Wapinga mabadiliko na wanufaika wa mfumo tawala "status quo" Tanzania hawawakilishi uhafihidhina

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,574
46,150
Maridhiano ya CCM na CHADEMA hayajakubalika na wote ndani ya vyama hivyo viwili. Rais Samia amekiri na kuwaita watu wanaoyapinga maridhiana hayo ndani ya chama chake na CHADEMA pia kama "wafahidhina". Hiyo imepeleka hata baadhi ya vijana wasaka fursa kujitokeza hadharani na kudai wao ndio wafahidhina wenyewe.

Hata hivyo kiuhalisia hili neno ufahidhina katika siasa kama za nchi yetu, Africa na zisizo na demokrasia imara linatumika isivyostahili kuwakilisha wapinga mabadiliko na wanufaikaji wa mfumo ulipo "status quo" tu.

Wafahidhina halisi katika chimbuko lake ni watu walio na misimamo ifuatayo;

1. Wanaopendelea serikali ndogo tena ambayo mamlaka na utendaji wake unaonekana zaidi katika ngazi za chini(serikali za mitaa) kuhakikisha tu kuna order inayowapa raia fursa ya kuendesha maisha yao watakavyo na sio kuwaamulia au kuwaelekeza cha kufanya . Wafahidhina halisi sio watu wanaotaka kuona serikali inakuwa na watu wengi kutoa huduma za kijamii kama Afya, maji, umeme n.k

2. Uhuru na haki za raia mmoja mmoja zaidi zaidi kupewa kipaumbele na kuheshimiwa kuliko manufaa ya jamii nzima au maslahi ya taifa .Wafahidhina halisi ni watu wanaoamini kwamba hata kama haki ya mtu mmoja inaleta madhara kwa jamii kubwa bado serikali haipaswi kuingilia kuiminya. Mfano ni Marekani katika suala la haki ya umilikaji wa bunduki.

3. Udhibiti mdogo wa uchumi na maisha ya watu kwa ujumla(Limited regulations). Wafahidhina halisi ni watu wa "laissez-faire", wao hawapendi mambo ya miongozo, kanuni na taratibu hasa zinapoingilia au kutatiza kutengeneza faida.

4. Matumizi kidogo ya serikali, kubana matumizi na serikali kutokopa sana. Wafahidhina halisi kwao sekta binafsi ndio inapaswa kuwa injini na kutoa muelekeo wa nchi na kwa maana hiyo hakuna sababu ya nchi kutenga bajeti kubwa na kujiingiza katika madeni kutoa huduma za msingi kama maji, umeme n.k

5. Msisitizo wa Katiba na utawala wa sheria juu ya kila kitu. Wafahidhina halisi katiba inapaswa ku overide kila kitu iwe sera, kanuni au matamko ya viongozi hata kama vitakuwa na faida kwa jamii kwa wakati huo.

6. Katika masuala ya kijamii; Dini kupewa nafasi ya mbele katika mambo ya jamii, kujihusisha sana na mambo ya mavazi ya wanawake, kupinga ushoga, kutopendelea wanawake kuwa viongozi na mambo mengine kama hayo.

Katika sifa hizi ukiondoa namba sita ni wapi utawaweka wanaoitwa Wafahidhina hapa Tanzania? Ni dhahiri kwamba hichi kinachoitwa ufahidhina na wanaoitwa wafahidhina Tanzania ni hadaa na matumizi mabovu ya maneno. Wengi wao ni opprtunists tu wa mfumo wenye hofu ya kupungukiwa fursa kutokana na mabadiliko. Hao ni wahafidhina uchwara waliojificha katika kichaka cha uhafidhina.
 
Back
Top Bottom