Wapi vinapatikana vifaa vya kupima UKIMWI?

Kashaija

JF-Expert Member
Aug 7, 2008
255
58
Nina mshikaji wangu ambaye aliondokewa na mke wake kiasi cha miaka minne iliyopita. Anatambua umuhimu wa kupima virusi ili kuishi kwa matumaini ila tatizo ni kwamba hataki kupima hospitali bali anataka kujipima mwenyewe.

Je kuna sehemu vinauzwa/vinapatikana vifaa hivi?
 
kwa sasa hivhi bado huwezi kuvipata kwa urahisi, kwa sababu haviuzwi kwenye maduka ya dawa.
Labda kama ana mtu anamfahamu ambaye yuko hospitali kitengo cha maabara amuombe ampe.
Na je amepata ushauri nasaha? maana majibu ya peke yake anaweza kufa kwa mshtuko akikuta anao,
Yuko dar?
 
Nina mshikaji wangu ambaye aliondokewa na mke wake kiasi cha miaka minne iliyopita. Anatambua umuhimu wa kupima virusi ili kuishi kwa matumaini ila tatizo ni kwamba hataki kupima hospitali bali anataka kujipima mwenyewe. Je kuna sehemu vinauzwa/vinapatikana vifaa hivi?

Njia ambayo ni sahihi ni kupata kwanza pretesting counseling na hata baada ya kupimwa, post counselling hii itakusaidia kuyapokea matokeo hata kama hayatakuwa mazuri. Nakushuri nenda kwenye VCT (voluntary couselling and testing) yeyote iliyo karibu, maana VCT ni entry point ya care and treatment ili kama maethirika ataingia kwenye mpango wa taifa wa dawa ART, hizi short cut si nzuri kabisa ndugu yangu, nenda waone Angaza ama AMREF wanaconsellors wazuri sana wala hutakiwi kuwa na hofu kuogopa matokeo, tumaini la kuishi bado lipo, acha njia za mkato si nzuri

Masa
 
mi naona labda aende Mabala aeleze ukweli halafu wamuelekeze anaweza kujipima mwenyewe.
 
mi naona labda aende Mabala aeleze ukweli halafu wamuelekeze anaweza kujipima mwenyewe.

Unethical approach....akiwa HIV + dawa atapata wapi, kujua umeathirika si suluhisho, ni hatua utakazochukua...nenda Hosp, ama kwenye Vituo vya Angaza ama AMREF anaficha nini? Ugonjwa? ama hataki matokeo yajulikane?
 
Njia ambayo ni sahihi ni kupata kwanza pretesting counseling na hata baada ya kupimwa, post counselling hii itakusaidia kuyapokea matokeo hata kama hayatakuwa mazuri. Nakushuri nenda kwenye VCT (voluntary couselling and testing) yeyote iliyo karibu, maana VCT ni entry point ya care and treatment ili kama maethirika ataingia kwenye mpango wa taifa wa dawa ART, hizi short cut si nzuri kabisa ndugu yangu, nenda waone Angaza ama AMREF wanaconsellors wazuri sana wala hutakiwi kuwa na hofu kuogopa matokeo, tumaini la kuishi bado lipo, acha njia za mkato si nzuri

Masa

Ushauri mzuri sana Masanilo, hofu aliyonayo huyu ndugu inaweza kuondoka kama atakutana na Counsellors wazuri. Hofu aliyonayo inatokana na kukosa ufahamu/taarifa sahihi kuhusu VVU/UKIMWI, akiwezeshwa kuelewa tatizo hofu itamuondoka na na ataweza kupima kwa wataalamu. Nasikitika kuwa hofu hii yote inatokana na unyanyapaa(stigma) mkubwa uliopo katika jamii yetu.Hali hii inmtisha muhusika. Tufahamu kuwa unyanyapaa ni mtazamo(attitude) hasi alionao mtu dhidi ya watu wenye hali/tatizo fulani. Pengine huyu bwana ameshashiriki katika kuwanyanyapaa watu wenye VVU/UKIMWI sasa leo ana hofu yakuwa naye yatamkuta!
 
Nina mshikaji wangu ambaye aliondokewa na mke wake kiasi cha miaka minne iliyopita. Anatambua umuhimu wa kupima virusi ili kuishi kwa matumaini ila tatizo ni kwamba hataki kupima hospitali bali anataka kujipima mwenyewe.

Je kuna sehemu vinauzwa/vinapatikana vifaa hivi?

inategemeana na unaishi wapi. ukienda CVS Pharmacy waweza kuvipata.

caution; kuna false positive na false negative results kwa 'rapid tests', kwa hiyo waweza kujikuta +ve kwenye kipimo kumbe in reality uko -ve and vice versa.

kwa hiyo ushauri wa masanilo bado una-hold inabidi kuwaona wataalam.
 
Wapi anaweza kupata?Ndio swali lake mambo ya aende akapime mwachieni yeye mwelezeni wapi atapata vifaa...
Mkuu mwenye shida...check na watu wa hospital kubwa kama agha khan...mtu wa lab anaweza kukuletea....hata kwa bei flan...hichi ndio nadhani unacho hitaji.Wengine hawataki kabisa kusika habari za ushauri nasaha...watu wanashauri sana kuhusu utakavyo ishi baada ya kuwa na ukimwi zaidi ya kama huna ukimwi ushi vipi.

Nenda kwenye counseling utakuwa katika 30mnts anaonge jinsi gani utaishi na ukimwi wakati hata hajakupa majibu..baada ya majibu kutoka unakuta uko -Negative.Hatumii hata dakika 10 kukushauri ufanyaje..utasikia hongera...what a hell.
 
Back
Top Bottom