Wapiga kura wa jimbo la Kongwa tumwache ndugu Job Ndugai akalime 2015 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wapiga kura wa jimbo la Kongwa tumwache ndugu Job Ndugai akalime 2015

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ebaeban, Jul 17, 2012.

 1. e

  ebaeban JF-Expert Member

  #1
  Jul 17, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 1,834
  Likes Received: 600
  Trophy Points: 280
  Mhe. Job Ndugai mbunge wa Kongwa amelewa madaraka, amechanganyikiwa , unaibu spika umempagaisha sasa hajui hata wajibu wake ni nini katika jimbo la Kongwa , wanawake toka kaskazini wamemchanganya, mke wake wa kwanza ni mchaga kamtelekeza Tabata, mke wa pili ni mpare huyu ndio kamchanganya kabisa kiasi kapeteza sifa ya kuwa mbunge wa Kongwa, amewacha kuwajibika kwa wapiga kura wake sasa anawajibisa zaidi kwenye kiti cha uspika. Mhe. Job Ndugai hatufai tena.

  Sisi wazee wa Kongwa :-

  1. Mzee Julius Roshee Mshama wa kijiji cha Mtanana
  2. Mzee Freedom Balisidya wa kijiji cha Majereko
  3. Mzee Yona Chilangwa wa Kongwa Mjini
  4. Mzee Jackson Jimmy wa kijiji cha Sagala
  5. Mzee Hassan Mchwembo wa kijij cha Mtanana
  6. Mzee Hussein Suleiman Madeni wa Kijiji cha Mtanana
  7. na Mzee Juma Hassan Yabwibwiki wa kijiji cha Ng`ambi.

  Tumekaa leo kwa kauri moja kumpendekeza Dr. Gidion John Kasilagila BSC University of.Dar,es salaam , Msc University of Zimbwabwe, P.hD ,UK wa kijiji cha Mtanana aje awe Mbunge wetu kuanzia kipindi cha uchaguzi cha 2015 kwa ticketi ya CHADEMA.

  Tumeona anafaa kabisa kuwa mbunge wetu kwa sababu zifuatazo:-

  1. Ni msomi ambaye ataendana na karne ya sasa ya sayansi na teknologia
  2. Ni mwana kijiji cha Mtanana na ameolea Mtanana
  3. Ni mbunifu ameshiriki kikamirifu katika kuibua mradi wa kupanda mti kijiji cha
  Mtanana awali ilikuwa jangwa ukiwa Mtanana ulikuwa inaweza kuiona hadi kijiji cha Ngomae na Kibaibwa hadi Ndulugumi mpaka NARCO sasa kuna miti kote

  1. Kenda Uingereza kanunua matrekta kaleta Mtanana angekuwa ndugu yetu Ndugai
  Angeyapeleka Moshi ukweni lakini kijana wetu kayaleta Mtanana yanalima Mtanana

  1. Akipata ubunge ataishi Mtanana , akimaliza vikao vya bunge anarudi Mtanana
  Kutusimlia yaliyojili, Yeye Ndugu yetu Ndugai anajali kiti cha unaibu spika na wanawake wake wa kaskazini.
  Ndugu Dr. Gidion John Kasilagila BSc, Msc, P.hD ni mtafiti katika kituo cha Ndorobo hapo Kange area Mjini Tanga akishugurika na uteketezaji wa Ndorobo kwa njia za kibaologia ( tse tsefly eradication using atomic energy).

  Tunawaombeni tumpe ushirikiane kijana wetu , msomi wa kwetu, kikao kingine cha matayarisha kitafanyika tarehe 1 October Mtanana kwa Mchembo karibuni

  Job Ndugai Masonenyi (hongera kwa kazi nzuri) tafuta mashamba sasa ukalime na hao wake zako.
   
 2. KOKUTONA

  KOKUTONA JF-Expert Member

  #2
  Jul 17, 2012
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 8,344
  Likes Received: 391
  Trophy Points: 180
  Hongereni sana kwa maamuzi yenu wazee.

  But kumbukeni human beings are unpredictable, hasa tunapopata madaraka.

  So be careful hata kwa huyo mliemteua.
   
 3. C

  CAY JF-Expert Member

  #3
  Jul 17, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 501
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Bravoooo!Tunataka mabadiliko sasa!
   
 4. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #4
  Jul 17, 2012
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Yote kwa yote Ndugai hakuchaguliwa kuwa mbunge bali aliteuliwa na kuwaondoa wengine kwenye kinyang'anyiro kwa pesa ya mafisadi ya Loliondo.

