Wapinzani acheni kuendeshwa na mihemko

mayaJr45

JF-Expert Member
May 12, 2016
560
205
Huenda ikawa ni lugha yenye ukakasi ila imebidi niitumie hivyo hivyo kwakua imebidi.Leo hii fuatilia kwenye social media ishu kubwa utasikia Sukari na Lugumi simply kwakua vimeongelewa vikasikika ila Nchi hii ina mambo mengi ambayo yanahitaji ukombozi wa wasomi na Wazalendo katika taifa ukiachilia mbali hali ya sasa watu wanaacha kufocus kwenye kada mbalimbali walizosomea kila mtu ni mwanaharakati ukiuliza mwanaharakati wa nn ?

Mazingira ,Haki za wanawake , kupinga mauwaji ya Albino utakuta wanaoeleweka wanadili na jambo gani ni kama asilimia 2 tu hivi .Wengine ni lolote litakalosikika anaruka nalonkimasai. Ila walipaswa kuwa wanaharakati wa kada walizosomea ili taifa liende mbele.

Biashara ya vyakula Tanzania inauchafu mwingi na michezo mingi michafu leo hii unasikia kuwa kuna uhaba wa sukari ila baada ya muda mfupi tegemea Kunaweza kutokea pia uhaba wa MCHELE .

Najua wapo watakao shtuka kusikia mchele ila wafanya biashara hao hao wa sukari ni hao hao wanaopewa vibali vya kuingiza MCHELE nchini kutoka nje.kinachofanyika kwa sasa ni MCHELE wetu mzuri wanaununua wanaugrade ule daraja la kwanza unapelekwa nje hasa Uarabuni kujustfy uwepo wa gape la mchele, na ule wa mwisho unaingizwa soko la ndani. Makontena yakienda UARABUNI hayarudi matupu yanarudi na MCHELE ambao unaelekea kwisha muda wake wa kutumika aubuliokwisha muda wake na kuingizwa nchini kiujanja ujanja hapo awali.

Nimeelezea hilo kwa ufupi kwa maana kubwa moja Serekali inafuatilia mambo mengi najua siku itafika kwenye mchele litatokea sakata kama la sukari tena maana wafanya biashara ni hao hao wa sukari.Wakulima wa mpunga watakua wananielewa vyema maana ndio wanunuzi wakubwa wa mpunga toka maeneo mbalimbali.Sitaki kuwataja kwa majina.

Hiyo itakua tena vita nyingine kubwa tu muda ukifika na serekali ikaamua kujikita kufuatilia jambo hilo kwa faida ya wakulima wetu.Kwanza wamechangia kushusha bei maana mtu mmoja anavikampuni ka 20 vya kununua mpunga wakienda kwa mkulima inaonekana watu wanashindana kumbe ni mtu huyo huyo mmoja hivyo kubalance bei na kununua kwa bei wanayotaka na kumfanya mkulima asifaidike na kazi ya mikono yake.

Namalizia kwa kwaambia wasomi tuwe wenye kuleta changamoto kuna mambo mengi kwenye jamii tumepelekwa kupata elimu ili tuikomboe jamii yetu kwa mengi huo ni mfano mmoja ila ipo mingi .
 
Wenda ikawa ni lugha yenye ukakasi ila imebidi niitumie hivyo hivyo kwakua imebidi.Leo hii fuatilia kwenye social media ishu kubwa utasikia Sukari na Lugumi simply kwakua vimeongelewa vikasikika ila Nchi hii ina mambo mengi ambayo yanahitaji ukombozi wa wasomi na Wazalendo katika taifa ukiachilia mbali hali ya sasa watu wanaacha kufocus kwenye kada mbalimbali walizosomea kila mtu ni mwanaharakati ukiuliza mwanaharakati wa nn ?Mazingira ,Haki za wanawake , kupinga mauwaji ya Albino utakuta wanaoeleweka wanadili na jambo gani ni kama asilimia 2 tu hivi .Wengine ni lolote litakalosikika anaruka nalonkimasai. Ila walipaswa kuwa wanaharakati wa kada walizosomea ili taifa liende mbele.

Biashara ya vyakula Tanzania inauchafu mwingi na michezo mingi michafu leo hii unasikia kuwa kuna uhaba wa sukari ila baada ya muda mfupi tegemea Kunaweza kutokea pia uhaba wa MCHELE .

Najua wapo watakao shtuka kusikia mchele ila wafanya biashara hao hao wa sukari ni hao hao wanaopewa vibali vya kuingiza MCHELE nchini kutoka nje.kinachofanyika kwa sasa ni MCHELE wetu mzuri wanaununua wanaugrade ule daraja la kwanza unapelekwa nje hasa Uarabuni kujustfy uwepo wa gape la mchele, na ule wa mwisho unaingizwa soko la ndani. Makontena yakienda UARABUNI hayarudi matupu yanarudi na MCHELE ambao unaelekea kwisha muda wake wa kutumika aubuliokwisha muda wake na kuingizwa nchini kiujanja ujanja hapo awali.

Nimeelezea hilo kwa ufupi kwa maana kubwa moja Serekali inafuatilia mambo mengi najua siku itafika kwenye mchele litatokea sakata kama la sukari tena maana wafanya biashara ni hao hao wa sukari.Wakulima wa mpunga watakua wananielewa vyema maana ndio wanunuzi wakubwa wa mpunga toka maeneo mbalimbali.Sitaki kuwataja kwa majina.

Hiyo itakua tena vita nyingine kubwa tu muda ukifika na serekali ikaamua kujikita kufuatilia jambo hilo kwa faida ya wakulima wetu.Kwanza wamechangia kushusha bei maana mtu mmoja anavikampuni ka 20 vya kununua mpunga wakienda kwa mkulima inaonekana watu wanashindana kumbe ni mtu huyo huyo mmoja hivyo kubalance bei na kununua kwa bei wanayotaka na kumfanya mkulima asifaidike na kazi ya mikono yake.

Namalizia kwa kwaambia wasomi tuwe wenye kuleta changamoto kuna mambo mengi kwenye jamii tumepelekwa kupata elimu ili tuikomboe jamii yetu kwa mengi huo ni mfano mmoja ila ipo mingi .
downloadfile-23.jpeg

bora miyeyuko kuliko ccm inaendeshwa na watu kama hao

swissme
 
Umejiunga Thursday,ila your tone in your writings naifananisha na mtu very common in here!by the way:
mauwaji=mauaji
 
Huwezi kutufundisha siasa wewe.! Kwa taarifa yako huo mchele utakosekana tu wakati ukifika maana tayari naskia nako wamepiga marufuku mchele kutoka nje. Ujinga wa CCM unaendelea. Huwezi kuzuia mtu askuletee chakula kwenye nchi! Hata marekani kuna bidhaa za nchi nyingine.
 
Heri ya ccm Ina viongozi wenye elimu inayojulikana. Mbowe Ana elimu gani 0 zero form six yaani round about shame on you Na tukianza kuchunguza mabebi mtashangas

Wewe mwenye elimu inayoeleweka life wise unaweza jilinganisha na Mbowe? Kwani lengo la elimu ni nini? Kama unaweza kuwa na good life bila elimu then where is the problem? Usikariri
 
Niwashauri Wapinzani hata pale Wanaikosoa Serikali au kudadavua jambo fulani.Hawa kama Vyama venye Sera na Ilani zao.Na suala ambalo wanaikomalia Serikali Huwa ni mahala muafaka kwao Kupenyeza Sera yao na hata Ilani yao kimkati wangefanyaje jambo linalozungumziwa na kupigiwa kelele.Sioni Mantiki ya wao kulalama na kususia ima kuzomea mjengoni.Ikumbukwe kuna baadhi ya wabunge wa Upinzani huongea hoja ambayo Serikali huibeba na kuifanyia kazi.Inawezekana kwa minajili ya Ustawi wa Nchi yetu.Niseme wanavyojieleza na staili walivyoiwasilisha hoja ni kama wana Crush.Na toka Day one waliudhihirishia Umma wa Watanzania wao ni watu/Viongozi wa kaliba ya namna gani.Niwaulize tu kuwa Kiongozi hajalishi wa Chama cho chote unapaswa kufanya nini?Kitabia kifikra,kimaadili,Nidhamu,Uvaaji hata Kusema? Natoa hoja
 
View attachment 348017
bora miyeyuko kuliko ccm inaendeshwa na watu kama hao

swissme
Hivi wabunge wasiojua haki yao ya kisiasa kwenye chama chao cha chadema wakaamua kugawa penzi ili wateuliwe nao utawaita wameelimika? Ushahidi wa swala hili ni tuhuma zinazomkabili Salum Mwalimu na John Lema kwamba walidai rushwa kwa hawa mabeiby ikiwamo ngono
Pili wabunge wasiojua haki zao za kiraia inayotaka kuwa mtuhumiwa wa kike hukaguliwa na askari wa kike tena falagha. Wabunge(viti maalum chadema) hawa kwa kuwa wamo humo kutoa penzi wao kushikwa na wanaume siyo swala la falagha, hivyo kukubali kupekuliwa na askari wa kiume hadharani kwa kuvuliwa nguo za ndani. Hayo yanathibitishwa na Kubenea pale alipoomba muongozo, mnajua alichokisema.
Sasa hawa wabunge wa aina hii hata kama walipata daraja la kwanza katika eleimu ya sekondari. Kwa matukio haya wanayofanya hiyo elimu inawasaidia nini?
 
natumaini wewe pia ni mmoja wa hao madada

swissme
 
Umejiunga Thursday,ila your tone in your writings naifananisha na mtu very common in here!by the way:
mauwaji=mauaji
very poor english ever to come across with .kwani umelazimishwa kutumia lugha hiyo na vyuo vyako vya uchochoroni ?jipange ila na kesho uje
 
halafunkwann watanzania tukisahau tunasahau wote kwa Pamoja .

ivi Stanbic walisemaje Kuhusu zile account za Escrow .
Richmond issue iliishaga . ?
Radar je . ..au mm ndio siko update ..

sasa ni Lugumi na Sukari . ... mbaya zaidi tunasahau wote ..na Viongozi wa upinzani nao wanasahau Hivyo hivyo . tunahitaji sindano Moja kutoka Mataifa ya mbali
 
Heri ya ccm Ina viongozi wenye elimu inayojulikana. Mbowe Ana elimu gani 0 zero form six yaani round about shame on you Na tukianza kuchunguza mabebi mtashangas

Hao wasomi walioko ccm wameisadia nini nchi hii? Mbona mpaka toothpick tunaagiza nje? Acheni sifa za kijinga jamani. Leo hii hiyo ccm yenye wasomi ndio iliyoongoza nchi mpaka hapa ilipo. Kila wakati wanakuja na kauli mbiu, mara siasa ni kilimo, kilimo kwanza, maisha bora kwa kila mtanzania, ari zaidi kasi zaidi, sasa hivi ni mapinduzi ya viwanda. Lakini ukiangalia yoote ni hadithi ndefu kwani hakuna mtu ana maisha duni kama mkulima. Leo kuhubiri mapinduzi ya viwanda bila kuwekeza nguvu kwenye kilimo ni kama kuwafanya wananchi wamechoka kufikiri. Sasa hapa ukisifia kuna wasomi huko ccm huoni ni kama unajitia aibu tu?
 
Back
Top Bottom