Wapi Edil Ganzel??? Ni kweli

Sumba-Wanga

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
5,349
1,224
Jamani Edil Ganzel nimemkumbuka huyu Gwiji wa tamthilia. Nimekumbuka moja ya tamthilia zake: Kama simu ya Kifo, Kijasho chembamba na nyingine......

Jamaa alikuwa mzuri sana enzi hizo tukiwa bado wadogo. Kuna kipindi kama nilisikia hayuko nasi tena.........?

Ni kweli jamani? Kama kuna mwenye habari zake kamili.
 
msako wa hayawani, kimetulia

Yaah hicho niliwahi kukisikia tu lakini sikukisoma.....

Kijacho chembamba kinamhusu jamaa mmjoa aliyekuwa bosi wa polisi.
Mkewe yuko Hosp kujifungua, yeye akaamua kukata kamba mitaani, akaishia kwa malaya.
Mara malaya alielala naye akauawa kwa kisu, Kwenye kisu kuna finger prints za bosi wa polisi..
Mpelelezi wake aliyekuwa anachunguza hiyo kesi yuko makini sana, akaanza kumshuku bosi wake...

jamaa alitokwa na kijasho chembamba.....
 
RIP Eddie Ganzel.

Watu wa aina yake ni adimu sana siku hizi.

Unakumbuka hadithi zake zaidi ya Kijasho chembamba?????
Kweli watu wa aina yake wameadimika sana,
Nani wa kuziba pengo la MUSIBA na Willy Gamba wake??
 
Kweli watu wa aina yake wameadimika sana,
Nani wa kuziba pengo la MUSIBA na Willy Gamba wake??

Ni kweli kabisa, hawa wakina Shigongo sina hakika kama wameweza kujiza haya mapengo, kwa maana sijapata nafasi ya kusoma thrillers zao!
 
Shigongo kafulia cku hz! Anatengeneza stories zenye diferent heading bt same content! Nshaachaga kusoma mistory yake! Eddie Ganzel alikuwa anaandika pia story za katuni ktk jarida la BONGO enzi hzo! Kwa Mungu mbali, msako wa hayawani, mzimu wa mzee ole, n.k!
 
Labda Issa Hussein Tuwa kidogo alikuja vizuri na riwaya zake kama
Mkimbizi,
Mdunguaji,
Bondia na
Utata wa 9/12 ambayo ilikua ni hadithi ya aina yake
 
Okay hapo sasa nimekupata. Mzimu wa Mzee Ole ni tofauti na zile stories za mzee Ole wa kwenye gazeti la sani?
Kwa kweli sijasoma kabisa stories za Shigongo, huwa naona ziona headings nzuri sana za kiingereza, ila najua ndani yanaweza kwua yale yale ya headings za Bongo Movies....
 
Labda Issa Hussein Tuwa kidogo alikuja vizuri na riwaya zake kama
Mkimbizi,
Mdunguaji,
Bondia na
Utata wa 9/12 ambayo ilikua ni hadithi ya aina yake

Mkuu SHARK, kusema ukwlei huyo sijawahi kabisa hata kumsikia!:embarrassed1::disapointed:
 
Back
Top Bottom