Wapi naweza fanya DNA hapa DAR? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wapi naweza fanya DNA hapa DAR?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by She, Jan 29, 2010.

 1. S

  She New Member

  #1
  Jan 29, 2010
  Joined: Jan 29, 2010
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nina mimba na nina hisi kama sio ya mume wangu. mume wangu ni mzungu ,nilietembea nae ni mweusi kama mkaa, kutoa mimba naogopa kwasababu nimekuwa nikitafuta mimba muda wa miaka 7 sasa bila mafanikio. Je kama mtoto mungu alieniandikia ndie huyu nifanyaje?

  Huyo nahemuhisi ndiye mwenye mtoto ana wake wawili na watoto 8, najua hana uwezo wa kuningalia ingawa ananipenda sana. Mume wangu ana kazi nzuri kwenya shirika moja la simu, nikijifungua mtoto sio wake najua lazima ndio iwe mwisho wetu

  Naelewa mwisho wa siku labda itanibidi niitoe hii mimba ila nahitaji kujua kama kuna njia yoyote ya kuweza kujua DNA ya mtoto kabla ya kuzaliwa, tayari najua blood group ya mume wangu na ya huyo mtu wangu wa nje, Je wanaweza kunichekia blood group ya mtoto bado akiwa tumboni wakaniambia ni yupi ndio baba?
  Nimesikia Tanzania kuna sehemu wanacheki DNA Ila mimi nahitaki wanifanyie hiyo DNA sasa hivi wakati mtoto yupo tumboni

  Nipo njia panda
  Pendo
   
 2. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #2
  Jan 29, 2010
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,326
  Likes Received: 1,793
  Trophy Points: 280
  Mimi sio Dokta ila kuwa jasiri mama umlee mtoto. Maisha ndiyo hayahaya hatuendi kuishi kwenye sayari nyingine.Unaweza kabisa ukamlea huyo mtoto kama unataka
   
 3. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #3
  Jan 29, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,185
  Trophy Points: 280
  Huyo mtoto si wa mumeo na wala usitake kumuua kwa tamaa zako.

  Dar-es-salaam hamna DNA, na hata kama ipo hawawezi kumpima mtoto ambaye hajazaliwa.

  Colin Powell angekwambia "You break it, you own it"

  Kama ulitaka ku jump around kwa nini ulikimbilia kuolewa? Au unatuona tusiotaka kuoa/ kuolewa wajinga?

  Nachukia sana ninapoona watu wanataka heshima ya ndoa bila ya kutunza misingi yake.

  Hypocrisy.
   
 4. Saikosisi

  Saikosisi JF-Expert Member

  #4
  Jan 29, 2010
  Joined: May 4, 2007
  Messages: 528
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  DNA hawapimi kirahisi kama vipimo vingine. Kwa bongoTZ itakuwa ni issue ya wewe na mume wako kuwa referred na mahakama kwenda kupima kwa mkemia mkuu wa serikali! Kwa maelezo yako hayo... hiyo DNA hutaweza kufanya hapa TZ.
  Na kuhusu blood group, ni ngumu sana kuweza kukusaidia kujua baba wa mtoto... mfano kama wewe ni group A, mume wako group B, mtoto anaweza kuwa group A, B, AB au O!
  kweli uko njia panda lakini njia nzuri ni kujiandaa kuwa responsible na actions zako.
   
 5. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #5
  Jan 30, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  yani umeangaika kutafuta mtoto kwa miaka 7 now unaujauzito unaanza kuwaza kutoa kkweli mungu akupi kila kitu kwenye maisha ushauri wangu jiandae kulea acha ujinga
   
 6. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #6
  Jan 30, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Ukome mmezidi kuruka ruka naombea uzae mtoto mweusi kama mkaa ili uumbuke kabisa. Mmezoea kutubambikizia
   
 7. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #7
  Jan 30, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  ukishatoa hiyo mimba una
  uhakika gani wa kupata mimba nyingine....
   
 8. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #8
  Jan 30, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Soma Signature yangu dada, Amin Amin nakwambia lazima yakukute
   
 9. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #9
  Jan 30, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Yaleyale ya wanawake kutotaka kujitegemea na kuwa magolikipa na kuishia kuolewa na wazungu ili waukate na kutakata. Sasa mama hilo tibwili unalo.
   
 10. Consultant

  Consultant JF-Expert Member

  #10
  Jan 30, 2010
  Joined: Jun 15, 2008
  Messages: 5,797
  Likes Received: 6,307
  Trophy Points: 280
  Pole na hongera kwa kupata mimba!

  1. Mimba yako 'unahisi' ina miezi mingapi?

  2. Umeoloewa na huyo mzungu wako kwa miaka mingapi sasa?

  3. Unasema kwamba umekuwa ukitafuta ujauzito kwa miaka 7.....does this mean umekuwa na mzungu wako kwa miaka 7?

  4. Kipi kinakufanya uhisi kwamba mimba hiyo si ya mumeo bali ni ya huyo jamaa mwingine?

  5. Huyo jamaa aliyekumega umeshamwambia kuwa unahisi kwamba una ujauzito wake?

  Watu wanaweza kukusaidia ushauri kama wanapata info za kutosha. Ingawa mimi sio daktari, ninahisi sio rahisi kupima DNA ya mtoto ambaye hata hajazaliwa!

  Jipe moyo
   
 11. Kamjingijingi

  Kamjingijingi JF-Expert Member

  #11
  Jan 30, 2010
  Joined: Mar 10, 2009
  Messages: 792
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 45
  Pole dada. na mungu akulinde uzae salama salimini.mali inatafutwa lakini mtoto ni uwezo wa mungu usiogope kuwa baba yake hana mali .ugumba hauna thamani uzeeni dada pendo .baki na mtoto tunda la thamani taifa la kesho .
   
 12. Who Cares?

  Who Cares? JF-Expert Member

  #12
  Jan 30, 2010
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 3,465
  Likes Received: 1,950
  Trophy Points: 280
  mnhhhh...hapo patamu dada yangu....mie nakushauri yafuatayo
  1:- kama umesoma kidooogo biolojia sio lazma mtoto azaliwe akifanana 100% na baba yake(ndio maana baba na mama weusi tiii anatokea albino....vivyo hivyo baba mzungu mama mswahili hutokea pia mtoto mzungu...au baba akiwa mswahili mama mzungu akazaa mzungu inamaana mama amemegwa na wazungu wenzie?
  2:- kibongobongo KITANDA HAKIZAI HARAMU....mzungu inabidi akubali matokeo...hata akija kupima dna baadae ajiandae kuwa baba mlezi
  3:- sahivi jiandae kumpiga ma-sapraiziii ya kufa mtu...anza mazoezi ya kulia kwa furaha...anza nyodo za kudekadeka kija-uzito, anza kutoa mahitaji ya msingi kwa future ya mwanao...maana usipojipanga now inaweza kula kwako kesho
  4:-kutoa mimba ilikuwa enzi za mwalimu...sikuhizi watu wanaelewa kuwa single parenting nayo inalipa na inawezekana...kama vipi kaza uzi zaa hata kama noma ikiwa na iwe...wewe utakuwa umepiga bao ...yes..ndoto yako imetimia

  ..ni maoni tuu...finitoo
   
 13. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #13
  Jan 30, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Kwa Dar DNA inapimwa kwa Mkemia Mkuu, pale karibu na hospitali ya Ocean Road. Lakini haiwezekani kumpima mtoto aliye tumboni, ni mpaka azaliwe
   
 14. Konakali

  Konakali JF-Expert Member

  #14
  Jan 30, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 1,508
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145


  Hawa ndio wale ambao tukizungumzia kuhusu DNA wanakuja juu, je wadada mnasemaje? Mbona mnakaa kimya? Tafadhali, zungumzeni.
   
