Wapiga makofi Bungeni

Ze Rock

JF-Expert Member
Sep 15, 2020
273
1,000
Habarini za muda huu wana JF,

Hoja yangu kuu hapa ni yale makofi wanayopiga wabunge pindi mtu anapotoa hoja au anapojibu hoja/swali n.k

Nimeona niulize wezangu kama munaelewa mantiki ya wapiga makofi hasa pale mtu anapoongea hoja dhaifu kabisa, nilitegemea wabunge watulie na kusikitikia hoja zisizo na mashiko ila cha ajabu anapigiwa makofi kama vile ameongea kitu chenye mashiko sana.

Kwani ni lazima kila anayesimama kuongea akimaliza lazima asindikizwe na kupigiwa makofi?

Kama vipi kuwe na kitufe kwenye meza ya spika mtu akiongea vitu visivyo na tija kwa Taifa na hasa akitoka nje ya mada kwa kile wanacho jadili abonyeze iwe kiashiria cha kuonyesha ni hoja dhaifu na hapaswi kupigiwa makofi na kwa yule anayeongea point apewe green light au kuashiria anaweza akaungwa mkono kwa kupigiwa makofi.

Jamani Wabunge kuweni wazalendo kwa kujadiri vitu vyenye tija kwa maslai ya wananchi na Taifa, munapowasilisha hoja zenu mukumbuke ninyi ni wawakilishi wetu kwa hiyo mutulie kwenye utoaji wa hoja, hoja ziwe zenye mashiko kwa maslai mapana ya Taifa na wananchi. Muache kupiga piga mkofi hovyo hovyo kwa hoja zisizo na mashiko tunashindwa kuwaelewa huku wanachi wenu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom