Wapi panasema Wabunge wa Chadema wamevunja katiba na kanuni za Bunge? Wapi?

Mwanamayu

JF-Expert Member
May 7, 2010
11,349
6,476
Wabunge wa CHADEMA

Mara baada ya Rais kuanza kuhutubia Bunge la 10 la Jamhuri ya Muungano tarehe 18/11/2010 wabunge wa Chadema ambao wanaunda kambi rasmi ya upinzani Bungeni walitoka nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma

Katiba inasema:
Ibara ya 26
(1) kila mtu anawajibu wa kufuata na kutii katiba hii na sheria za Jamhuri ya Muungano

Ibara ya 28
(4) uhaini kama unavyofafanuliwa na sheria utakuwa ni kosa la juu kabisa dhidi ya Jamhuri ya Muungano

Ibara ya 18
(a) kila mtu anao uhuru wa kuwa na maoni na kueleza fikra zake

Ibara ya 71
(1) Mbunge atakoma kuwa mbunge na ataacha kiti chake katika Bunge litokeapo kati ya mambo yafuatayo:
(c)ikiwa Mbunge atakosa kuhudhuria vikao vya mikutano ya Bunge mitatu mfululizo bila ya ruhusa ya Spika

Ibara ya 100
(1) kutakuwa na uhuru wa mawazo, majadiliano na utaratibu katika Bunge na uhuru huo hautavunjwa wala kuhojiwa na chombo chochote katika Jamhuri ya Muungano; au katika Mahakama au mahali penginepo nje ya Bunge
(2) Bila ya kuathiri katiba hii au masharti ya sheria nyingine yoyote inayohusika, Mbunge yeyote hatashtakiwa au kufunguliwa shauri la madai mahakamani kutokana na jambo lolote alilolisema au kulifanya ndani ya Bunge au alilolileta Bungeni kwa njia ya maombi, muswada, hoja au vinginevyo

[Maswali ya Msingi: Je, wabunge hawa wamevunja katiba kwa kutoka nje ya Bunge? Hapana kwa sababu ibara ya 100 (2) inawalinda vizuri tu na hakuna ibara yoyote iliyovunjwa kwani tukio hilo limetokea ndani ya ukumbi wa Bunge na haiwezekani kuwashtaki kokote kule zaidi ya kuamuliwa ndani ya Bunge. Je, wamevunja kanuni yeyote ya Bunge? HAPANA na hakuna kanuni yoyote inayoongelea suala hilo. Nini Spika atafanya? Spika atatumia kanuni ya 5(1) inayosema: katika kutekeleza majukumu yakeyaliyotajwa katika ibara ya 84 ya katiba, Spika ataongozwa na kanuni hizi na pale ambapo kanuni hazikutoa mwongozo, basi Spika atafanya kazi kwa kuzingatia katiba, sheria nyingine za nchi, kanuni nyingine zilizopo, maamuzi ya awali ya Maspika wa Bunge pamoja na mila na desturi za Mabunge mengine yenye utaratibu wa Kibunge unaofanana na utaratibu wa Bunge la Tanzania. Kanuni ya 5(4) inasema mbunge yeyote ambaye hataridhika na uamuzi wa Spika anawezakuwasilisha malalamiko hayo kwa Spika. Basi wabunge wa Chadema watapangua uamuzi wowote kandamizi wa Spika kwa kutumia kanuni hii. Kama kanuni mpya itatungwa basi lazima kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani ni mjumbe kama kanuni ya 3(1) ya Bunge inavyosema.

Je ni sahihi wabunge wengine hasa wa CCM kupeleka hoja Bungeni ya kuwaondoa wabunge wa Chadema? Kanuni ya 50(1) Mbunge anaweza kutoa hoja binafsi Bungeni kuhusu jambo lolote linalomhusu na lililoifikia jamii; je, wabunge wa Chadema watajinasua vipi na hoja hii? Kanuni ya 54(5) inasema taarifa yoyote ya hoja ambayo inakiuka masharti ya katiba au ya kanuni hizi haitakubaliwa; kanuni hii ndio itakayowanusuru wabunge wa Chadema kutolewa Bungeni kwani hoja ya Chiligati ni kinyume na ibara ya 71(1)(c); na baadhi ya kanuni za Bunge kama 14, 15, 16, 53(5)(c) kwani itakuwa vigumu kwa shughuli au vikao vya mikutano ya Bunge kufanyika bila kambi rasmi ya upinzani. Pia Mbunge upelekwe Bungeni na wananchi na sio Chama cha Siasa hasa chama tawala – CCM.

Wabunge wote ula kiapo cha utii – kuilinda na kuifuata katiba, basi kama wabunge wa Chadema wamevunja katiba kwa kutoka nje ya ukumbi wa Bunge wakati Rais alipoanza kuhutubia – kitu ambacho tumeona ni HAPANA – je, wale wabunge walioshiriki kurekebisha katiba na kufuta ibara ya 10, 80 na 82 hawakula kiapo wakati ibara hizo zikiwemo kwenye katiba? Je, jambo hilo ni kuvunja katiba? Je, Chadema kama timu ya mpira wa miguu wangewezaje kucheza mechi za ligi kuu bila wachezaji wao kusajiliwa? Mechi inapigwa baada ya usajili na ndicho walichokifanya Chadema pale Bungeni na kuandika historia nzuri ya kufuata misingi ya kidemokrasia kama misingi ya katiba yetu inavyosema, kwa kfupi wameonyesha kwa jinsi gani wanafuata misingi hiyo ya katiba yetu.
 
Hata hivyo hakuna kipengele chochote katika katiba kinachomlazimisha mtu yeyote kumsikiliza rais
 
Back
Top Bottom