Kenya 2022 Wapiga kura hewa nusu milioni walipiga kura katika uchaguzi wa Kenya-Mlalamishi Okiya Omtatah adai

Kenya 2022 General Election

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,499
9,279
Seneta mteule wa Busia Okiya Omtatah Jumatano alidai kuwa kuna zaidi ya kura 500,000 ambazo hazijaelezewa katika takwimu zilizotangazwa na Tume ya uchaguzi baada ya Uchaguzi Mkuu wa Agosti 9.

Akizungumza katika Mahakama ya Juu, Bw Omtatah alisema “wapiga kura hewa” 508,687 walishiriki uchaguzi wa urais. Kulingana na mwanaharakati huyo, idadi ya vifaa vya Kiems bado vilikuwa vikisambaza data siku moja baada ya upigaji kura kufungwa, akisema, hii inaweza kuwa njia ya kuongeza wapiga kura ambao hawapo.

Aidha alidai kuwa watu 1,665,412 walipiga kura kati ya saa kumi na moja asubuhi na na saa tatu kasorobo usiku wa Agosti 9. Mwanaharakati huyo alieleza kuwa ongezeko la kura haliwezekani kwani wapiga kura wengi walipiga kura kufikia saa kumi na moja jioni .

"Na, bila kufichua madai ya vituo vya kupigia kura vilivyohusika, data hii inaficha jumla ya idadi ya vituo vya kupigia kura ambavyo vilidaiwa bado vinawatambua wapiga kura kupitia vifaa vya Kiems baada ya muda wa mwisho wa upigaji kura," alisema. Bw Omtatah ameteta kuwa hakuna mgombeaji yeyote wa urais aliyefikia asilimia 50 pamoja na kura moja kwa ushindi wa moja kwa moja.

“Udanganyifu wa takwimu kama ilivyoonyeshwa katika Fomu 34C, ambapo jumla ya kura halali kama zilivyohusishwa na wagombeaji wanne hutofautiana kutoka kwa jumla ya kura zilizopigwa kama ilivyonaswa na IEBC inawezekana tu pale kura zinapohesabiwa kwa mikono tofauti na mfumo wa kiufundi ambao unapaswa kuhesabiwa kwa njia sahihi,” alisema.

Aliwasilisha jedwali mahakamani linaloonyesha kuwa, kura zilizokataliwa kama zilivyo katika Fomu 34C zinapotolewa kutoka kwa jumla ya wapiga kura waliojitokeza kupiga kura, matokeo ya kura halali ni 14,213,137.

"Hiyo ndiyo takwimu halisi iliyoandikishwa katika fomu ya 34C, lakini ambayo ni makosa kwa sababu kura zilizowekwa kwa kila mmoja wa wagombea wanne kwenye fomu 34C zinapojumlishwa zinatoa jumla ya 14,213,027," alisema na kuongeza kuwa katika mazingira hayo. hitimisho pekee ni kwamba takwimu zilibadilishwa .
 
Porojo tu hao Azimio hawajaleta ushahidi wowote.

Meneno matupu.
 
Sasa kwanini walikuwa wanajisifu sana na uchaguzi wao kumbe ni manyanga matupu!!?
 
Back
Top Bottom