 15. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #15
  Jan 31, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,476
  Likes Received: 5,716
  Trophy Points: 280
  unalo babuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu eeeeeee
  Nyie mungu ndio anapenda kuonyesha miujiza yake kwa kupitia wengine ili
  watu waheshimu ndoa zao;m wala sina cha kukusaidia zaidi ya kusema polleeeeeeeeeeeeee
  ukiachika ni pm!!!1
   
 16. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #16
  Jan 31, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  hadithi ya kubuni hiii.....
  hamjashtukia?????????
   
 17. Annina

  Annina JF-Expert Member

  #17
  Jan 31, 2010
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 437
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  The Boss, upo rafiki?

  Tukirudi kwenye mada, inawezekana hii ikawa hadithi ya kutunga, ila kuna dada mmoja imewahi kumtokea. Alikuwa na mchumba mswahili aliekuwa masomoni nje ya nchi, huku nyuma dada akaanza mahusiano na baba mmoja wa kiarabu - akajengewa nyumba kigamboni, kunuliwa gari na matunzo mengine kama mke! Jamaa alikuja likizo alipoondoka dada akagundua ana mimba, mtihani ukawa kujua mimba ni ya nani, huku mipango ya harusi inaendelea, na mwarabu anaendelea kutunza mimba akiamini ni yake! Ilikuwa balaa, aliamua kwenda kujifungulia kwao bukoba ili ajue cha kufanya mtoto atakapozaliwa... naomba nisieleze kilichotekea kwa manufaa ya mtoa mada na wengine.


  Asante sana


  Annina
   
 18. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #18
  Jan 31, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  nipo mpenzi.....
  umesema huyo dada kwao bukoba......
  hapo sishangai kitu.
   
 19. Triplets

  Triplets JF-Expert Member

  #19
  Jan 31, 2010
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 1,103
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  mimi na assume kwamba hii story ni ya ukweli,
  kwanza hongera kwa kupata mimba watoto ni zawadi kutoka kwa Mungu na sio laana hata siku moja haijalishi amepatikana vipi?, naheshimu pia uoga wako wa kutoa mimba huo nao ni ujasiri mkubwa

  nakushauri usitoe mimba, usubiri mtoto azaliwe, wakati huo huo uanze kubuni mbinu ya jinsi ya kujitegemea ki fedha, kama mtoto sio chotara mpime hiyo DNA, kama sio wa mzungu ongea na mumeo umuombe msamaha, then yeye ataamua hitima yako inategemea na situation uliyompata huyo mtoto, mumeo ni mtu wa aina gani na je wewe unajisikiaje kuishi na mume mzungu na mtoto asiye wake ndani ya nyumba

  kama akitoa talaka, huna njia zaidi ya kujifunza kujitegemea na kutunza mtoto.

  halafu tokea sasa hivi achana na huyo baba wa watu stick na mumeo, ukishindwa ondoka pumzika tafakari ndio uende kwa mwingine unapochanganya wanaume una jiharibia mwenyewe, unaharibu ndoa zake huyo baba na unajivunjia heshima yako, unavunja heshima ya mumeo na unavunja ndoa yako
   
 20. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #20
  Jan 31, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Weweeeeeeee!

  What a sweet revenge! Yaani dada haya ndo malipo yako ya kutokuwa mwaminifu! Na hapa siachi kusema tamaa imekuponza!

  Lakini katu usitoe hiyo mimba; utakuwa unajiunga kwenye kundi la cold blooded killers! Na sauti ya mwano itakulili hadi uingiapo kaburini! I'm talking from kisipiriensi!

  Hopefully katakuwa ka-bouncing baby boy na ukikalea vilivyo katakuaj kukusetiri na kukupa maisha mazuri!

  Hongera kwa kuwa mama!
   
Loading...