Wapiga kura wamshangaa mgombea wao kuwakatisha tamaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wapiga kura wamshangaa mgombea wao kuwakatisha tamaa

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mubezi, Oct 4, 2010.

 1. Mubezi

  Mubezi Member

  #1
  Oct 4, 2010
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 68
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  MGOMBEA ubunge wa jimbo la Lindi mjini,kwa tiketi ya CCM, Bw, Mohamedi Abdullaziz amewakatisha tamaa wakazi wake, baada ya kuwaeleza bila ya aibu kuwa Serikali haina mpango wa kuboresha bandari yao kwa kile alichokieleza kukosekana kwa bidhaa za kusafirisha kutoka mkoani humo kwenda maeneo mengine.

  Abdullaziz ametoa kauli hiyo katika mikutano yake mbalimbali ya kampeni akiomba ridhaa achaguliwe tena kuongoza Jimbo hilo kwa mara ya nne mfululizo, katika viwanaj vya kata ya matopeni na Wailes mjini hapa.
  Mgombea akiomba tena ridhaa hiyo, Amesema Serikali kwa sasa haina mpango wakujenga au kuboresha Bandari iliyopo katika mji wa Lindi, kutokana na kukosabidhaa za kutosha za kusafirisha pamoja na abiria.

  Abdullaziz ambaye anawania tena nafasi hiyo kwa mara ya nne mfululizo alisema Serikali ingeboresha bandari hiyo iwapo wananchi wangekuwa wanazalisha zaidi mazao mbalimbali, ambayo ingesaidia meli zinapofika katika mji huo kupeleka mizigo na kurejea tena na mizigo ikiwa ni kwa ajili ya kupunguza gharama za meli kurudi bila ya kubeba bidhaa.

  “Jamani tusidanganyane na mtu yeyote, Serikali haina mpango wa kujenga bandari kutokana kutokuwepo kwa mizigo na abiria wa kusafirisha kwa meli kutoka Lindi kwenda Dar es salaam,,,,,,, Hivi ni nani atapanda meli masaa 24 na kuacha basilinalo safiri kwa masaa sita hadi manane?”.

  Kama malori ya tani kumi yanaleta mzigo na kurudi bila kubeba mizigo mingine,je meli ikija bandari ya Lindi itabeba kitu gani?” Amehoji mgombea huyo

  Kwa upande wa viwanda Bw, Abdullaziz ambaye pia ni mkuu wa mkoa wa Iringa alisema kutokana na Serikali kujiondoa katika Shughuli za kibiashara, haina mkakati wowote wa kujenga viwanda kutokana na kile alichokieleza kukosekana kwa mali ghafi za kutosha kwa ajili ya uendeshaji wake.

  Mgombea ubunge huyo ameitaja mali ghafi hizo kuwa ni pamoja na kutokuwa na umeme wa uhakika, miundombinu ya barabara, maji,mawasiliano ya ambavyo kwa jimbo la Lindi na Tanzania kwa ujumla ni tatizo kubwa.

  Abdullazizi amesema wajibu wa kujenga viwanda uko mikononi mwa wawekezaji ambao uchagua maeneo au mikoa ya kuwekeza katika viwanda wakizingatia upatikanaji wa huduma muhimu za kijamii.

  Mgombea huyo amewaomba wananchi wa jimbo hilo la Lindi mjini kumchagua yeye kuwambuge kwa mara ya nne mfululizo, Jakaya mrisho Kikwete kuwa rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania pamoja na madiwani wote kupitia Chama cha mapinduzi (CCM).

  Wakizungumza na gazeti hili baada ya mkutano huo, baadhi ya watu waliojitokezakumsikiliza wameondoka katika mkutano huo,huku wakisikitishwa na kauli ya mgombea huyo amekiuka ahadi zake alizokuwa akizitoa wakati wa kampeni zake za kuomba ridhaa achaguliwe katika mikutano yake, ikiwemo ile ya mwaka 2000
  na 2005 alipokuwa akisema akichaguliwa atahakikisha bandari inajengwa ili watu waendelee kupata ajira.

  “Huyu mtu anakanusha hata ahadi zake, kwani uchaguzi wa mwaka 2000 na 2005 wakati akiomba tumchague alituambia moja ya kero atakalolishighulikia ni pamojana uboreshaji wa bandari, Leo ametugeuka?” Wamesema Martin Michael na Issa Selemani.
   
 2. Mubezi

  Mubezi Member

  #2
  Oct 4, 2010
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 68
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Hii ni nzuri mana kawa mkweli
   
 3. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #3
  Oct 4, 2010
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  anatakiwa kuchagua kazi moja ama mkuu wa mkoa au mbunge, kung"ang"ania yaote mawili ndio kunafanya ashindwe kubuni mikakati ya kuboresha uchumi wa jimbo lake.
   
 4. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #4
  Oct 4, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Huko Lindi naona ndo wangekuwa wa kwanza kuipiga chini CCM ila nashangaa mtu kwa mara ya nne bado Mbunge hali yake inabdalika ninyi mnabaki hohehahe
   
 5. Mlachake

  Mlachake JF-Expert Member

  #5
  Oct 4, 2010
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 2,923
  Likes Received: 630
  Trophy Points: 280
  Kama kuna uchawi basi kuna watu wamerogwa na CCM.
   
 6. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #6
  Oct 4, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Kawa mkweli sasa ni zamu ya wananchi kutoa hukumu ila kwa mawazo yangu naona anafaa sababu nimkweli saana but atafute njia za kuendeleza uzalishaji jimboni kwake
   
 7. QUALITY

  QUALITY JF-Expert Member

  #7
  Oct 4, 2010
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Afadhali ya huyo amesema ukweli badala ya kuwadanganya kuwa bandali itapanuliwa kumbe wapi!! Ili waamue kama watampa au la. Very good. Wagombea wengine wa CCM kama wapo wajifunze kwa huyu.
   
 8. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #8
  Oct 4, 2010
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,504
  Likes Received: 2,744
  Trophy Points: 280
  Hivi JK hajapita huku??? Kama bado basi wasubiri ahadi!! Ila kama wako serious Dr. Slaa ni mkombozi.
   
 9. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #9
  Oct 4, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Hii nayo ni moja ya failure ya katiba yetu. Mtu akipewa u-RC anakuwa mwa siasa na kusahau jimbo lake. Conflict of interest inatokea na kuwa tatizo.

  Jamani chagua D. Slaa for real change in our system. Kumbukeni kwa kuwa Slaa na CHADEMA wanaahidi kubadili katika, wakishindwa tuta-vote kuwatoa. Shida na kumtoa hili monstaer!!!!

  Mungu bariki watTZ wachague viongozi shahihi end of OCT 2010. Amen.
   
 10. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #10
  Oct 4, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Tena basi awe competent kwa post zote izo,yale yale ya akina mama Mbega
   
 11. Joseph

  Joseph JF-Expert Member

  #11
  Oct 4, 2010
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 3,527
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Nimeipenda sana hii habari maana inaonesha ni jinsi gani mgombea huyu alivyo mkweli si kama wengine wanafiki ambao wanatoa ahadi ambazo hazitekelezeki.
   
 12. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #12
  Oct 4, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,345
  Likes Received: 418,852
  Trophy Points: 280
  Abdul Aziz mwongo sana. Bandari hiyo ingetoa mwanya wa bidhaa nyingi za Msumbiji, Mbeya Mtwara, Malawi na Zambia kupitia huko sasa hivi hazipiti huko kwa sababu bandari hiyo haina uwezo.

  Huyo La Azizi wapigakura wanapaswa kumtema ni mzigo usiobebeka
   
 13. DICTATOR

  DICTATOR JF-Expert Member

  #13
  Oct 4, 2010
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 392
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  wampige chini, keshachoka mbaya hana jipya wala uchungu. Kwanza mtu anakaa Iringa anaomba kura Lindi its crazy! juzi katukana albino harafu wanamchekea tu. Kama ccm wanatumia dawa basi dawa yao itakuwa ile ya msata.
   
 14. C

  Chief JF-Expert Member

  #14
  Oct 4, 2010
  Joined: Jun 5, 2006
  Messages: 1,490
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Nami namuunga mkono kwa kuwa mkweli kwa hilo. It make sense.
   
 15. b

  bagamoyo JF-Expert Member

  #15
  Oct 4, 2010
  Joined: Jan 14, 2010
  Messages: 4,531
  Likes Received: 2,113
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Mkoa wa Lindi (rangi nyekundu kwenye ramani) una potential (lulu) ya kuwa bandari ya kuhudumia mikoa ya jirani kama Ruvuma, Morogoro, Mbeya pia nchi za Congo DRC, Malawi, Zambia kama serikali ya CCM ingekuwa na mkakati wa kweli.

  Pia pichani inaonekana mkoa wa Lindi ni mkubwa kieneo, hivyo serikali za awamu zote za CCM zilitakiwa kuwa na mikakati ya kujenga barabara, viwanda vya kusindika mazao ya kilimo na bahari, kilimo bora, uvuvi wa kisasa, migodi ya chuma Liganga na makaa ya mawe toka Mbeya bila yakusahau bandari ya kuhudumia shughuli hizo za kiuchumi ndani ya Mkoa wa Lindi na mikoa jirani na nchi jirani pia.

  Usafiri wa majini ukifanyiwa uwekezaji mzuri ni wa gharama nafuu na wenye uwezo wa kuhudumia abiria na mizigo mizito ya tani nyingi. Pia itaifanya Bandari za Dar-es-Salaam kutoelemewa na mizigo kupita kiasi na kusababisha tija kupungua ktk Bandari ya Dar-es-Salaam.

  Kwa ufupi, Mgombea Ubunge kushindwa kuona 'potential' ya Mkoa wa Lindi ni sababu tosha asichaguliwe kuwa mwakilishi wa wananchi wa Lindi. Uamuzi wanao wenyewe wana-jimbo la Lindi mjini kuchagua chama mbadala au kuendelea na CCM ambayo imeshakata tamaa ya kuweza kuwa 'chachu' ya maendeleo kwa wana Lindi.
   
Loading...