Wapi ntapata chai?

TIMING

JF-Expert Member
Apr 12, 2008
24,889
11,285
Leo nina hamu, tena hamu ni ya chai,
chai isiyo sanda, tena iso na viungo
tena nijibanze kona, wakati najifyonzea
chai iwe ya kweli, niinywe kwa kuivuta

Nina hamu nina hamu, kuliko hata ya jana,
sijui kwanini hamu, ati ije ijumaa
wakati leo wikendi, utamu wake ni bar
chai iwe ya kweli, niinywe kwa kuivuta

wajameni, nina hamu, chai ntapata wapi
hata ya kuinyatia, basi japo kodokolea
nipakate na kikombe, sukari ntaitilia
chai iwe ya kweli, niinywe kwa kuivuta

kikombe nacho napenda, kiwe cha mahanjamu
kwani nikianza kunywa, nisiwe nafunga macho
sikitaki cha mabati, nataka dongo rutuba
chai iwe ya kweli, niinywe kwa kuivuta
 
Chai iliyo utamu, nenda Baa ya Sakina,
Hautaishiwa hamu, hakika weye kijana,
Naomba ulifahamu, hilo neno kwa upana,
......Chai isio viungo, Kimbia Sakina Bar!
 
mbona jua limeshakuwa kal utainywaje hyo chai ila hyo chai kaka duu!
 
Tamu ya chai sukari, sio ya kujitilia
Iliyoungwa jikoni, na kisha ikakolea
Hiyo ndo ya asili, mimi niliyozoea
Kama wataka kuvuta, utakunywa kwa mrija?
 
chai nyeusi mahala kote ipo, hata uswahilini inapatikana,
chai nyeupe ni gharama, mgahawani inapatikana,
chai ya kijani ya kichina, hoteli kubwa utaipata,
chai mbona ipo, kila mahali inapatikana,


chai zote tamu, kama utaweka sukari,
chai ni dawa ukinywa bila sukari,
chai ya viungo utaipenda, ukienda zanzibari,
chai nikupe nini usiishe kikombeni
 
Chai iliyo utamu, nenda Baa ya Sakina,
Hautaishiwa hamu, hakika weye kijana,
Naomba ulifahamu, hilo neno kwa upana,
......Chai isio viungo, Kimbia Sakina Bar!

pijei ndugu yangu, tena sikiza makini
sikati chai ya baa, isije leta balaa
nataka chai ya rangi, ile ya majimoto
chai ninayoitaka, ni chai hasa ya kupoza

halahala ndugu pije, umakini uwe mno
sitaki ile baa, nataka ile ya jiko
niipashe nipulize, nimimine nikoroge
kisha nigugumie, kwa utamu wa sukari
 
mbona jua limeshakuwa kal utainywaje hyo chai ila hyo chai kaka duu!
tulishaambia sana, any time is tea time
wakatunga na manyimbo, ili tulambe sote
chai mie nitakayo, yanywewa wakati wote
sasa wewe ni wa wapi, hata uazame jua?
 
Tamu ya chai sukari, sio ya kujitilia
Iliyoungwa jikoni, na kisha ikakolea
Hiyo ndo ya asili, mimi niliyozoea
Kama wataka kuvuta, utakunywa kwa mrija?
chain niitakayo, ni ile ya kukoroga
nichezeshe na kijiko, kila kuta za kombe
nionje-onje kimikogo, huku nikijiramba
jamani nataka chai, hamu yake mantashahu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom