Wapinzani acheni kucheza ngoma za CCM, wote ni walewale

Jumong S

JF-Expert Member
Jul 3, 2013
6,324
2,000
Nashangaa kwa sasa Chadema na vyama vingine vya siasa mpo bize kumpigia vigelegele Mama President as if ni mwanachama cha Hashim Rungwe kaingia Ikulu, mind u, CCM ni ile ile na ndio bado iko madarakani. CCM haijawahi kuwa fair kwa Upinzani nchi hii.

Huu ni wakati wa Upinzani kujenga na kurejesha imani kubwa kwa wananchi. Waje na mbinu mbadala za kuwashawishi wananchi wawachague. Come 2025, mkiendelea na hivi vigelegele mnavyokazania CCM inashinda kiulaini.

Mama ni M-CCM wa zaidi ya 15 yrs, kaongoza na Magufuli 5 yrs, now ni rais. Yes, kuna vichaka vya Magu ataviwasha moto, lakini yote ni kwa faida ya CCM, trust me!

Pambaneni mitandaoni, pambaneni majimboni, onesheni CCM inaboronga wapi na nyie mtarekebisha nini ikiwa mtapata japo ubunge again.

Kumbuka: Mkimsifu sana Mama, mnaisifia CCM ile ile inayowasurubu!!

Kazi kwenu!
 
Lupweko

JF-Expert Member
Mar 26, 2009
14,587
2,000
CCM ni ile ile, lakini kuna moja inazipigia ndege makofi na vigelegele, na nyingine inasema zinaleta hasara miaka mitano mfululizo, moja inamteua fisadi nyingine inamtengua fisadi huyo huyo!
 
denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
5,668
2,000
Wataamka tu ikiwa tayari too late.

Huyu mama now ana score marks toka kila upande, kuanzia kwa upinzani wenyewe, magazeti, na CCM wenzake, wananchi nao wanaliona hili. Siku wapinzani wakiamka waseme tunataka Katiba Mpya wakati mama anaendelea ku score marks kwa utendaji wake hali ya wapinzani itakuwa ngumu zaidi, wananchi wengi watakuwa upande wa Rais.

Nawashangaa mara hii wameshaisahau Katiba Mpya itakayo wa-set free hata hao wanaoishi ukimbizini, now wapo huko wameridhika kuandika tu mitandaoni, next time akija Rais mgumu watarudi tena ukimbizini kwa hii katiba tuliyonayo, wanasahau Magufuli aliitumia hii katiba iliyopo kuwa vile alivyokuwa.

Wanampa Rais kazi nyepesi anazoonekana kuzimudu vyema kama utawala bora ( ACT wameshinda jana uchaguzi mdogo Znz), na hata ukiukwaji haki za binadamu naamini Rais mpya ataondoa hili, it's only a matter of time from now, ata score tena marks watamshangilia.

Wakija kuamka itakuwa tayari close na 2025, waanze kuidai Katiba Mpya uchaguzi mkuu ukikaribia, then watashiriki uchaguzi na Katiba ya zamani wapate wabunge 50 and above kule bungeni maisha yaendelee, jamaa sidhani kama wanaikumbuka ikulu tena.

Hapa hakuna kusubiri siku 100, zinaweza kwisha hizo bado pasiwepo na anything concrete kuwapelekea wananchi, sijui watampa siku 100 nyingine, wakati Rais anaendelea ku-score marks from all different angles, wakati wakudai Katiba Mpya ni sasa, kumshangilia Rais waachiwe CCM.

Hili linasababishwa na wengi upinzani kufuata akili/mawazo ya wachache twitter, watu wajifunze kufikiria kwa kutumia akili zao, vinginevyo mtarudishwa utumwani na hao hao mnaowaamini, wale wakipata ubunge kwao unawatosha.
 
shinyangakwetu

JF-Expert Member
Jun 25, 2015
1,917
2,000
Hakuna anaesema mama ni chadema, ila hawezi kua arrogant kama marehemu.
Hata jana hakumfokea mkurugenzi wa bandari,
Aliagiza kwa upole kabisa
Nashangaa kwa sasa Chadema na vyama vingine vya siasa mpo bize kumpigia vigelegele Mama President as if ni mwanachama cha Hashim Rungwe kaingia Ikulu, mind u, CCM ni ile ile na ndio bado iko madarakani. CCM haijawahi kuwa fair kwa Upinzani nchi hii.

Huu ni wakati wa Upinzani kujenga na kurejesha imani kubwa kwa wananchi. Waje na mbinu mbadala za kuwashawishi wananchi wawachague. Come 2025, mkiendelea na hivi vigelegele mnavyokazania CCM inashinda kiulaini.

Mama ni M-CCM wa zaidi ya 15 yrs, kaongoza na Magufuli 5 yrs, now ni rais. Yes, kuna vichaka vya Magu ataviwasha moto, lakini yote ni kwa faida ya CCM, trust me!

Pambaneni mitandaoni, pambaneni majimboni, onesheni CCM inaboronga wapi na nyie mtarekebisha nini ikiwa mtapata japo ubunge again.

Kumbuka: Mkimsifu sana Mama, mnaisifia CCM ile ile inayowasurubu!!

Kazi kwenu!
 
Jumong S

JF-Expert Member
Jul 3, 2013
6,324
2,000
Hakuna anaesema mama ni chadema, ila hawezi kua arrogant kama marehemu.
Hata jana hakumfokea mkurugenzi wa bandari,
Aliagiza kwa upole kabisa
Awe Arrogant au awe mpole, bado ni mwana CCM na atafanya yote kwa Sifa ya CCM!
Kikwete was so diplomatic, ila wapinzani walimnanga sana! Magu kaja kama moto wa vichakani, wakamnanga na akawakandamiza sana! Sasa maza kaja kivingine, bado atawaliza tu!

Adui mkuu wa upinzani ni CCM!
 
Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
7,568
2,000
CCM must go. Hata iwe chini ya malaika tofauti na yule aliyepita. Bado kinatakiwa kistaafishwe. Kimeitawala nchi yetu kwa miaka mingi na kuwafanya wananchi walio wengi kuwa na umaskini wa kutupwa wa kipato na hivyo kushindwa kuijua kesho yao.
 
idawa

JF-Expert Member
Jan 20, 2012
24,229
2,000
Kabla ya yote tunataka Taifa lenye Afya mshikamano na umoja kwa mstakabali wa vizazi vijavyo.

Hatutaki kuja kuchukua nchi iliyogawanyika vipande vipande halafu tushindwe kutawala.
 
Mkwawe

JF-Expert Member
Jun 10, 2016
1,937
2,000
CCM must go. Hata iwe chini ya malaika tofauti na yule aliyepita. Bado kinatakiwa kistaafishwe. Kimeitawala nchi yetu kwa miaka mingi na kuwafanya wananchi walio wengi kuwa na umaskini wa kutupwa wa kipato na hivyo kushindwa kuijua kesho yao.
Hata ningependa iwe hivyo ila mbadala wake isiwe chadema au act
 
Jumong S

JF-Expert Member
Jul 3, 2013
6,324
2,000
Kabla ya yote tunataka Taifa lenye Afya mshikamano na umoja kwa mstakabali wa vizazi vijavyo.

Hatutaki kuja kuchukua nchi iliyogawanyika vipande vipande halafu tushindwe kutawala.
Kwa hiyo CCM ndo ikuunganishie watu? Thubutu! Fight the enermy even if he is so down!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom