wapi sehemu nzuri ya kufanyia service gari mpya? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

wapi sehemu nzuri ya kufanyia service gari mpya?

Discussion in 'Matangazo madogo' started by Original Pastor, Dec 3, 2009.

 1. Original Pastor

  Original Pastor JF-Expert Member

  #1
  Dec 3, 2009
  Joined: Nov 14, 2007
  Messages: 1,256
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Wadau wenzangu Poleni na majukumu mlionayo, Mimi nimeona nilete kwenu ndugu zangu muweze kunijulisha maana nimeamua hili liwehapa nipate msaada na ushauri mzuri . Nimejikwamua nimenunua Ka gari kangu ka Suzuki Escudo Nomade sasa nimekitoa jana Bandari nataka kufanyia services na sijui sehemu nzuri ya kufanyia hiyo services kwa gari mpya. Nikisema niende Kariakoo hapo ndo nimeliwa sasa naomba kama kuna Mdau wa JF ambaye anajua vyema sehemu hiyo na pia kuhusu AC inaonekana sasa sijui ni kuset ukiangalia naonekana inafanya kazi ila niliwauliza watu wa Japani walioniuzia wakasema ni Adjust sasa sijajua kwa hili gari jipya. Hili gari nimeagiza kutoka Japan. Nasubiri ushauri wenu nilipeleke . asanteni sana
   
 2. Serendipity

  Serendipity JF-Expert Member

  #2
  Dec 4, 2009
  Joined: Jan 24, 2009
  Messages: 475
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Kwa mujibu wa maelezo yako hiyo gari yako sio mpya, ni second hand!...
  Any way, sehemu zipo nyingi, nenda city garage pale opposit na DIT( Dar tech) au nenda Victoria
   
 3. Tripo9

  Tripo9 JF-Expert Member

  #3
  Dec 5, 2009
  Joined: Sep 9, 2009
  Messages: 2,168
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  Mambo saf mkuu.
  Sorry pastor natoka nje ya mada kidoogo.
  Kuliagiza na kulipia kila kinachohitajika mpaka ukalichukuaw gari lako ume2mia gharama kiasi gani? Km hutaki iwe public usisite kuni-pm.
  Natanguliza asante.
   
 4. Sugar wa Ukweli

  Sugar wa Ukweli JF-Expert Member

  #4
  Dec 5, 2009
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 373
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  City garage ni wazuri!!!
   
 5. DMussa

  DMussa JF-Expert Member

  #5
  Dec 15, 2009
  Joined: Sep 24, 2007
  Messages: 1,301
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Well kama unadeal na Suzuki basi sio mbaya ukajisogeza DT Dobie..... kwa mtu mwenye uelewa flani kwenye mambo ya magari mara nyingi hizi service za kilometer 3000 unaweza ukafanya manunuzi ya Oil+Filters then ukaenda gereji/petrol station zenye quick service wakakufanya hiyo kazi kwa gharama ndogo tu ya labour charge. Ila inapofikia suala la matengenezo(repair) hii ni vizuri ukapata gereji zenye mafundi wazoefu wa aina ya gari unayotumia. Maana kwa gari hizi za siku hizi mfumo wake mwingi ni electronic sasa ukipata fundi wa mwaka 47 atapiga nyundo za kutosha bila kutatua tatizo....

  ni hayo tu.... ila ujue gari lako sio jipya...gari mpya unachukua DT Dobie, Diamond Motors, Quality Motors au CMC! na zinakuja na warranty!
   
 6. SHUPAZA

  SHUPAZA JF-Expert Member

  #6
  Dec 15, 2009
  Joined: Aug 4, 2009
  Messages: 548
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Check na DT Dobie au authorized dealer wao ila ujiandae na invoice ya ukweli ukweli ndugu
   
 7. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #7
  Dec 15, 2009
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,767
  Likes Received: 216
  Trophy Points: 160
  Nenda pale Victoria petrol station wanafanya service vizuri sana, badilisha na tairi kabisa usije ukapata matatizo. Power window lazima wakulambe, cha msingi weka alarm inasaidia. pia jitahidi kupaki sehemu zenye usalama. kama ni gari yako ya kwanza Lazima Utaota imeibiwa Mkuu.

  Hongera kwa mafanikio.! - hayo ndo maisha bora kwa kila mtanzania.
   
Loading...