wapiga debe wapandishwa mahakamani kwa kulazimihsa abiria kupanda magari wasiyataka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

wapiga debe wapandishwa mahakamani kwa kulazimihsa abiria kupanda magari wasiyataka

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Saint Ivuga, Oct 21, 2010.

 1. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #1
  Oct 21, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,471
  Likes Received: 19,861
  Trophy Points: 280
  Wasichana 11 wadaiwa kufanya ukahaba Dar Send to a friend Thursday, 21 October 2010 10:16 0diggsdigg

  Ndeninsia Lisley, (RCT)
  WASICHANA 11 wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Sokoine Drive jijini Dar es salaam kwa tuhuma za kufanya biashara ya kujiuza katika maeneo ya wazi.

  Mwendesha mashtaka wa mahakama hiyo, John Kijumbe alidai jana kuwa watuhumiwa walitenda kosa hilo, Oktoba 14, mwaka huu.

  Alidai wasichana hao, walikutwa barabara ya ufukweni saa 8:15 usiku wakiuza miili yao, jambo ambalo ni kosa kisheria.
  Kijumbe aliwataja watuhumiwa kuwa ni Lucy Edward (21), Abir Ameir (24), Fatuma Ghaza (20), wakazi wa Kinondoni wakati Janeth Joseph (30) na Amina Ramadhani (26), wakazi wa Magomeni.

  Aliwataja wengine kuwa ni Lina Frank (22), mkazi wa Tabata Bima, Subira Suleiman, (26) mkazi wa Mchikichini wilayani Ilala, Paulina John (27), mkazi wa Changombe, Mwanaidi Hussein (31), mkazi wa Mwananyamala, Fatuma Said (26), mkazi wa Mabibo na Amina Abdallah (35), mkazi wa Mbagala.

  Watuhumiwa hao, walikana shtaka hilo na walirejeshwa rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana ya kulipa Sh1 milioni kila mmoja. Kesi imeahirishwa hadi Oktoba 18, mwaka huu.

  Wakati huohuo, wapigadebe watatu wamepandishwa kizimbani kwa kosa la kuwalazimisha abiria kupanda magari wasiyoyataka.
  Mwendesha mashtaka huyo, alidai watuhumiwa walitenda kosa hilo, Oktoba 15 maeneo ya Mbagala Mission.

  Aliwataja wapigadebe hao kuwa ni Said Juma (24), Kibwana Abudi, (25), na Mudsa Abdullah (22).

  Hata hivyo, watuhumiwa walikana shtaka hilo na wamerejeshwa rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana ya kulipa Sh 5,000 kila mmoja.

  Mahakama imehairisha kesi hiyo mpaka Oktoba 21, mwaka huu itakapotajwa tena
  source:mwananchi:
  bongo tambarare?
   
 2. p

  pierre JF-Expert Member

  #2
  Oct 21, 2010
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 211
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Haya ni maisha bora kwa kila mtanzania usijali.
   
 3. Nyange

  Nyange JF-Expert Member

  #3
  Oct 21, 2010
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 2,180
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  Uchumi wa nchi ni mbovu wakati wasomi wa kugushi wanatoa takwimu za uchumi wa TZ kuwa umekua!!!! kama mwaka 2004 lita ya petrol ilikuwa Tsh. 360/ iweje baada ya miaka sita tu petrol iwe Tsh 1,700/?
  Badala ya kuboresha uchumi, wananunua magari mengi ya kusomba waharifu! (MUNGU WANGU) kweli hii nchi ndo inaimbia wimbo wa amani na utulivu?

  Hasira za watu tutaziona 31/10/2010 pale watakapo ukataa USANII wa Kiwete!!!
   
 4. tzjamani

  tzjamani JF-Expert Member

  #4
  Oct 21, 2010
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 997
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hali halisi ni maisha ni mbaya kuliko hata maelezo kwa wale wa vijijini kulinganisha mipaka kumi iliyopita na sasa utasikitika. Watu waishia kunywa gongo tu.
  Viongozi amkeni muwatumikie wananchi. Mungu atawabariki.
   
 5. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #5
  Oct 21, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Just out of curiosity, hivi kumtunza mahabusu mmoja kwa siku ni shillingi ngap????? Maana kama hii hadithi ni kweli basi twachekesha. Unamuweka mtu mahabusu kwa kukosa dhamana ya 5,000/=. Na wakipatikana na kosa adhabu yake ni faini kiasi gani au jela miaka mingapi??????

  Isije kuwa ni stratergy nyingine ya kupunguza wapiga kura!!!!!!! As these are potential voters
  .
   
 6. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #6
  Oct 22, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  mods thread zinafanana
   
Loading...