Wapi nitapata fundi mzuri wa AC ya gari hapa Dar?

Ramthods

JF-Expert Member
Jun 2, 2009
515
186
Wana JF, tangu miezi 3 iliyopita nimekuwa nikipata matatizo ya AC ya gari, ukizingatia tena hili jua letu la hapa bongo.

Nimeenda kwa mafundi tofauti, lakini baada ya mwenzi mmoja tu tatizo linarudi pale pale, na pia AC haipoozi sana kama hapo mwanzo.

Nahisi hawa mafundi naowapelekea hawajui wanachofanya bali ni kazi ya kubahatisha tu, huku hela zikiendelea kunichomoka mfukoni bila solution ya kueleweka.

Kama kuna mtu anafahamu fundi mzuri wa AC ya gari hapa Dar, ambae anajua nini anachofanya na si kubahatisha embu posti hapa au ni PM.

Natanguliza shukrani
 
Km upo Dar unaweza pia ukamuona bwana fulani anaitwa Magang'hila, pale CoET kwenye jengo lililo karibu na Staff Canteen, Groung floor
 
College of Engineering and Techology (CoET), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
 
Pale BMK namanga karibu na gym..hasa kwa Mercedes.....otherwise mcheki mchawi Maulid 0777334791 wa shaurimoyo
 
kwa makofia pale mt.lindi na shaurimoyo tatizo lako litaishia mara moja.
 
Asanteni sana wakuu kwa michango yenu. Inaonekana huyu jamaa makofia wa Lini na shauri moyo ni mkali sana, naona watu wengi wame mrecommend, pamoja na pale Gym moroko.
 
Pale BMK namanga karibu na gym..hasa kwa Mercedes.....otherwise mcheki mchawi Maulid 0777334791 wa shaurimoyo

Zamazamani, huyu mchawi Maulid ndio makofia wa mtaa wa lindi na shaurimoyo? Naona kuna watu wamezungumzia jamaa wa mtaa wa lindi na shaurimoyo anaitwa makofia.
 
Zamazamani, huyu mchawi Maulid ndio makofia wa mtaa wa lindi na shaurimoyo? Naona kuna watu wamezungumzia jamaa wa mtaa wa lindi na shaurimoyo anaitwa makofia.
Duh,

Makofia naona ana soko kubwa sana. Angalia mtaa huo huwa kuna jamaa wanajiita Makofia na wanakuwa wamevaa kofia ili kujiita wao Makofia na wenzao wanakwambia 'Huyo ndiye Makofia mwenyewe'. Ndiyo Bongo

Makofia mwenyewe ni mkali kwenye AC za magari, he fixed two of my cars and I approve him!
 
Bora umenishtua, nadhani ningeingia mkenge mzima mzima! Watanzania tuna ubunifu sana kwenye mambo ya wizi, lakini zero kwenye mambo ya maendeleo!
 
Duh,

Makofia naona ana soko kubwa sana. Angalia mtaa huo huwa kuna jamaa wanajiita Makofia na wanakuwa wamevaa kofia ili kujiita wao Makofia na wenzao wanakwambia 'Huyo ndiye Makofia mwenyewe'. Ndiyo Bongo

Makofia mwenyewe ni mkali kwenye AC za magari, he fixed two of my cars and I approve him!

Kiongozi na wewe unaelekea kwenye ufisadi? gari mbili za nini zote? za mamsap hujaweka hapo!
 
Kiongozi na wewe unaelekea kwenye ufisadi? gari mbili za nini zote? za mamsap hujaweka hapo!
Kwa kawaida mkuu unatakiwa uwe na gari walau 4 hivi home...

Unaweza kujua za nini na nini... Jamaa zangu hapo Dar wanajua kwanini! Ukienda Bongo nambie nikuunganishe na jamaa wanaoweza kukupa deal za maana upate gari fasta la kuzungukia jijini
 
Mamsap car is my car and my car is mamsap car.. Huenda Kiongozi anaongelea gari moja linalomilikiwa na watu wawili wamoja!
Duh, watu mna akili za haraka si kawaida.

Mkuu Ramthods, angalia matapeli wa Dar pale ni wengi sana, wataweza kukuzungusha na kujifanya Makofia, tatizo la Makofia mwenyewe anapoona mtu ana-fake kujiita Makofia hachukui hatua, hilo ni tatizo kubwa. Bora uwasiliane naye ukifika maeneo yale kwa kumpigia simu then mwonane u-confirm ndiye. Ni mkali kweli
 
Namba yake nitaipata wapi, au ndio hii kuna jamaa kaitoa kwa jina la Maulid?
 
Kwa kawaida mkuu unatakiwa uwe na gari walau 4 hivi home...

Unaweza kujua za nini na nini... Jamaa zangu hapo Dar wanajua kwanini! Ukienda Bongo nambie nikuunganishe na jamaa wanaoweza kukupa deal za maana upate gari fasta la kuzungukia jijini

Nimekusoma kiongozi! Nitafanya hivyo kwanza niwekee simu yako kwenye PM nyie ndo watu muhimu mjini...si wazee wengine wanasubiri kupiga mzinga!
 
Naitafuta then nitakupa soon, kuna jamaa yangu hapo Dar anaweza kunipa namba yake... I might be late but will have a solution

Mkuu nakubaliana na wewe hapo.

Zamani alikuwepo makofia kweli lakini siku hizi eneo lote lile limejaa 'mafundi' wa AC, kila mmoja akijifanya mtaalamu, na ni kuwa magari yamekuwa mengi na makofia haweza kuyahudumia yote so ndo kisa cha hii boom ya mafundi wengine uchwara na wengine wa kweli.

Hadi STK/STJ/DFP huwa zinaenda kwa makofia.

Ni vizuri kuwa na contact kabla mkuu ili kuepuka kuingia kichwa kichwa nadhani kwa hapa utapata, mi nishaipoteza contact ya fundi wangu lakini alifix AC for good sasa haisumbui tena!

All the best
 
Back
Top Bottom