Wapiga Kura Wenye haki ya kupiga kura wangepiga Tungekuwa na Serikali tofauti na hii Tuliyonayo

Mkenazi

Senior Member
Apr 11, 2011
124
43
Elimu kuhusu uchaguzi kwa raia wote wa Tanzania.

Utangulizi
Ni miaka 19 sasa tangu mfumo wa vyama vingi umeanza hapa nchini (1992-2011) na tumeishafanya uchaguzi mkuu mara 4 kwa madiawani, wabunge na rais pamoja na chaguzi nyingine ndogo ndogo kuziba nafasi zilizoachwa wazi kwa sababu mbali mbali. Katika chaguzi zote hizo tumeshuudia idadi ndogo ya wapiga kura ikilinganishwa na wale waliojiandikisha, hili ni tatizo kubwa na ndipo nitakapojikita zaidi.
 1. Uchaguzi (Voting): Kwa maana halisi ya kuchagua
· Kukubali mtu/kitu, chama/mfumo fulani kwamba unakufaa. Mtu asiposhiriki kupiga kura ameruhusu asichokitaka kipite.
· Kukataa mtu/kitu, chama/mfumo fulani kwamba haufaii kwa kura yako ile ile uliyompigia unayemtaka. Mtu asiposhiriki kupiga kura anakuwa ameruhusu asichokitaka kipite.
· Kuonyesha hisia zako kivitendo kuwa hauridhishi na utendaji mzima wa yule unayemtaka/unachokipenda kama kilikuwa na nafasi hiyo kabla ya uchaguzi. Usipopiga kura hawezijua mapungufu yake na kujirekebisha na hivyo kushiriki kuendeleza yasiyoridhisha kwa kutopiga kura.
· Kutimiza haki yako ya kikatiba ya kushiriki mamlaka ya wananchi ya kuweka/kuondoa mtu/chama/mfumo madarakani na hivyo kutoruhusu watu wachache kuweka utawala madarakani na wewe unabaki unalalamika tu.
 1. Nani ni mpiga kura?
“Entitlement to Register
Any citizen of the age of 18 years or above has the right to register as voter and to vote in any public election in Tanzania.

 1. Mambo ya kisheria yanayokunyima haki ya kupiga kura
A citizen loses the right to vote if he or she is:
a. Under a declaration of allegiance to some country other than Tanzania;
b. Under a sentence of death imposed by any court in Tanzania;
c. Under sentence of imprisonment for a term exceeding six months;
d. disqualified from registering as a voter for being convicted for corrupt offences in elections.
e. Declared to be of unsound mind
(Constitution of the United Republic of Tanzania, 1977 Art.5.)”4. Upigaji kura 2005 na 2010
Upigaji Kura

2005

2010

Ongezeko/Pungua kati ya 2005/2010
Idadi
% Ya waliojiandikisha
Idadi

% Ya waliojiandikisha

Valid votes (Kura halali)

11,014,855

69%

8,376,022

46%

2,638,833 (24%)

Spoilt votes (Zilizoharibika)

495,290

3%

227,241

1%

-268,049 (54%)​

Total voted (Jumla ya kura zilizopigwa)

11,510,145

72%

8,603,263

47%

-2,906,882 (-34%)

Did not vote – (Hawakupiga kura)

4,400,768

28%

9,411,404

52%

5,010,636 (53%)

Total registered Voters

15,910,913

100%

18,014,667

100%

2,103,754 (13%)
Kutoka kwenye jedwali hapo juu tunaona yafuatayo kati 2005 na 2010:
 1. Idadi ya waliojiandikisha kuwa wapiga kura iliongezeka kwa watu 2,103,754 sawa na ongezeko na 13% (2005 to 2010)
 2. Idadi ya wasiopiga kura iliongezeka kwa watu 5,010,636 sawa na ongezeko la 53% pamoja na kwamba idadi ya wenye haki kupiga kura kuongezeka kwa 13% . Idadi hii ya wasiopiga kura ni sawa na 58.2% ya waliopiga kura 2010. Ni idadi kubwa kuliko kura zilizoiweka madarakani serikali inayotawala sasa.
 3. Idadi ya kura zilizoharibika ilipungua kwa 268,049 (54%) labda pengine kwa sababu ya kupungua kwa wapiga kura.
 4. Idadi ya kura halali ilipungua kwa 2,638,833 (24%)
 5. Idadi ya kura halali ilipungua kwa 2,906,882 (34%)
Kutoka kwenye jedwali hapo juu tunaona yafuatayo Kwa 2005:
 1. Upigaji kura – 72% ya waliojiandikisha (2005) - 47% ya waliojiandikisha (2010)
 2. Kura halali - 69% ya waliojiandikisha (2005) - 46% ya waliojiandikisha (2010)
 3. Kura zilizoharibika - 3% ya waliojiandikisha (2005) - 1% ya waliojiandikisha (2010)
 4. Kutopiga kura - 28% ya waliojiandikisha (2005) - 52% ya waliojiandikisha (2010)
Je hii tafakari inawakilisha nini?
 1. Kama wenye haki ya kupiga kura na hawakupiga wangetumia haki yao na wote kuwapa chama tawala kingekuwa kinajiamini zaidi na bila hofu yoyote ya nguvu ya umma.
 2. Kama wenye haki ya kupiga kura na hawakupiga wangetumia haki yao na wote kuwapa chama kimojawapo cha upinzani basi tungekuwa na serikali ya Chama tofauti na CCM.
 3. Kama wenye haki ya kupiga kura na hawakupiga kura wangetumia haki yao na wote kuamua kuharibu kura kwa kutoridhishwa na vyama vilivyoweka wagombea ingetupa picha kwamba chama/wagombea mbadala wanatakiwa.
 4. Na kama wote wangepiga kura kwa kila mtu kuchagua amtakaye kati ya waliogembea tungekuwa na picha halisi ya siasa za yanzania na hivyo kila mwanasiasa wakiwemo walio madarakani wangejipanga vizuri na pengine kuondoa uwezekano wa vurugu
Kuna uwezekano mkubwa Iko serikali tofauti na hii iliyo madarkani kama waliojima haki yao ya kupiga kura wangejitendea haki.
WADAU WOTE TOENI ELIMU YA UMUHIMU WA KUPIGA KURA, HAITOSHI KUWA NA WATU WENGI KWENYE MIKUTANO WASIOWEZA KUAMUA HATIMA YAO KWA KUPIGA KURA.
 
Attachments

 • Wadau toeni Elimu ya umuhimu wa kupiga kura.pdf
  54.9 KB · Views: 92

makwimoge

JF-Expert Member
Apr 14, 2011
298
41
Elimuya kupiga kura imekwisha eleweka
Tatizo no huo uongo wa takwimu,haikubaliki hata siku moja kuniambia kuwa idadi ya wapiga kujiandikisha waongezeke halafu wapigaji wapungie ..........haihitaji digrii yeyote hapa .......#@!*?%
 
politiki

JF-Expert Member
Sep 2, 2010
2,376
1,504
kwako mkenazi,
naomba kuuliza kulingana na uchambuzi wako murua, unafikiri kupungua kwa wapiga 2010 kulinganisha 2005 kulisababishwa na nini wakati
kitakwimu ilibidi waongezeke kwa sababu idadi ya watu inaongezeka haipungui ?

Malalamiko ya Dr.Slaa ya kuchakachuliwa matokeo ya urais yanaweza kuwa na nafasi gani ktk hizi namba hasa ukizingatia NEC ilikataa kata kata
kura za urais zisiasabiwe vituoni zilikopigwa ??

nashukuru sana kwa uchambuzi wako kwani umenifanya ni think kitu ambacho kinajenga kuelimika kwa maana ili uelimike you got to think.
 
Mimibaba

JF-Expert Member
Jul 1, 2009
4,558
1,285
Elimu kuhusu uchaguzi kwa raia wote wa Tanzania.

Utangulizi
Ni miaka 19 sasa tangu mfumo wa vyama vingi umeanza hapa nchini (1992-2011) na tumeishafanya uchaguzi mkuu mara 4 kwa madiawani, wabunge na rais pamoja na chaguzi nyingine ndogo ndogo kuziba nafasi zilizoachwa wazi kwa sababu mbali mbali. Katika chaguzi zote hizo tumeshuudia idadi ndogo ya wapiga kura ikilinganishwa na wale waliojiandikisha, hili ni tatizo kubwa na ndipo nitakapojikita zaidi.

 1. Uchaguzi (Voting): Kwa maana halisi ya kuchagua
· Kukubali mtu/kitu, chama/mfumo fulani kwamba unakufaa. Mtu asiposhiriki kupiga kura ameruhusu asichokitaka kipite.
· Kukataa mtu/kitu, chama/mfumo fulani kwamba haufaii kwa kura yako ile ile uliyompigia unayemtaka. Mtu asiposhiriki kupiga kura anakuwa ameruhusu asichokitaka kipite.
· Kuonyesha hisia zako kivitendo kuwa hauridhishi na utendaji mzima wa yule unayemtaka/unachokipenda kama kilikuwa na nafasi hiyo kabla ya uchaguzi. Usipopiga kura hawezijua mapungufu yake na kujirekebisha na hivyo kushiriki kuendeleza yasiyoridhisha kwa kutopiga kura.
· Kutimiza haki yako ya kikatiba ya kushiriki mamlaka ya wananchi ya kuweka/kuondoa mtu/chama/mfumo madarakani na hivyo kutoruhusu watu wachache kuweka utawala madarakani na wewe unabaki unalalamika tu.
 1. Nani ni mpiga kura?
"Entitlement to Register
Any citizen of the age of 18 years or above has the right to register as voter and to vote in any public election in Tanzania.

 1. Mambo ya kisheria yanayokunyima haki ya kupiga kura
A citizen loses the right to vote if he or she is:
a. Under a declaration of allegiance to some country other than Tanzania;
b. Under a sentence of death imposed by any court in Tanzania;
c. Under sentence of imprisonment for a term exceeding six months;
d. disqualified from registering as a voter for being convicted for corrupt offences in elections.
e. Declared to be of unsound mind
(Constitution of the United Republic of Tanzania, 1977 Art.5.)"4. Upigaji kura 2005 na 2010
Upigaji Kura

2005

2010

Ongezeko/Pungua kati ya 2005/2010
Idadi
% Ya waliojiandikisha
Idadi

% Ya waliojiandikisha
Valid votes (Kura halali)

11,014,855

69%

8,376,022

46%

-2,906,882 (-34%)
Spoilt votes (Zilizoharibika)

495,290

3%

227,241

1%

-268,049 (54%)
Total voted (Jumla ya kura zilizopigwa)

11,510,145

72%

8,603,263

47%
Did not vote – (Hawakupiga kura)

4,400,768

28%

9,411,404

52%

5,010,636 (53% )
Total registered Voters

15,910,913

100%

18,014,667

100%

2,103,754 (13%)

Kutoka kwenye jedwali hapo juu tunaona yafuatayo kati 2005 na 2010:
 1. Idadi ya waliojiandikisha kuwa wapiga kura iliongezeka kwa watu 2,103,754 sawa na ongezeko na 13% (2005 to 2010)
 2. Idadi ya wasiopiga kura iliongezeka kwa watu 5,010,636 sawa na ongezeko la 53% pamoja na kwamba idadi ya wenye haki kupiga kura kuongezeka kwa 13% . Idadi hii ya wasiopiga kura ni sawa na 58.2% ya waliopiga kura 2010. Ni idadi kubwa kuliko kura zilizoiweka madarakani serikali inayotawala sasa.
 3. Idadi ya kura zilizoharibika ilipungua kwa 268,049 (54%) labda pengine kwa sababu ya kupungua kwa wapiga kura.
 4. Idadi ya kura halali ilipungua kwa 2,906,882 (34%)
Kutoka kwenye jedwali hapo juu tunaona yafuatayo Kwa 2005:
 1. Upigaji kura – 72% ya waliojiandikisha (2005) - 47% ya waliojiandikisha (2010)
 2. Kura halali - 69% ya waliojiandikisha (2005) - 46% ya waliojiandikisha (2010)
 3. Kura zilizoharibika - 3% ya waliojiandikisha (2005) - 1% ya waliojiandikisha (2010)
 4. Kutopiga kura - 28% ya waliojiandikisha (2005) - 52% ya waliojiandikisha (2010)
Je hii tafakari inawakilisha nini?
 1. Kama wenye haki ya kupiga kura na hawakupiga wangetumia haki yao na wote kuwapa chama tawala kingekuwa kinajiamini zaidi na bila hofu yoyote ya nguvu ya umma.
 2. Kama wenye haki ya kupiga kura na hawakupiga wangetumia haki yao na wote kuwapa chama kimojawapo cha upinzani basi tungekuwa na serikali ya Chama tofauti na CCM.
 3. Kama wenye haki ya kupiga kura na hawakupiga kura wangetumia haki yao na wote kuamua kuharibu kura kwa kutoridhishwa na vyama vilivyoweka wagombea ingetupa picha kwamba chama/wagombea mbadala wanatakiwa.
 4. Na kama wote wangepiga kura kwa kila mtu kuchagua amtakaye kati ya waliogembea tungekuwa na picha halisi ya siasa za yanzania na hivyo kila mwanasiasa wakiwemo walio madarakani wangejipanga vizuri na pengine kuondoa uwezekano wa vurugu
Kuna uwezekano mkubwa Iko serikali tofauti na hii iliyo madarkani kama waliojima haki yao ya kupiga kura wangejitendea haki.
WADAU WOTE TOENI ELIMU YA UMUHIMU WA KUPIGA KURA, HAITOSHI KUWA NA WATU WENGI KWENYE MIKUTANO WASIOWEZA KUAMUA HATIMA YAO KWA KUPIGA KURA.

Pamoja na kupata takwimu toka kwenye attachment, nimekerwa na zilivyonyofolewa hapa, si sahihi. Takwimu ndizo msema kweli
 
Mkenazi

Senior Member
Apr 11, 2011
124
43
kwako mkenazi,
naomba kuuliza kulingana na uchambuzi wako murua, unafikiri kupungua kwa wapiga 2010 kulinganisha 2005 kulisababishwa na nini wakati
kitakwimu ilibidi waongezeke kwa sababu idadi ya watu inaongezeka haipungui ?

Malalamiko ya Dr.Slaa ya kuchakachuliwa matokeo ya urais yanaweza kuwa na nafasi gani ktk hizi namba hasa ukizingatia NEC ilikataa kata kata
kura za urais zisiasabiwe vituoni zilikopigwa ??

nashukuru sana kwa uchambuzi wako kwani umenifanya ni think kitu ambacho kinajenga kuelimika kwa maana ili uelimike you got to think.

Kuna mambo mwawili yanaweza kuwa yalitokea
1. Kwanza tuseme ni Kweli watu hawakupiga kura _ lakini inaacha maswali mengi yakitakwimu - Ndiyo maana nikaamua kuweka hapa hili wadau tusaidiane kupata majibu sahii.

2. Pili inawezekana malalamiko ya Dr. Slaa yakawa kweli; ilitakiwa/Inatakiwa kura za vituon nchi nzima zijumlishwe tuone kama zinatofautiana na za NEC. Utafiti ni muhimu hata kama hautabadilisha serikali iliyo madarakani ili kuweza kujipanga upya.

Ni muhimu kujua wapiga kura waliopiga kura ni hao tu?
Ni muhimu kujua kama ni kweli watu hawakupiga/hawapigi kura ni kwa sababu gani nini kifanyike ili watimize wajibu wao wa kidemokrasia.
Ni muhimu kujua kama si hao tu waliopiga idadi yao ambayo haijulikani ilikwenda wapi na kwa sababu gani?

Mchango wa wadau wote hasa wanaotumia gharama kubwa kuzunguka nchi hii kuleta mabadiliko wajue tatizo ni nini?
 
Mkenazi

Senior Member
Apr 11, 2011
124
43
Pamoja na kupata takwimu toka kwenye attachment, nimekerwa na zilivyonyofolewa hapa, si sahihi. Takwimu ndizo msema kweli

Jedwali lenye kuonyesha figure zote.
4. Upigaji kura 2005 na 2010
Upigaji Kura
2005
2010
Ongezeko/Pungua kati ya 2005/2010

Idadi
% Ya waliojiandikisha
Idadi
% Ya waliojiandikisha
Valid votes (Kura halali)
11,014,855
69%
8,376,022
46%
2,638,833 (24%)
Spoilt votes (Zilizoharibika)
495,290
3%
227,241
1%
-268,049 (54%)
Total voted (Jumla ya kura zilizopigwa)
11,510,145
72%
8,603,263
47%
-2,906,882 (-34%)
Did not vote – (Hawakupiga kura)
4,400,768
28%
9,411,404
52%
5,010,636 (53%)
Total registered Voters
15,910,913
100%
18,014,667
100%
2,103,754 (13%)
 
politiki

JF-Expert Member
Sep 2, 2010
2,376
1,504
Kulingana na takwimu hizi za NEC binafsi ningependa kusema ni hali ya kushangaza sana kuona idadi ya wapiga kura kuzidiwa kwa aslimia kubwa na wale wasiopiga yaani hii ni kinyume kabisa cha utamaduni wa Tanzania kwani chaguzi za nyuma za chama kimoja pamoja na kwamba ulikuwa hauna changamoto participation ilikuwa mpaka asimilia 80% ya waliojiandikisha lakini leo hii pamoja na vyama vingi na changamoto kuongezeka sasa idadi ya wapiga kura inapungua nina wasiwasi sana na hizi takwimu za NEC.

UKWELI TUTAUJUAJE.
Nina amini siku tutakayopata Tume huru ya uchaguzi ikafanikiwa kusimamia uchaguzi mmoja tu kutokea pale ndio tutajua hasa ukweli wa Takwimu hizi za sasa.

KINACHOSHANGAZA SANA.
Idadi ya wapiga kura wa ccm za urais inapopungua kwa kasi kubwa kutoka milioni 8 mwaka 2005 mpaka milioni 5 mwaka 2010 na pia idadi ya wapiga kura zilizopigwa imepungua kutoka milioni 11 mwaka 2005 mpaka milioni 8 tu mwaka 2010 pamoja na kwamba idadi ya wapiga kura imeongezeka kutoka milioni 15 mpaka milioni 18 nayo pia imepungua sana kinyume na miaka yote tangu tupate UHURU kwamba wapiga kura kupungua kwa kiasi kikubwa namna baada ya miaka mitano kupita. dunia nzima wapiga kura uongezeka kila baada ya miaka mitano kwenye uchaguzi mpya na wala haipungui. kwa mujibu wa takwimu haiwezekani watakaopiga kura mwaka 2015 wawe wachache kuliko waliopiga kura 2010 hiyo ni kinyume cha behaviour statistics za dunia nzima.

UKWELI NI HUU HAPA.
Endapo wapiga kura wale wale wa mwaka 2005 milioni 11 wangepiga kura mwaka 2010 inamaanisha JK angekuwa ameanguka kwa maana
ukiondoa kura alizopata milion 5 tu kura milion 6 zingekwenda upinzani na kwa Lipumba alikuwa very weak aslimia kubwa ya kura hizo zingekwenda kwa Slaa na kumuongusha JK. NEC ilibidi ipunguze idadi ya wapiga kura kwa makusudi kutoka milioni 18 mpaka milioni 8 tu ili waweze ku match
kura chache alizopata JK. kama wapiga kura wangekuwa angalau milioni 15 tu mwaka 2010 ambayo binafsi ninahisi ndio idadi kamili ya waliopiga kura basi NEC ingebidi itoe maelezo kwa wananchi (milioni 15 - milioni 8 =milioni 7) kura milioni 7 zimekwenda wapi ??
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom