Mada maalum kwa wapenzi wa Tamthilia ya Isidingo

Brad na jody wametoka fishing,wakiwa ofisin kwa barker wakiongelea ya huko walipotoka mara barker anaingia na kuendeleza maongez,mlango unagongwa anaingia kamo akimwambia jody kasahau simu yake kwenye gari,barker anagundua fishing walienda na kamo hali inayomchukiza

Obakeng anapeleka file la kazi kwa papa g,papa g anamuuliza kuhusu mtu mwingine wa kazi,obakeng anasema ni calvin ila amekataa ofa na kwamba saiv kajiweka karibu na aphiwe. Papa g anamwambia obakeng amsahau aphiwe,awe karibu na kamo,obakeng hapendezw na ushauri huo

Tyson na barker wakiwa ofisin duncan tyson anamuuliza kafikia wapi kuhusu nina ila barker anamwambia asubirie ataona,nina anaingia na kuuliza alichokifata hapo,barker anamwambia amekubali kumpa ofa ya share,tyson hajakubaliana na wazo hilo

Skhu anampa ofa aphiwe ya kuwa boss the rec ila bidada ana mipango yake hivyo anakataa ofa

Matlala na wenzie wanampelekea gabriel mawe ya dhahabu,gabriel anawauliza kama walikua makin hawafatiliw,matlala anamshushua na kumtaka awalipe kwa muda pesa zao kisha anaondoka na wenzie,gabriel anachagua mawe madogo kwa ajili ya papa g huku makubwa kwa ajili yake,morogwa anamuonya kucheza na hatari

Nikiwe anarudi penthouse,ila anaishia kulumbana na linc kuhusu kesi ya linc

Rajesh anapeleka file la nzinga kwa barker huku akkmtaka barker afanye haraka kuwaleta karibu kibiashara nzinga,ila barker anamuuliza kama kgotha ndio sababu ya rajesh kuwa na haraka hio ila rajesh anaishia kumpa mkwara barker ili asimfatilie zaid maisha yake binafsi

Skhu akiwa shebeen anatoa ofa ya kinywaji kwa morogwa huku akimwambia anataka kumsaidia kwa kushirikiana na watu mashuhuri kutoka kwenhe matatizo ya mgodin ila mororgwa anakataa ofa hio

Kamo anawaeleza lerato na mama ake juu ya alipokua fishing

Brad anamshauri juu ya masomo ya chuo jody hasa masomo ya miamba au engineering. Jody hana mpango wa kusoma ika brad anamwambia akachukue hata diploma amfurahishe barker

Gabriek anamlipa pesa jamaa fulan geto kwake mara morogwa anaingia na kumwonya gabr kwa michezo yake hatar na kwamba papa g hatar anaweza kumuua,gabr anamkaba morogwa na kutisha achunge mdomo wake kias cha kumtetemesha morogwa

Aphiwe anakuta maua mezan na kusoma ujumbe,skhu anamkuta na kuuliza yametoka kwa nani,aphiwe anajibu kwa obakeng,skhu anataka kuyatupa ila aphiwe anakataa na kuyagawa kwa wateja hadi zukisa na calvin,calvin anauliza kulikon,skhu anamwambia ukweli,calvin ana aphiwe wanafurahia huku skhu akiangalia eneo alilojibanza obakeng akishuhudia yote hayo

Brad anamwambia barker jins alivuomshaur jody kimasomo,barker hapendezwa na ushauri wa brad yeye anataka jody asoasome utawala.brad anajaribu kutetea hoja yake ila barker anamwambia yeye(brad)haitatokea akawa mrithi wakewake. brad anakosa raha kwa maneno hayo makali

Kgotha anapiaga simu kuulizia oda yake,mara mlango unagongwa bidaxa anadhan ni mhusumu,kufungua anamkuta rajeah na kushangaa ila rajesh anaingia kwa excuse ya majadiliano ya kibiashara,kgotha anamtaka rajwsh akaongee na barker. Na anamtaka aondoke humo rum haraka kabla ttson hajatokea mara tyson anatokea na kuwauliza kinachoendelea hapo
 
***** Morongwa AmeLike Comment Yangu Ktk Post Yake Instagram. Mniombee Jamani Nataka Kuwakilisha Taifa Kama Diamond.
Follow Her At Twitter soso Rungqu.
I Love This Sturdy Thuggish Bitch,Damn. Mwanzo Nlizimika Na Khabonina Khabodacious Khabosexy (Nina Zamdela) Ila Morongwa Kampiku. Na Ile Sauti Ilivokua Ya Kukwaruza.
 
Najua Tunaangalia Ya January 2017 Ila Nikiangalia ITV Inanifanya Mambo Yangu Mengine Yaende. Maana Mimi Najijua Nikianza Kuangalia Za SABC Youtube Ntakua Sifanyi Shughuli Yeyote Ya Kujenga Taifa.
Wacha Niwe Mtumwa Wa Kina Joyce Mhaville Tu.
 
Tyson anahitaji ufafanuzi kwann rajesh yupo humo chumbani,mkewe anasema ni masuala ya kibiashara ila tyson anasema mbona barker hafahamu,rajesh anajibu sio kila akifanyacho lazima barker afahamu. Tyson haelew somo kiasi cha rajesh kutaka kutoboa siri ila kgotha anawahi na kusema ni masuala ya nzigha na HI. Rajesh anaondoka,kgotha anataka kutoa maelezo zaidi ila tyson anampuuzia

Brad anamshauri jody achague kila anachoona sahihi kwake maana barker ana mipango nae pia

Jody analalamika kwa kamo jinsi brad na barker wanavyompangia cha kufanya,kamo anamwambia bora yeye ni tajiri kaandaliwa kila kitu na kumtaka afate anayoambiwa na wakubwa. Jody anabisha.kamo anamweleza jinsi alivyo na mimba bila mipango ya mbeleni,jodh anamwambia mwenye mimba yupo atalea,kamo anakataa obakeng kushirikishwa hapo ila jody anamwambia hawez beba(kamo) kila kitu pekee na kwamba asikate tamaa bali aangalie fursa zaidi

Skhu anamwambia aphiwe atamsindikiza kanisani ila aphiwe anasema calvin atampitia,mara calvin anatokea,aphiwe anasema anafata pochi yake,skhu anamuuliza calvin ukaribu wake na aphiwe,calvin anasema ni wa kawaida tu,skhu anamwonya akae mbali na mdogo wake hataki matatizo mengine.

Barker anamtaka jody akasomee business ila jody anataka engineering jambo lonalomkera barker. Jody anatoa mfano wa kamo ila barker anajugde kivyake mara anapigiwa simu kuambiwa jambo linalomkera na kuondoka ofisin

Rajesh yupo ofisin kwake mara barker anaingia na kumuuliza kwann anafanya mazungumzo ya kibiashara bila kumhusisha ,rajesh anamwambia sio kila akifanyacho lazima atoe repoti. Barker anamtisha kuwa akirudia tena atamfuta kazi,rajesh anatabasamu na kusema yeye sio muajiriwa wa kufukuzwa kirahisi maana pia ni shareholder hapo

Kanisani aphiwe na calvin baada ya zoez calvin anamwambia aphiwe kuhusu biaahara aliyoambiwa na obakeng ila kaikataa. Pia anampa ushauri aphiwe kuwa bora alivyoachana na obakeng

Barker na tyson wakiwa duncan baa,wanamuuliza skhu alipofikia kwenye ishu ya morogwa,skhu anawaambia morogwa kakataa,wakiwa wanamlaumu kwa kushindwa mapema mara morogwa anatokea na kutaka kuongea na skhu ila skhu anamtambulisha morogwa kwa barker na tyson na kumwambia hao watamsaidia,ila morogwa anamashaka nao kwa utajiri walionao kumsaidia yeye. Wakati skhu akiagana na tyson na barker mafa gabriel anatokea na kumuuliza skhu alikua anafanya nini na hao watu au ndio anasalit kampun,skhu anamwambia gabr afate kampen zake asijishughulishe na visivyomhusu. Gabr anamwambia skhu hata akiwa na hao watu nikiwe hawezi kumrudia

