Uchaguzi 2020 Wapiga kura wapya takribani Milioni sita na nusu (6.5M) kuamua mshindi wa Urais mwaka huu 2020

Trust None

JF-Expert Member
Feb 12, 2018
1,260
4,415
Wapiga kura kwa mwaka 2015 walikuwa 23,161,440 na mwaka 2020 ni 29,804,992 Hivyo mshindi wa uchaguzi mwaka huu ataamriwa na hawa wapiga kura wapya takribani milioni sita na nusu.

Ikumbukwe kuwa hawa ni vijana angalau waliomaliza darasa la saba na kuendelea ambao walikuwa UNDER 18 mwaka 2015 na wale wote walioona umuhimu wa kupata kadi ya mpiga kura baada ya kushindwa kupata kadi ya NIDA.

Hawa aidha watampigia Lissu au Magufuli. Tusubiri tarehe 28.

Idadi ya wapiga kura Tanzania waongezeka
 
Mwaka 2015 CCM waliishinda Chadema kwa kura 2.8M tu! inamaana hapo ngoma ni ngumu sana. Wale watumishi wa umma ambao miaka yote hupigia kijani na njano safari hii hata hawaeleweki wapo upande gani.

Kwa kauli ya mheshimiwa leo mkoa wa pwani naona hofu yao wajaogopa hawa wapiga kura vijana lakini wanasahau hilo kundi kubwa la watumishi wa umma.

Kazi ipo!
 
Mkuu unaamini wapiga kura ni 29m+? Hiyo idadi ni ya kupika ili kutengeneza ushindi fake kwa ccm. Tuhakikishe tu mawakala wanatunza rekodi vizuri kisha uone kwenye majumuisho.

Kuna idadi kubwa ya wapiga kura hewa na lengo ni kusaka % inayotafutwa na Magufuli ya 85%+. Tunza hii post uone uhuni utakaofanyika siku ya kura na wakati wa kuhesabu kura.
 
Mkuu unaamini wapiga kura ni 29m+? Hiyo idadi ni ya kupika ili kutengeneza ushindi fake kwa ccm. Tuhakikishe tu mawakala wanatunza rekodi vizuri kisha uone kwenye majumuisho. Kuna idadi kubwa ya wapiga kura hewa na lengo ni kusaka % inayotafutwa na Magufuli ya 85%+. Tunza hii post uone uhuni utakaofanyika siku ya kura na wakati wa kuhesabu kura.
Nakumbuka sana hili suala tumelijadili sana hapa JF.

Kuna mdogo wangu yupo NBS,nilimuomba takwimu za idadi ya makundi rika ya Watanzania.

Kitu nilichokiona hakiakisi uhalisia huu wa idadi ya waliojiandikisha kupiga kura.

Takwimu za wapigakura halisi waliojiandikisha haiwezi kuwa nusu ya idadi ya Watanzania wote.
Haiwezekani.
 
Mkuu unaamini wapiga kura ni 29m+? Hiyo idadi ni ya kupika ....Tuhakikishe tu mawakala wanatunza rekodi vizuri kisha uone kwenye majumuisho. Kuna idadi kubwa ya wapiga kura hewa na lengo ni kusaka % inayotafutwa na Magufuli ya 85%+. Tunza hii post uone uhuni utakaofanyika siku ya kura na wakati wa kuhesabu kura.
Mkuu inavyooneka hata kama ungepewa wewe mwenyewe usimamie uchaguzi huu nchi nzima bado husingeamini matokeo. Kwa hiyo, lazima mtafute sababu za kuficha aibu baada ya tarehe 28/10/2020. Na posti hii ya kwako ni moja ya mipango hiyo!
 
Mkuu inavyooneka hata kama ungepewa wewe mwenyewe usimamie uchaguzi huu nchi nzima bado husingeamini matokeo. Kwa hiyo, lazima mtafute sababu za kuficha aibu baada ya tarehe 28/10/2020. Na posti hii ya kwako ni moja ya mipango hiyo!
Usipoishi kwa kuhoji kila kitu utaishia kuimba maendeleo kujenga madaraja yasiyosaidia kuondoa mafuriko ya maji.
 
Usipoishi kwa kuhoji kila kitu utaishia kuimba maendeleo kujenga madaraja yasiyosaidia kuondoa mafuriko ya maji
Mkuu, kiukweli kabisa baadhi yetu humu ama kwingine, wanatumia vibaya "nafasi ya kuhoji kila kitu"!
 
Mkuu inavyooneka hata kama ungepewa wewe mwenyewe usimamie uchaguzi huu nchi nzima bado husingeamini matokeo. Kwa hiyo, lazima mtafute sababu za kuficha aibu baada ya tarehe 28/10/2020. Na posti hii ya kwako ni moja ya mipango hiyo!
Mkuu sina chembe ya shaka na nisemacho. Kwanza sina tatizo la kushindwa kihalali maana kwenye ushindani kuna kushinda na kushindwa. Usitake kunibadilishia maelezo yangu na kuwa ni lazima upande wangu ushinde.

Maelezo yangu yako wazi kabisa, na mashaka yangu yana mantiki kuhusu hiyo idadi ya wapiga kura. Hakuna uwezekano wa watu wenye miaka 18+ popote pale duniani, idadi yao kuwa sawa kabisa na walio chini ya umri huo. Fahamu kwamba kwa sasa watanzania tupo 59m+.
 
Wapiga kura kwa mwaka 2015 walikuwa 23,161,440 na mwaka 2020 ni 29,804,992 Hivyo mshindi wa uchaguzi mwaka huu ataamriwa na hawa wapiga kura wapya takribani milioni sita na nusu..
Ndugu yangu ngoja pia nikukumbushe kitu. CCM wamebiresha orodha ya wanachama wao waminifu kwa mfumo mpya wa kidigitali. 2015 walikuwa na wanachama milioni8. 2020 CCM inawanachama waminifu zaidi ya milioni 14.

Kwahesabu rahisi ni kwamba katika wapiga kura ambao ni zaidi ya milioni 29 wanaccm tayali wanawapiga kura milioni 14. Sasa unaweza kuona ushindi wa kimbunga utakavyopatikana kwa JPM.

Ndiomana leo kama uliona mheshimiwa Jakaya mwenyekiti mstahafu alimhakikishia ushindi mkubwa JPM. Unaweza kubishana na data kama na wewe utaleta data zako full stop.
 
Hahaha ushindi ni ushindi hata tukiwazidi ccm kura moja ndio tumeshinda sisi.

Kwa sasa tuna uhakika kuwashinda kwa kura milioni 6.8, ni ushindi mnono kwa Lisu na chadema, halafu tukiisha kaa ikulu tunapanga mkakati wa kurudia uchaguzi wa wabunge na madiwani, nchi nzima hakuna kupita bila kupingwa nchi huru kama hii.

CCM mtajinyea mwaka huu.
 
Ndugu yangu ngoja pia nikukumbushe kitu. CCM wamebiresha orodha ya wanachama wao waminifu kwa mfumo mpya wa kidigitali. 2015 walikuwa na wanachama milioni8. 2020 CCM inawanachama waminifu zaidi ya milioni 14. Kwahesabu rahisi ni kwamba katika wapiga kura ambao ni zaidi ya milioni 29 wanaccm tayali wanawapiga kura milioni 14. Sasa unaweza kuona ushindi wa kimbunga utakavyopatikana kwa JPM. Ndiomana leo kama uliona mheshimiwa Jakaya mwenyekiti mstahafu alimhakikishia ushindi mkubwa JPM. Unaweza kubishana na data kama na wewe utaleta data zako full stop.

Ccm inaweza kuwa imeuza kadi hata 20m acha hiyo milioni 14. Lakini ccm haina uwezekano wa kuwa na wanachama wanaokaribia 5m wenye mapenzi ya dhati. Watu wananunua kadi za ccm kwa ajili ya kupata upendeleo wa kimfumo kama mikopo, kufanya biashara nk, na kwa kuwa kadi hiyo inauzwa chini ya shilingi 1,000 hakuna anayeona tabu kuinunua.

Mfano mrahisi, kuna jamaa zangu wanaofisi kwenye majengo ya ccm, hivyo walishawishiwa kuwa na kadi ya ccm ili kuweza kupata mkopo. Na kweli wote watano wana kadi za Ccm, lakini hawana mahaba yoyote na ccm, na kura zao wote ni cdm. Mfano huo ni mmoja ya kadi nyingi za Ccm walizouziwa watu.

Wanachofanya ccm ni kutumia idadi ya kadi walizouzia watu, na sio wanachama wa kweli kutaka kuhalalisha ushindi wa hujuma. Na ifahamike nchi hii haijawahi kutokea kiongozi anayepika data kama Magufuli, hali hiyo tunaiona kwenye data za serikali, na alikuwa na tabia hii toka alipokuwa waziri.

Nakumbuka kuna wakati alikuwa anataja idadi ya samaki na mayai yake nchini wakati akiwa waziri wa mifugo. Tabia hiyo binafsi ya Magufuli ya kupika data, ndio kaingiza serikalini na ccm respectively. Sasa hivi jaribu kufuatilia miradi ya awamu ya tano, yote utasikia iko juu ya 80%. Mfano reli SGR toka mwaka jana tunaambiwa iko 85% kipande cha Dar-Moro na tuliambiwa novemba mwaka jana itakuwa imekamilika kipande cha Dar-Moro, fuatilia ulete mrejesho.
 
Mwaka 2015 CCM waliishinda Chadema kwa kura 2.8M tu! inamaana hapo ngoma ni ngumu sana. Wale watumishi wa umma ambao miaka yote hupigia kijani na njano safari hii hata hawaeleweki wapo upande gani...
Toa ushahidi kuwa ccm ilishinda kwa kura 2.8m
 
Mkuu unaamini wapiga kura ni 29m+? Hiyo idadi ni ya kupika ili kutengeneza ushindi fake kwa ccm. Tuhakikishe tu mawakala wanatunza rekodi vizuri kisha uone kwenye majumuisho. Kuna idadi kubwa ya wapiga kura hewa na lengo ni kusaka % inayotafutwa na Magufuli ya 85%+. Tunza hii post uone uhuni utakaofanyika siku ya kura na wakati wa kuhesabu kura.

Mkuu APO wata chomoa battery aisee..
 
Ccm inaweza kuwa imeuza kadi hata 20m acha hiyo milioni 14. Lakini ccm haina uwezekano wa kuwa na wanachama wanaokaribia 5m wenye mapenzi ya dhati. Watu wananunua kadi za ccm kwa ajili ya kupata upendeleo wa kimfumo kama mikopo, kufanya biashara nk, na kwa kuwa kadi hiyo inauzwa chini ya shilingi 1,000 hakuna anayeona tabu kuinunua...
Ndugu yangu wewe unamahaba kwahiyo huwezi kukubaliana na ukweli. Unaweza kusibitisha benki gani inatoa mikopo kwa kadi CCM? Pia je unataka kuwadanganya watu kuwa nchi hii huwezi kuwa mfanyabiasha au kuajiliwa mpaka uwe na kadi ya CCM.

Unahitaji uwe na akili za ajabu sana ili kushawishi watu wenye fikra zao kukubali utopolo wako. Sina haja ya kufanya utafiti wowote wakati wewe mqenyewe ni ushahidi huna kadi ya CCM na mambo yako yanaenda. Au naongea uongo? #JPM mi5 tena kazi iendelee.
 
Kura yangu nilishaifanyia maamuzi ata kabla ya kampeni, nitakuwa kichaa nikichagua tano tena.
 
Back
Top Bottom