Wapi naweza kupata mafunzo ya mbwa?

msemakweli2

JF-Expert Member
Jul 28, 2013
1,627
1,879
Heshima kwenu wakuu,

Naulizia mwenye kufahamu sehemu ambayo naweza kuwapeleka mbwa wangu kwaajili ya mafunzo, nilisikia polisi kurasini kitengo cha mbwa wana hii huduma, tafadhali mwenye taarifa za kina kuhusu kurasini anipe, kama vile gharama, jinsi ya kujiunga huko, naanzia wapi na mafunzo huchukua muda gani.

Heshima kwenu wakuu.
 
Nenda kitengo cha farasi na mbwa kilwa Road ukaonane na afande yeyote akusaidie. Wana list ya dog trainers ambao siyo polisi wanaoweza kukupatia hiyo huduma. Nilikuwa na namba ya trainer mmoja ila niliipoteza kitambo, alinifundishia Belgian Malinois wangu.
 
ahsante mkuu
 
heshima kwenu wakuu, naulizia mwenye kufahamu sehemu ambayo naweza kuwapeleka mbwa wangu kwaajili ya mafunzo, nilisikia polisi kurasini kitengo cha mbwa wana hii huduma, tafadhali mwenye taarifa za kina kuhusu kurasini anipe, kama vile gharama,jinsi ya kujiunga huko, naanzia wapi na mafunzo huchukua muda gani.
Heshima kwenu wakuu.

Mpigie huyu kijana anaweza kukusaidia issue yako 0714-006126
 
Sikushauri kupeleka Mbwa wako kule utakuja kujuta Ni sawa na kupeleka gari lako binafsi Temesa kwa kuwa tu kuna Mafundi wa Serikali.
Vya kula kule vya PPRA vyenye 10%
Usishangae Siku unaenda kumchukua unaambiwa yamemkuta Kama ya Faru John
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom