Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 74,850
- 155,795
Mwanzoni nilikuwa nikianika bafuni, kuna siku tumbo la kuaibisha likanishika. Nikatoka nduki hadi bafuni kwetu ambako choo na bafu viko ndani ya chumba kimoja, huko kilichonitokea sitakaa nisahau. Nilikuta mke wa mpangaji mwenzangu akiitumia chupi yangu niliyokuwa nimeifua asubuhi kujisugulia mwilini mwake. Tumbo langu la kuhara likaishia hapo na yule bibie sikumuuliza kisa cha yeye kuifanya chupi yangu dodoki lake la mwilini. Tangu siku hiyo nikawa naanika chumbani.
Jana nimetembelewa na mke wangu mtarajiwa. Yeye anajiendeleza katika chuo cha mahakama kilichopo Lushoto.
Alipoona chupi nimeanika chumbani akaanza nigombeza kuwa ni mwiko na aibu kuanika chupi chumbani. Nimejaribu kumuuliza kuwa nianike wapi? Badala ya kunielewesha kaanza kunilaumu kuwa simjali wala simsikilizi. Mimi ni mtu jeuri nisiyemthamini na kumuenzi.
Tangu jana hadi muda huu kanuna.
Jamani wana MMU nyie chupi zenu mnaanika wapi nami nije kuanika yangu?