Wapigadebe Stendi ya Msamvu wana ushawishi kuliko wa stendi zote nchini

matunduizi

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
6,570
15,314
Natanguliza pole kwa wote waliolishwa mbwa hapo nje ya stand Msamvu. Nimefanikiwa kukagua eneo liko swari na kuna kijana anauza mishkaki halali ya nyama inayosadikiwa kuwa ya ng'ombe. Ila nilibaki na swali tu, ikiwa moro wametafuna mbwa hivyo sio zaidi Dar ambako watu wanakula hovyo vimishikaki kwenye chelewa na vindizi vya kuchoma?

Turudi madani
Aisee hii ni zaidi ya mara ya 20 napita hapa 'msamvu' hawa wakaribishaji sijawahi kuwaona stand yoyote nchini. Wanabidii ya ushawishi na hawakati tamaa kirahisi.

1: Hata kama sura wengine ni za kiteja kidogo lakini wanalugha nzuri, yakiungwana.

2: Waongo sana, ila wanavyokushawishi kwa uongo utapenda. " Nimewahi panda BM naambiwa ina "Maliwato ndani". Jamaa nikamkaba twende nihakikishe alikuwa na ujasiri wa kutoka nje hadi mlangoni mwa Bus, kwa ujasiri na ushawishi ule nikamwambia basi sawa kuingia hakuna cha maliwato wala maliwata. Ila Yenye maliwato huwa ipo.

3: Hii tabia ya ucustomer care wameambukizana wahudumu wote. Wale wa msosi, tax, machinga, kila mtu yuko active kupitiliza.

Nimewahi kufika stand nyingi, ila msamvu nawakubali sana kuliko hata mbezi mwisho ambako watu wanakomaa kidogo tu anakata tamaa na kutafuta mtu mwingine. Kwa sababu ya usanii mwingi ambao wamenifanyia kwa kuwaamini japo siwalaumu nimewawekea formula kali sana kiasi kwamba hawanisumbui tena bila idhini yangu.

Leo walipojua nahitaji kuchaji, nimepelekwa siti ya mbele ya kosta ya kwenda wilayanu nikaletewa na usb cable nikaunganishwa kwenye radio ili niendelee kula JF. Kuuliza wenzagu wamo tangu saa nne, mimi naambiwa dakk 15 kwa heshima yangu wataondoka ingawa tumeondoka baada ya saa. Wanasema hali mbaya sana leo.

Hawa jamaa wako vzri aisee, ndio maana wanalisha watu mbwa, watu wanauziwa nazi za kuoza, powerbank zenye 0 charging capacity, battery mpya za simu ambazo hazijai na bado watu wanatoa pesa. Hasa wale panic buyers.
 
Ukiwa makini tega sikio usikilize/jifunze ladhuzi ya kiswahili chao utajua ni wazawa wa kutoka kisaki, kinole, mgeta, n.k ni mapromoter wazuri kama Bwakila mwenyewe, kwa hali kama hiii hivi unaachaje kupanda BUS lao hata kama halina kiyoyozi?
 
Natanguliza pole kwa wote waliolishwa mbwa hapo nje ya stand Msamvu. Nimefanikiwa kukagua eneo liko swari na kuna kijana anauza mishkaki halali ya nyama inayosadikiwa kuwa ya ng'ombe. Ila nilibaki na swali tu, ikiwa moro wametafuna mbwa hivyo sio zaidi Dar ambako watu wanakula hovyo vimishikaki kwenye chelewa na vindizi vya kuchoma?

Turudi madani
Aisee hii ni zaidi ya mara ya 20 napita hapa 'msamvu' hawa wakaribishaji sijawahi kuwaona stand yoyote nchini. Wanabidii ya ushawishi na hawakati tamaa kirahisi.

1: Hata kama sura wengine ni za kiteja kidogo lakini wanalugha nzuri, yakiungwana.

2: Waongo sana, ila wanavyokushawishi kwa uongo utapenda. " Nimewahi panda BM naambiwa ina "Maliwato ndani". Jamaa nikamkaba twende nihakikishe alikuwa na ujasiri wa kutoka nje hadi mlangoni mwa Bus, kwa ujasiri na ushawishi ule nikamwambia basi sawa kuingia hakuna cha maliwato wala maliwata. Ila Yenye maliwato huwa ipo.

3: Hii tabia ya ucustomer care wameambukizana wahudumu wote. Wale wa msosi, tax, machinga, kila mtu yuko active kupitiliza.

Nimewahi kufika stand nyingi, ila msamvu nawakubali sana kuliko hata mbezi mwisho ambako watu wanakomaa kidogo tu anakata tamaa na kutafuta mtu mwingine. Kwa sababu ya usanii mwingi ambao wamenifanyia kwa kuwaamini japo siwalaumu nimewawekea formula kali sana kiasi kwamba hawanisumbui tena bila idhini yangu.

Leo walipojua nahitaji kuchaji, nimepelekwa siti ya mbele ya kosta ya kwenda wilayanu nikaletewa na usb cable nikaunganishwa kwenye radio ili niendelee kula JF. Kuuliza wenzagu wamo tangu saa nne, mimi naambiwa dakk 15 kwa heshima yangu wataondoka ingawa tumeondoka baada ya saa. Wanasema hali mbaya sana leo.

Hawa jamaa wako vzri aisee, ndio maana wanalisha watu mbwa, watu wanauziwa nazi za kuoza, powerbank zenye 0 charging capacity, battery mpya za simu ambazo hazijai na bado watu wanatoa pesa. Hasa wale panic buyers.
Umenikumbusha hapo Moro sitapasahau,walinipandisha cost kwenda Mbeya.waniliniambia bro kuna basi kubwa linatokea Tanga walienda msibani,sasa kuna siti mbili.hiyo haina kusimama popote so utawahi kufika Mbeya. Baada ya kuelewana nao,si nikaacha mabasi yote yakapita,kuja kutahamaki ni ki costa flan hiv ambacho kinafanya dala dala pale mbeya wao huita mzunguko ndiyo kimefika kweli kutoka Tanga kupeleka msiba.

Sina jinsi,muda umeenda na lazima niende.wakaniingiza humo,na wao wakavuta chao.nilikuja jua nimejichanga baada ya kuondoka hapo stendi na kunote speed yake.safari ya mbeya ilikuwa ndefu saana kiwahi kutokea
 
Watu wa morogoro ni wakarimu sana, ni moja ya sehemu ambazo natamani kuja kuzeekea.
Morogoro napapenda sana kuna ukarimu wa ajabu.

Niliwahi kukodi mashamba kwa mama mmoja hivi nilikuwa nikienda shambani kwa sababu ilikuwa kijijini sana ukilala pale mama anakuachia chumba chake anaenda kulala na wajukuu.

Na mimi nikawa nabeba mazaga yote ya mjini nampelekea.

Ila ndiyo hivyo nilishapoteza mawasiliano nae.
 
Back
Top Bottom