila kutumia mabavu.

Sidhani kama chaguzi zijazo litakuwa ni suala la kusindikiza SISIEMU, majira yanabadirika na watu wanabadirika.
 
Ninachotaka kusema ni kwamba Watu wanaelimishwa na Kauli zetu ndio zinakujenga au Kukubomoa hujui msemo usemao.... "ULIMI ULIPONZA KICHWA..."

Wewe mkuu Pope, lazima ni "mtu mzima sana", maana maneno kama haya husemwa na wanaoelewa mambo mengi sana, yaani umeniogopesha sana mkuu, maana sijawahi kuona maneno mazito kama haya hapa JF!
 
Mkuu Lunyungu, ninakubaliana na maneno yako,

However, hoja nyingi kwenye hii topic zinaonyesha kuwa wengi wetu hapa JF sio wapiga kura, maana tunaonekana kutegemea miujiza huku tukiangalia kwa pembeni, wakuu tujimwage kuchukua fomu sisi wenyewe wana JF!
 
Kama tunaongelea utaifa mimi nadhani cha msingi ni kuwang'oa viongozi wabovu wawe CCM au Chama kingine chochote kile. Kamatulivyo ona mfano wa wabunge katika suala la richmond.
 
Mkuu Lunyungu, ninakubaliana na maneno yako,

However, hoja nyingi kwenye hii topic zinaonyesha kuwa wengi wetu hapa JF sio wapiga kura, maana tunaonekana kutegemea miujiza huku tukiangalia kwa pembeni], wakuu tujimwage kuchukua fomu sisi wenyewe wana JF!

FMES hapo juu wewe ndio uliyeniogopesha:) nilifikiri una kadi ya chama fulani vile!

Nakubaliana na papa!
 
Wewe mkuu Pope, lazima ni "mtu mzima sana", maana maneno kama haya husemwa na wanaoelewa mambo mengi sana, yaani umeniogopesha sana mkuu, maana sijawahi kuona maneno mazito kama haya hapa JF!

Mkuu am 32, anyway inawezekana ni mtu mzima sana ila kumbuka ukubwa wa pua si wingu wa kamasi maana hata Bungeni kuna watu wazima sana ambao wanaongea Pumba na kuna Vijana Kama Mh. Zito wanamwaga Point.

Naumia nikiona nguvu nyingi zinatumika wakati wa Kampeni na wananchi wanapokuja kusikiliza Kwaya au kuangalia Mbwembwe tunazokwenda nazo na sio Kusikiliza Sera!! Amini nakwambieni Mtu haelimishwi kuhusu Sera za Chama kwa kipindi cha Kampeni, huyu huyu anakusikiliza wewe leo na kesho anasikiliza watu wengine leo hapa umesema hili kesho umesema lile "Miluzi Mingi ilimpoteza Mbwa"

Ni imani yangu kabisa Upinzani wa kweli ndio mombozi wa Nchi hii, Hata leo wakiingia Chadema bado tunataka CCM kiwe chama cha Upinzani chenye nguvu. Tunachotaka kuwe na mtu wa kumnyooshea kidole mwenzie.

Kwani hakuna atakaye taka kufanya kosa ili apoteze nafasi aliyonayo, "Uoga wa kupoteza kiti ndio Chachu ya maendeleo yetu"
 
  • "kumbuka ukubwa wa pua si wingu wa kamasi
  • "Miluzi Mingi ilimpoteza Mbwa"

Papa hapo juu umeniacha hoi!:D
Point taken!
Ni imani yangu kabisa Upinzani wa kweli ndio mombozi wa Nchi hii, Hata leo wakiingia Chadema bado tunataka CCM kiwe chama cha Upinzani chenye nguvu. Tunachotaka kuwe na mtu wa kumnyooshea kidole mwenzie.

Kweli... Kidumu!
 
Mkuu Lunyungu, ninakubaliana na maneno yako,

However, hoja nyingi kwenye hii topic zinaonyesha kuwa wengi wetu hapa JF sio wapiga kura, maana tunaonekana kutegemea miujiza huku tukiangalia kwa pembeni, wakuu tujimwage kuchukua fomu sisi wenyewe wana JF!

Hapo mwanzo nilisha sema kabisa kwamba mwezi wa 7 narudi kujiunga rasmi na CHADEMA.
Mwaka 2009 nitafafanya utafiti wa siku 60 kuona uwezekano wa kushinda na 2010 nitachukua likizo ya miezi 6 na kujimwaga rasmi katika kinyang'anyiro cha Ubunge.

Mpinzani wangu wa SISIEMU ambaye mpaka sasa hajui mipango hii ajiandae tu.Sasa sijui atajiandaeje naje hajui nakuja.

Na si mbaya kama nikienda kuomba kibali cha kuchangisha fedha ya kampeni kutoka kwa wasamalia hapa majuu.

Tumejiweka nyuma kama mikia ya hayawani kwa muda mrefu mno, inatosha sasa.

Sisi ndiyo tutaleta mageuzi au hayaji kamwe.
 
Sisi ndiyo tutaleta mageuzi au hayaji kamwe.

Mkuu Sura,

Mimi ni ccm damu mkuu,

Mkuu Madilu,

Haya maneno yako hapo juu, ndio mwanzo na mwisho, hakuna wa kutufanyia ni lazima tuingie wenyewe, ni lazima hizi siku za karibuni tuandae semina rasmi ya wana-JF kushika hatamu, tukutane tuzungumze uso kwa uso, jina kwa jina hakuna es wala madilu, exactly who we are, hakuna uwt wala njagos, walahi siku inakuja!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom