Wapi nitapata vitabu/machapisho/hotuba za abeid karume (muasisi wa muungano)

joshua_ok

JF-Expert Member
Jun 27, 2012
12,999
2,000
Salam wadau
Mimi nimekuwa mfuatiliaji wa Muungano wa Tanzania na Zanzibar sasa nimefanikiwa kupata machapisho/vitabu na hotuba za Mwl. Nyerere na Prof. Shivji sasa nataka kupata pia machapisho ya Muasisi wa muungano upande wa Zanzibar (Abeid Karume) kwa ajili ya kujisomea na kuwa na historia iliyo sahihi. asanteni
 

Gagnija

JF-Expert Member
Apr 28, 2006
8,356
2,000
Salam wadau
Mimi nimekuwa mfuatiliaji wa Muungano wa Tanzania na Zanzibar sasa nimefanikiwa kupata machapisho/vitabu na hotuba za Mwl. Nyerere na Prof. Shivji sasa nataka kupata pia machapisho ya Muasisi wa muungano upande wa Zanzibar (Abeid Karume) kwa ajili ya kujisomea na kuwa na historia iliyo sahihi. asanteni
Hayo kaulize huko Zanzinet. Sisi hatuwezi kuwa na majibu.
By Jaji Werema
 

blessings

JF-Expert Member
Jul 9, 2012
6,460
2,000
mmh abeid karume awe na machapisho? aaanzie wapi kuandika mzee wetu yule jamani ? au hamjui background yake? alikuwa kuli bandarini kabla hajingia siasani sasa fikiria kuli aandike nini cha kueleweka? yaani in short kumfananisha Nyerer na Karume ni kama kufananisha kifo vs usingizi
 

Majita

JF-Expert Member
Jan 13, 2008
608
250
Salam wadau
Mimi nimekuwa mfuatiliaji wa Muungano wa Tanzania na Zanzibar sasa nimefanikiwa kupata machapisho/vitabu na hotuba za Mwl. Nyerere na Prof. Shivji sasa nataka kupata pia machapisho ya Muasisi wa muungano upande wa Zanzibar (Abeid Karume) kwa ajili ya kujisomea na kuwa na historia iliyo sahihi. asanteni

kafuatilie huko huko kwao Zanzibar
 

makubazi

JF-Expert Member
Feb 15, 2013
2,048
1,195
Ooyooo nilitaka kumjibu lakini tena basi na kesho nitakwenda unguja nikaulizie kwa sefu balozi na akinipa jibu basi nitarudi tena tanganyika
 

andreakalima

JF-Expert Member
Jun 2, 2012
4,064
2,000
Karume hakusoma jamani angeandika nini sasa? hiv mkisikia Lissu anahoji Muungano mnafikiri anatania? anajua Nyerere alimlazimisha tu bila kutafakari Karume akaingia kichwa kichwa
 

kibogo

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
9,727
2,000
Abdulrahman Babu: Tanuru la mapinduzi Zanzibar na Muungano lisilokumbukwa II

KATIKA sehemu ya kwanza ya makala haya, tuliona ni nani mwanaharakati huyu Babu, na jinsi alivyoanzisha harakati za ukombozi chini ya Chama cha kiharakati – Zanzibar Nationalist Party (ZNP) na kuwatia hofu wakoloni wa Kiingereza na kuanza kumfuatilia. Tuendelee na sehemu hii ya pili kuona ilivyokuwa
Waingereza waliingiwa hofu kwa kuona ZNP kimesheheni Wakomunisti wakipata misaada kwa siri kutoka Urusi na China. Mamwinyi wa Kiarabu kwa upande wao walikiona ZNP kama tishio kwa maslahi yao na katika kuhodhi uchumi wa nchi.

Kwa Waafrika na vibepari uchwara Visiwani, ZNP kilikuwa aina fulani ya mkakati wa Waarabu kuwaondoa Wazungu ili Waafrika watawaliwe na Waarabu.
Kwa mitizamo hii hasi na kinzani yenye hofu, Waingereza walihamasisha na kusaidia kuanzishwa kwa Chama kipya chenye utiifu kwao, kupingana na ZNP. Na kwa msaada wa Mwalimu Julius Nyerere, wakati huo Rais wa Chama cha Tanganyika African National Union (TANU), Vyama viwili vya Kijamii, African Association (AA) na Shirazi Association (SA) upande wa Unguja, viliungana, Februari 5, 1957, muda mfupi kabla ya uchaguzi wa vyama vingi; kuunda Muungano uliojulikana kama African – Shirazi Union (ASU) kwa lengo la kushirikiana katika uchaguzi, lakini AA na SA upande wa Pemba vilikataa kufanya hivyo.
Uchaguzi huo ulishuhudia kushindwa kwa ZNP ingawa ASU hakikushinda pia, baada ya kupata chini ya theluthi mbili ya kura Visiwani na viti vitatu tu kati ya sita vya Bunge (LEGCO). Miezi kadhaa baadaye SA upande wa Pemba kilikubali kushirikiana na ASU shingo upande kuwezesha kuundwa kwa Afro – Shirazi Party (ASP), na Sheikh Abeid Amani Karume akateuliwa Rais wa Chama hicho.
Kufikia mwaka 1958, ASP kilisheheni matabaka mbali mbali ya kiuchumi, wakiwamo Wakulima na Wafanyakazi, Mamwinyi, Wafanyabiashara na mabepari wawakilishi wa Chama cha Wahindi – “Indian National Association” wenye kauli turufu kwenye Chama chenye kupungukiwa Wasomi, kikilinganishwa na ZNP. Kwa upande huu, Chama hiki kiligeuka tegemezi kwa TANU kwa Wasomi na kwa ushauri.
Wakati ZNP cha Babu kikiendelea kuchanja mbuga kudai uhuru sawia, kauli mbiu katika kampeni za Karume ilikuwa kuzuia uhuru, maarufu kama “Uhuru Zuia”, ili Zanzibar iendelee kutawaliwa na wageni. Sababu kubwa ilikuwa kwamba, Zanzibar ilikuwa haijawa tayari kwa uhuru kwa ASP kukosa Wataalam wa kuongoza nchi.
Wakati huo huo, utii wa Karume kwa Sultani wa Zanzibar ulikuwa dhahiri. Wakati mmoja, Julai 1958, Karume alitoa tamko dhidi ya Sultani ambalo siku mbili baadaye aliomba msamaha kwa unyenyekevu mkuu akisema ilikuwa ni “kuteleza kwa ulimi”. Katika barua ya Julai 26, 1958 kwa Sultani kuomba msamaha, aliandika: “Mtukufu Sultani; mimi ni raia wako, na pamoja na wanachama wote wa ASP, napenda kukuhakikishia utiifu wangu kwako. Mimi binafsi, Abeid Amani Karume, napenda kuwasilisha kwako ukweli mtupu, Sultani wangu [kwamba] katika hotuba yangu eneo la Raha Leo, nilidhani nilitumia maneno ya kistaarabu, lakini sikujua maana ya maneno hayo. Kwa hiyo, ni dhamira yangu, na ni dhamira ya wenzangu pia kutoka ndani ya mioyo yetu, mpendwa Mfalme Maulana, kukuomba na kukuhakikishia kwamba, tuko chini ya miguu yako na chini ya himaya yako pia.
Sisi ni watiifu, bila kusita, kwa kila amri yako. Sote tunajua wema wako wa kweli na ukarimu wako. Nakuomba unisamehe makosa yangu kwa kutumia lugha ambayo sikuielewa, ewe Maulana. Niko chini ya miguu yako na nabakia mtiifu daima. Abeid Amani Karume” (Nyaraka, Makumbusho ya Taifa, Julai 1958).
Kuhakikisha kwamba ZNP kinavunjwa miguu, ASP, kwa kuungwa mkono na Marekani na Uingereza kwa hofu ya Ukomunisti, ilifungua kasha la chuki za kibaguzi kwa misingi ya rangi kwa kuwalenga Waarabu washabiki wa ZNP, kiliongoza mgomo mkubwa kugomea maduka ya Waarabu Vijijini wakafilisika na pia kuwatisha wamiliki wadogo wa ardhi na kuwaacha Mamwinyi waliokiunga mkono.
Ndani ya ZNP nako moto ulikuwa ukifukuta kwa mgongano mkubwa, kati ya makada wa mrengo wa sera za kulia (Wa-Liberali) waliotaka Chama kifuate na kuongozwa kwa sera za kibepari, na makada wa mrengo wa kushoto (Wakomunisti) waliotaka ZNP kiongozwe kwa sera za Kikomunisti bila ya ubaguzi wa rangi au asili ya mtu.
Mfarakano huu ulitarajiwa kutokana na mtizamo wa kitabaka ulioanza kujijenga ndani ya Chama. Wakati kundi la Wahafidhina wa sera za kiliberali, likiongozwa na Ali Muhsin walikuwa bado watiifu kwa Sultani, kundi la Wakomunisti, likiongozwa na Babu, lilitaka kuwaunganisha Wakulima, Wafanyakazi na “manamba” katika mashamba ya Mamwinyi chini ya ZNP kuwakilisha matakwa yao ili kwamba Chama kiweze kuwasemea wote nchini.
Katikati ya mkanganyiko huu na uhasama kutoka wafuasi wa sera za kihafidhina ndani ya ZNP wakishabihiana na Serikali ya Kikoloni, Wakomunisti wa ZNP walifikiria mikakati kadhaa ya kujiponya. Kwa mtizamo wao dhidi ya ukoloni, hawakuuchukulia ukinzani kati ya ZNP na ASP kama jambo muhimu sana, ikizingatiwa kwamba ASP na Karume walikuwa tayari wamefuta kauli mbiu ya “Uhuru Zuia” na kukubali kushiriki katika mapambano ya uhuru, baada ya kukemewa vikali na Mwalimu Nyerere kwenye Mkutano wa “Pan African Freedom Movement of East and Central Africa” [PAFMECA], uliofanyika mjini Mwanza, Septemba, 1958 ambapo Ali Muhsin (ZNP) na Karume (ASP) walihudhuria pia.
Aidha, Mwalimu Nyerere alikuwa amekihakikishia ASP kutohofu matokeo ya kushirikiana na Wazalendo wengine kupata uhuru mapema kwa sababu ilitambulika kwamba Wa-Afro-Shirazi walikuwa wamiliki halali wa Zanzibar kama raia wengine.
Pili, ASP haikuwa na sababu za kuhofu uhuru mapema kutokana na kukosa watu wenye elimu kwa sababu TANU kingehakikisha kwamba, Wazanzibari wenye elimu waliokuwa wameajiriwa Tanganyika wangepelekwa Zanzibar kusaidia uhuru ukipatikana.
Tatu, Mwalimu alitaka ASP kitambue kwamba, makundi mengine ya Kizanzibari (mbali na Wana-ASP) na Wazanzibari kwa ujumla, walikuwa na haki sawa za kisiasa.
Chini ya mtafaruku huu ndani ya ZNP, mtizamo huo uliwafanya baadhi ya makada wa ZNP wafikirie kujiunga na ASP, lakini wengi wao waliona wabakie ZNP kupambana ndani kwa ndani kukinusuru Chama hicho walichokisumbukia kwa jasho kukiweka kwenye reli ya kimapinduzi.
Miezi kadhaa kabla ya uchaguzi wa Julai 1963, ZNP kilishuhudia mpasuko mkubwa kuliko yote katika uhai wake. Mpambano ulikuwa kati ya Viongozi Wakuu wa Chama hicho, Ali Muhsin na Abdulrahman Babu, baada ya wawili hao kutofautiana juu ya mpango wa uchaguzi na juhudi za Chama kujenga jamii ya Kizanzibari isiyo na ubaguzi wa rangi.
Babu aliamini kwamba, mtindo wa kuteua wagombea kuwakilisha majimbo kitabaka kwa misingi ya rangi au asili ya mgombea, ulikuwa haufai na wa kibaguzi. Kwa maana hiyo, hakukubaliana, kwa mfano, na utaratibu wa kuweka mgombea wa Kiarabu kwa jimbo lenye Waarabu wengi; au Muasia kwa jimbo lenye Waasia wengi. Alitaka mfumo ambao ungewalazimisha washabiki wa Mwarabu, Muasia au Mngazija kuwapigia kura Viongozi wa Kiafrika wenye asili ya Shirazi kuthibitisha ZNP kilikuwa Chama kisichobagua.
Babu alisisitiza ZNP kutosahau asili yake kama Chama cha kiharakati cha Wakulima wa Kiafrika, kwamba kiteue angalau mmoja wa waasisi wake kwenye jimbo salama. Aliona kwa kufanya hayo, ZNP kingethibitika kuwa kweli cha kizalendo.
Muhsin kwa upande wake, alipinga mabadiliko hayo akisema haukuwa wakati mwafaka kwa Chama hicho kujipima “usafi” wake juu ya fursa sawa kwa watu wa rangi zote. Na kwa kuwa uchaguzi mwingine ulitarajiwa kufanyika Julai, 1963; Muhsin alihofia kwamba, kama hoja za Babu zingekubaliwa, uwezekano wa ZNP kushinda ulikuwa mdogo.
Kuhakikisha kwamba hoja za Babu zinabwagwa chini, alianza “kampeni” za chini kwa chini kuungwa mkono na Viongozi wa Matawi na Mikoa. Juni 1963, katika Mkutano Mkuu Maalum wa ZNP, hoja ya Babu iliwasilishwa na kukataliwa. Babu na kundi lake la Wakomunisti walijiengua sawia kutoka ZNP na kuunda Chama kipya – “Umma Party” (UP) siku hiyo hiyo.
Hatua ya Ali Muhsin kumpinga Babu ilitarajiwa, kwani taarifa za awali tangu Machi 1962 zilionesha kwamba, Waingereza waliwaambia Viongozi wa ZNP – ZPPP kwamba, Muungano wa Vyama vyao hautaruhusiwa kurithi madaraka Zanzibar kama hawakuwaondoa Wanaharakati wa sera za mrengo wa kushoto, ambapo Muhsin na Mohamed Shamte (ZPPP) walikubaliana kushirikiana na Wakoloni hao.
Umma Party kilianza kwa kishindo kama ilivyodhihirika kwenye Mkutano wa kwanza wa hadhara kesho yake, kwa maelfu ya watu kuhudhuria kwa kukanyagana. Vijana, hasa wale wa tabaka la Wafanyakazi na Wakulima wafuasi wa Vyama vyote vya siasa na makundi ya rangi zote, walizizima wakishangilia kwa matumaini. Katika kipindi chini ya wiki moja, Umma Party kilikuwa na wanachama kwa maelfu wa tabaka zote.
Lofchie, Michael; katika kitabu chake, Zanzibar: Background to Revolution, anamwelezea Babu na msisimko aliozua kwa jamii ya Kizanzibari kwa maneno yafuatayo: “Babu alitambulika kimataifa kwa kipaji cha kutawala na kudhibiti siasa za Zanzibar, na katika kipindi kifupi aliweza kukipandisha hadhi Chama cha Umma juu ya Vyama na vikundi vyote vya kiharakati Visiwani, akiwa na uhusiano imara wa kikazi na Vyama vikuu vyote vya Wafanyakazi, Vyombo vya Habari na hata Viongozi wakuu wa ASP wenye ushawishi mkubwa”.
Ndiyo maana, kama tutakavyoona baadaye, makada wa Umma Party waliweza kupanga Mapinduzi ya 1964 kwa kushirikiana na Wanaharakati wenzao wa mrengo wa Kisoshalisti wa ASP bila kumjulisha Karume, wakihofia kwamba angeyazuia Mapinduzi kwa kuwa alikuwa mwoga wa kumwaga damu.
Umma Party hakikushiriki kwenye Uchaguzi wa Julai 1963, badala yake, kwa kuona muda wa ukombozi ukipita mbio, kilijikita zaidi katika harakati dhidi ya Serikali. Na kufikia Julai 1963, kilikuwa Chama tishio kwa Serikali, chenye nidhamu ya hali ya juu kwa kuongozwa na itikadi ya Ki-Karl Marx na hivyo kuzua hofu mpya kwa Marekani na Uingereza ambazo tayari zilikuwa zimeanza kusherehekea na kupumua baada ya kufanikiwa kupandikiza chuki na uhasama ndani ya ZNP kikadhoofika; kwa kuanzia na Chama hicho kugawanyika kuunda vyama viwili, ZNP na The Zanzibar and Pemba Peoples Party (ZPPP) na hatimaye kujiengua kwa Babu na kundi lake kuunda Umma Party.
Uchaguzi wa Julai 8 – 15, 1963 ulitoa ushindi (bandia) kwa Muungano wa ZNP na ZPPP, na Mohamed Shamte, ambaye kabla ya mgawanyiko alikuwa mmoja wa Viongozi wa ASP, akateuliwa Waziri Mkuu na kuombwa kuunda Serikali ya ZNP/ZPPP, ambapo Sultani wa Zanzibar, kwa mujibu wa makubaliano ya Lancaster House ya Machi 19 na Aprili 6, 1962 na tena Septemba, 20 – 24, 1963; kati ya Waziri wa Uingereza wa Makoloni, Duncan Sandys na Viongozi wa ASP, ZNP, ZPPP na Umma Party (Babu kama mtazamaji na msikilizaji), aliendelea kuwa Mkuu wa nchi (Constitutional Monarchy) na mwenye mamlaka ya kuteua mrithi.
Sherehe za uhuru zilifanyika Desemba 10, 1963 ambapo Mwakilishi wa Malkia wa Uingereza, Prince Phillip, alikabidhi Hati ya Uhuru (Instrument of Independence) kwa Sultani Jamshid Abdullah bin Khalfa, kuashiria kile Esmond Martin anasema katika kitabu chake: Zanzibar Tradition and Revolution, “Utawala wa Waarabu sio tu kwamba ulibakia na kusalimika licha ya kuanzishwa kwa taasisi za kiwakilishi (vyama, LEGCO), bali pia ulipata hadhi na uhalali chini ya demokrasia ya Kikatiba”.
Na pale Babu alipoombwa kutoa salaam za Uhuru za Chama chake siku hiyo, aliushangaza umma na wageni waalikwa bila kumwelewa aliposema: “Salaam…Watu wa Zanzibar na Chama chao cha Umma, wanasubiri kunyakua Serikali na madaraka kuyaweka mikononi mwao siku na saa itakapowadia”.
Kwa wanaharakati wa uhuru wa kweli, lugha ya Babu ilikuwa wazi na dhahiri, kwamba Mapinduzi yalikuwa yakinyemelea Serikali mpya.- See more at: Raia Mwema - Abdulrahman Babu:-Tanuru la mapinduzi Zanzibar na Muungano lisilokumbukwa II
 

kanone

JF-Expert Member
Oct 10, 2013
6,197
1,500
Du! pole sana ndugu yangu nimepitia majibu ya wengi waliyokupa kuhusu hoja yako.watazania wa sasa ni washabiki na washangilia siasa kwenye hoja za msingi utapata majibu ya hovyo sana aswa tunaokaa kwenye mitandao.hili upate vitabu vinavyoeleza historia ya mzee huyo nenda kwenye makitaba kuu za taifa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom