Wapi Nitapata Matofali haya??

Doltyne

JF-Expert Member
Aug 29, 2011
440
170
Wadau nina shuda sana na Matofali ya namna hii, kwa mwenye ujuzi anijuze tafadhali. Haijalishi yapo mkoa gani, Cha muhimu ni upatikanaji na bei... 10.jpg

Shukran
 
mkuu nenda makambako kuna kijiji kina itwa kidegembasi utapata matofari hayo, nimazuri sana.
 
Peramiho unaweza kupata mazuri kuliko hayo,bei sifahamu kwa sasa ila once nikijua nitapost hapa
 
Hongera kwa kupata mwamko wa kutumia mali ghafi bora na rahisi inyopatikana sehemu nyingi. Matofali ya aina hii yanaweza kufyatuliwa kwa kutumia udongo wenye madini ya iron na clay (Ruvuma, Rukwa, Geita, Njombe etc), na mafundi wa kuyafyatua wanapatikana Songea, Sumbawanga, Mbozi, Tunduma na Makambako. Nenda pale maeneo ya nyuma ya mlimani city kama uko Dar ukajionee nyumba zilizojengwa kwa tofali hizi, au pitia Vawa Mbozi, Laela Sumbawanga kote utaona nyumba zimejengwa kwa tofali za rangi na aina hiyo. Anza kuchakarika ndugu, ushauri nimekupa.
 
Mkuu, kwa jinsi ninavyoziona hzo ni tofali za kawaida tu za kuchoma, zimefyatuliwa kwenye udongo wa kichuguu na mfyatuzi mzoefu! Ukitaka kupata Tofali za kuchoma za kisasa na zenye kiwango cha hali ya juu nendA PERAMIHO-SONGEA-RUVUMA; Ninayo namba ya Fr mmoja kule lakn kwa baht mbaya hayupo nchini, hata hvyo kama kweli unazihitaji, na unaweza kuzisafirisha kutoka huko (Ningekushauri uangalie ukaribu pia, nadhani zipo sehm nyingi), kama unainsist ni-PM ili nione jinsi gani naweza kukuunganisha nawahusika!
 
Shukran sana ndugu, nimehamasika sana na ujenzi huu. Kwa kweli unapendeza sana na hauhitaji plaster wala chipping nje ya nyumba.
 
Mkuu, kwa jinsi ninavyoziona hzo ni tofali za kawaida tu za kuchoma, zimefyatuliwa kwenye udongo wa kichuguu na mfyatuzi mzoefu! Ukitaka kupata Tofali za kuchoma za kisasa na zenye kiwango cha hali ya juu nendA PERAMIHO-SONGEA-RUVUMA; Ninayo namba ya Fr mmoja kule lakn kwa baht mbaya hayupo nchini, hata hvyo kama kweli unazihitaji, na unaweza kuzisafirisha kutoka huko (Ningekushauri uangalie ukaribu pia, nadhani zipo sehm nyingi), kama unainsist ni-PM ili nione jinsi gani naweza kukuunganisha nawahusika!

Asante sana mkuu, kwa kweli peramiho ni mbali kidogo. Mi nipo dar, nikipata fundi mzuri akanichomea tanuri site kwangu bagamoyo yaani sijui atakuwa kanisaidiaje kwakweli. Asante sana.
 
mkuu nimejenga nyumba 2 in Dar kwa kutumia hayo matofali.na sasa hivi niko ktk mchakato wa kuchoma tofali ,nimeshapanga tanuru la 10000 bricks.
kuna rafiki yangu ni mtaalam wa kuchoma ,anaweza kuja site yako aka kagua na kukuchomea au kukuletea site yako,wewe unalipa tofali liko site.ila kama unakichuguu karibu anaweza kuja kukuchomea site yako.tatizo ni miti-kuni na aina ya udongo.

pia unaweza kujenga bila simenti,unatumia chokaa na mfinyanzi, a good example ni majengo ya Samora Avenue in Dar,mengi yametumia chokaa na mawe ktk ujenzi wake.

mkuu bei sh ngapi? Maeneo ya kimara bonyokwa vp? Hata mimi nahitaji sana
 
Bei ni Tsh 80/- kwa tofali. matofali 6 ni sawa na 1 tofali la cement.

Aisee, asante sana kwa taarifa. Nikiwa tayari ntakupm tuangalie mchakato utaendaje. Kupatikana udongo sio issue kabisa, kwani kifusi kingi kipo maeneo ya mbali na wadau wanaweza kubeba kwa matipper mpaka site zao, nadhani hata mimi kupata mfinyanzi na udongo mzuri wa tofali haitosumbua.
 
Bei ni Tsh 80/- kwa tofali. matofali 6 ni sawa na 1 tofali la cement.

Asante Newmzalendo kwa info!
Bei hiyo ya 80 Tshs ni bei ya tofali anayokuuzia mchomaji (fundi) au ni bei unayompatia akuchomee gharama za zingine zinakuwa kwako, au? Sijaelewa.
Maana nahofia kama utamlipa kwa kila tofali kabla ya kuchoma inaweza kula kwako, au unamlipa mkishachgua matofali yaliyochomwa vizuri?
Mimi mwenyewe nayazimikia sana.

Huyo fundi anaweza kwenda Tabora manispaa kunitengenezea hizo tofali?

Asante!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom