Wadau nina shuda sana na Matofali ya namna hii, kwa mwenye ujuzi anijuze tafadhali. Haijalishi yapo mkoa gani, Cha muhimu ni upatikanaji na bei...View attachment 37892
Shukran
nenda Rombo utayapata.mia
Hongera kwa kupata mwamko wa kutumia mali ghafi bora na rahisi inyopatikana sehemu nyingi. Matofali ya aina hii yanaweza kufyatuliwa kwa kutumia udongo wenye madini ya iron na clay (Ruvuma, Rukwa, Geita, Njombe etc), na mafundi wa kuyafyatua wanapatikana Songea, Sumbawanga, Mbozi, Tunduma na Makambako. Nenda pale maeneo ya nyuma ya mlimani city kama uko Dar ukajionee nyumba zilizojengwa kwa tofali hizi, au pitia Vawa Mbozi, Laela Sumbawanga kote utaona nyumba zimejengwa kwa tofali za rangi na aina hiyo. Anza kuchakarika ndugu, ushauri nimekupa.
Mkuu, kwa jinsi ninavyoziona hzo ni tofali za kawaida tu za kuchoma, zimefyatuliwa kwenye udongo wa kichuguu na mfyatuzi mzoefu! Ukitaka kupata Tofali za kuchoma za kisasa na zenye kiwango cha hali ya juu nendA PERAMIHO-SONGEA-RUVUMA; Ninayo namba ya Fr mmoja kule lakn kwa baht mbaya hayupo nchini, hata hvyo kama kweli unazihitaji, na unaweza kuzisafirisha kutoka huko (Ningekushauri uangalie ukaribu pia, nadhani zipo sehm nyingi), kama unainsist ni-PM ili nione jinsi gani naweza kukuunganisha nawahusika!
Asante sana mkuu, kwa kweli peramiho ni mbali kidogo. Mi nipo dar, nikipata fundi mzuri akanichomea tanuri site kwangu bagamoyo yaani sijui atakuwa kanisaidiaje kwakweli. Asante sana.
mkuu nimejenga nyumba 2 in Dar kwa kutumia hayo matofali.na sasa hivi niko ktk mchakato wa kuchoma tofali ,nimeshapanga tanuru la 10000 bricks.
kuna rafiki yangu ni mtaalam wa kuchoma ,anaweza kuja site yako aka kagua na kukuchomea au kukuletea site yako,wewe unalipa tofali liko site.ila kama unakichuguu karibu anaweza kuja kukuchomea site yako.tatizo ni miti-kuni na aina ya udongo.
pia unaweza kujenga bila simenti,unatumia chokaa na mfinyanzi, a good example ni majengo ya Samora Avenue in Dar,mengi yametumia chokaa na mawe ktk ujenzi wake.
Wadau nina shuda sana na Matofali ya namna hii, kwa mwenye ujuzi anijuze tafadhali. Haijalishi yapo mkoa gani, Cha
muhimu ni upatikanaji na bei...View attachment 37892
Shukran
Bei ni Tsh 80/- kwa tofali. matofali 6 ni sawa na 1 tofali la cement.
Bei ni Tsh 80/- kwa tofali. matofali 6 ni sawa na 1 tofali la cement.