  Orodha hii kama ni kweli basi kumekucha kwani wengi wa hawa ni makada wa CCM

  Masalia ya uccm (ufisadi) ndani ya wananchi na baadhi ya viongozi wala makombo ya ccm ndilo tatizo. Naomba vita ianzie kwenye kujinasua na hao wapo mtanana, ndurugumi wanatumika na wenye fedha wa kibaigwa.

  Nilijualo vijana wengi wana mwamko ila hawako kwenye uongozi kwa sasa na wanagandanizwa. Pamoja na azimio hilo kwanza kazi ifanyike kukataa upuuzi wa viongozi wa ngazi zote wanahongwa bia kilo ya sukari na Ndugai. Ni pm nitakupa majina
   
 5. M

  Magesi JF-Expert Member

  #5
  Jul 17, 2012
  Joined: Jul 10, 2012
  Messages: 2,590
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mpeni ushirikiano katika kusimika viongozi kuanzia kwenye mashina kwan wakati ni sasa nakama sio sasa ni sasa hivi M4C 2NASONGA MBELE
   
 6. S

  STRONG GIRL Member

  #6
  Jul 17, 2012
  Joined: Jan 7, 2012
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Mpo sawa lakini napinga wazo lenu la kuwa huyo mgombea wenu mnayetaka achukue ubunge 2015 kupitia CHADEMA eti kaoa kogwa, hayo ni mawazo finyu tena yasiyofaa kuchukuliwa kama kigezo cha kuchagua kiongozi msafi na bora.

  Huu ni ubaguzi unaopaswa kupigwa kwa nguvu zote, mwanamke mstarabu na makini na mwenye upendo ni tabia ya mtu na si suala la kabila, kama ndugai hayuko sahihi muondoeni KUTOKANA NA UTENDAJI WAKE DHAIFU lakini mkitumia kigezo cha kuoa kaskazini mtaambulia ziro mana hata watanzania wenzenu tutawaona hamna maana, tutawaona kama KITUKO, kama watu toka kaskazini sio makini mbona mnaipenda CHADEMA?

  Kwani CHADEMA ilianzia wapi kama si KASKAZINI, tena hao walioianzisha ni vijana waliolelewa na wanawake wa KASKAZINI hivyo wanawake wa KASKAZINI ni MAKINI KULIKO WA KOGWA?

  MPINGENI JOB KWA HOJA SIO KURETA UPUUZI WA KUOA KASKAZINI, MBONA MAFISADI KIBAO WA CCM WAMEOA MAKABILA YAO NA BADO WOTE NI MAFISADI WAMETELEKEZA WANANCHI,
   
 7. Wile GAMBA

  Wile GAMBA JF-Expert Member

  #7
  Jul 17, 2012
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 1,809
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  mwanzo mzuri, lakini msiegemee kwenye ukabila
   
 8. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #8
  Jul 17, 2012
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Pole sana mama kwa kuguswa na hili. Hoja ni kwamba Ndugai is hopeless achaguliwe mwingine. Huyo anaependekezwa hajasema anaafiki. NA MIMI NASISITIZA NDUGAI HAKUCHAGULIWA NA WANANCHI; kinachotokea ni matokeo ya kutochaguliwa. Kama amebanwa na mkewe toka kaskazini mbona hata Mkapa ni hivyo? Lakini focus kwenye issue Ndugai hafai na hajachaguliwa na wananchi kwenye sanduku la kura.
   
 9. mwagavumbi 11

  mwagavumbi 11 JF-Expert Member

  #9
  Jul 17, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,255
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kuweni makini kwa uamuzi huo. kwani Ndugai amewakosea nin na ameonywa mara ngapi?
   
 10. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #10
  Jul 17, 2012
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Ndugai hajakidhi kigezo cha kuwa mbunge ndilo kosa lake, au wewe amekufanyia nini kama mbunge katika eneo kako?
   
 11. S

  STRONG GIRL Member

  #11
  Jul 17, 2012
  Joined: Jan 7, 2012
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  mimibaba unaujua hoja ya mleta hoja ni nzuri but alichokosea ni kuingiza masuala ya mgombea wa CHADEMA kuoa kogwa kama moja ya kigezo wanachoona kinafaa wananchi wamchague huyo waliyempendekeza hii ni hatari kesho tutaambiwa UCHAGUE MBUNGE WA KABILA LAKO, haya ndiyo Mwal NYRERERE aliyakataa, "Usimchague mtu kwa sababu ya kabila lake"

  Watanzania wengi ambao ndio wapiga kura wapo vijijini, wakiwemo wakazi wa kogwa, hawana hata huduma ya mitandao, hawapati hata kuyaona magazeti,RADIO, TV ndio usiseme! unaambiwa ni asilimia 12 ya watanzia wanapata huduma ya umeme,hivyo hata vituko na upuuzi wa wabunge hawauoni, sisi ambao angalau tunajua dunia inaendaje tunapaswa kuwa sauti zao, leo tukiwambia wanakogwa wamuondoe job kwa kuwa kaoa kaskazini tutakuwa tunawapotosha
   
 12. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #12
  Jul 17, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,797
  Likes Received: 36,826
  Trophy Points: 280
  Kwenye ratiba ya operesheni sangara tunaongeza na jimbo la kongwa.

  Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
   
 13. Ukwaju

  Ukwaju JF Bronze Member

  #13
  Jul 17, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 8,287
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Ndugu yangu ww umetumwa kwani kampeni bado, na hao wazee hawajakutuma kwani hiyo sio barua ni mawazo yako.
  Hivi Mbunge akichaguliwa kuwa Spika au Naibu unataka asilihudumie Bunge awe anashinda na nyie hapo barabarani Mtanana mnahesabu magari? funguka ndugu yangu mna Wabunge watatu bado hamjaliona hilo? Unataka nini kwani huyo Prof. umeambiwa ndio atakuwa Naibu Spika au Waziri, tafadhali mlichonacho kishikilieni, msiwe na mawazo ya Ugogo na Ukonongo eti kaoa kaskazini, Malecela Simbachawene hawajaoa Kaskazini
  Mwacheni Ndugai, hawezi kuondolewa kupitia mitandao, ANAKUBALIKA
   
 14. chuki

  chuki JF-Expert Member

  #14
  Jul 17, 2012
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,691
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Hao wazee watakuwa wana cdm tu,wametumwa na Ma-freemason.
   
 15. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #15
  Jul 17, 2012
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Anakubalika na nani wakati hakupigiwa kura? Wewe ndiye ulitumwa na Ndugai. Angepata ubunge kupitia sanduku la kura ndiyo tungesema anakubalika. Tunachokizungumzia hapa si ugogo wa kuwa naibu spika, mwenyekiti wa bunge au waziri; kinazungumzia matarajio ya mchango wa mwakilishi. Lete taarifa za alichokifanya Ndugai jimboni na hata bungeni kama siyo kutia aibu za mnyauzo.
   
 16. e

  ebaeban JF-Expert Member

  #16
  Jul 17, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 1,834
  Likes Received: 600
  Trophy Points: 280
  I appriceate so much your corcern STRONG GIRL, kuhusu Mwl Nyerere alikataza mambo ya ukabila, ninakuuliza na uwe mkweli ni mambo mangapi Mwl Nyerere aliyakataza na sasa hivi CCM yake inayatekeleza kama haina akili nzuri, nitakutajia machache ;-

  1. Kama ulichakuwa na akili kuna watu waliokuwa wanachukua form kugombea ubunge kwa ticket ya CCM enzi za mwalimu majina yao yalikuwa hayarudi kwa mantiki kwamba hawana sifa za uongozi mfano Aden Rage, Abood, Mohamed Dewji baada ya mwalimu kutangulia mbele ya haki wote hao wamejitoma ndani kwa tucket hiyohiyo ya CCM

  2. . Edward Lowassa ndo kabisa alifeli interview ya urais mbele ya mwalimu lakini sasa anapiga jalamba usishangae mwaka 2015 anakuwa rais wa Tanzania
  3. Mwl Nyerere alipinga kabisa mambo ya rushwa kwenye uchaguzi lakini sasa rushwa ndani ya CCM ni mwimbo wa taifa.
  4. Nyerere aliulinda muungano kwa nguvu zake zote lakini sasa eti wakina Mohamed Raza , Ismail Jussa ndio watetezi wa muungano wetu.


  Hoja ya Mwl alikataza naona haina mashiko, kwani walioko mezani ni wa kwanza kuonyesha mfano mbaya wa kumpuuza mwl.

  Jamani nyie hamtaki sisi tuende na wakati kwa kupata mbunge wa kisasa? Mnataka tu tuendelee na mbwiga huyu?
   
Loading...