Aphiwe akiwa kanisanj zjkisa anamuuliza kuhusu maua aliyokua anagawa,aphiwe anasema ni zawadi toka kwa mtu aisiyemtarajia. Zukisa anasema ni vibaya kugawa zawadi maana ni ujjmbe wa kuomba msamaha ila aphiwe anamkumbusha zukisa usaliti wa sizwe,zukisa anasema situation yake ilikua tofauti na kumtaka aphiwe asamehe

Shebeen kijana anamletea fujo sechaba,skhh anajngia na kuuliza kulikon,sechaba anamwambia vijana wanataka kurud kazin na mgodi umefungwa, na kumwomba skhu akaonhee na linc wajue kinachoendekea.skhu anasema nj ngumu hajaonana na linc siku nyingi,sechaba anasema atajaribu kuonhea na linc,skhu anamwambia amwambie linc kuwa awe makin maana kuna wanaotaka kumdondosha haraka.sechaba anashangazwa na ujumbe huo

Nina yupo the dec kaagiza msosi,skhu anashangazwa na uwepo wa nina mahali hapo na kumuuliza kama yupo sawa,nina anajibu ndio.skhu anaondoka mara aphiwe anaingia,nina anamfata na kumwambia kammis na kwamba urafiki wao usife awe anamtembelea home,aphiwe anagoma maana anahisi nina anataka kumrudisha kwa obakeng,baada ya nina kujitetea aphiwe anamwambia atafikiria

Kamo anaenda the rec na kumkuta aphiwe kaunta,aphiwe anamkaushia kamo anaagiza keki,kisha anamwambia aphiwe kuhusu salun kupooza maana wao hawapo na kwamba haruhusiwi(kamo) kuingia salun.kisha anamwambia aphiwe alihitaj rafiki wa kumwambia hayo tu

Gabriel akiwa na mawe ya dhahabu anampigia mtu na kumwambia anataka kufanya biashara huru akiwa pekee bila kuajiriwa na mtu
 
Monday

Nina anaingia sebulen na kumuuliza obakeng jamaa aliyetoka humo mdan muda mfupi ni nani,obakeng anajibu ni afisa wa serikali atakayesaidia dili la biashara yao.nina anakasirika na kumwambia obakeng hio shughuli haimfai. Nina anamtaka obakeng akazane kumrudisha aphiwe ila obakeng anasema kashindwa hasa baada ya aphiwe kugawa maua yake. Nina anamhakikishia atamrudisha aphiwe

Jody anaenda kwa barker kuomba pesa ya kufanyia party ya muagano na rafiki zake kabla hajaondoka HD ila barker anakataa na kumkumbusha jody vituko vyake vya mwanzon na kumtaka kama anataka party alipe 60k. Jody anakereka

Aphiwe anaenda kwa nina,nina anampa maneno mengi matamu kiasi kwamba aphiwe anarudisha moyo wa kumsamehe obakeng

Nikiwe anampelekea linc files za kusain,linc anashangaa kupelekewa file wakati huo huo nikiwe ndo alikua wa kwanza kumtoa kwenye bodi,mara zukisa anaingia na maua,nikiwe kusoma anakuta yametoka kwa ben,linc anashangaa uhusiano upi mpaka atumiwe maua. Gabriek anaingia kwa mbwembwe,linc anamuuliza kafata nn,nikiwe anasema ni mgeni wake. Linc anaondoka kimya kimya

Barker na tyson wanamsubiria skhu aliyetoa wito wa kuwaona. Skhu anawashauri waache kumtumia morogwa ila jamaa wanasema its too late lazima wamtumie na kwamba skhu akitaka kujiondoa ajiondoe maana wao wameshapata documents alizoiba SG. Skhu hana ujanja.

Gabriel anamuuliza nikiwe kuhusu aliyemletea maua na je ni skhu ila nikiwe anasema ni rafiki. Gabriel anamwambia nikiwe amfikirie na kwamba hajaona mwanamke mwingine zaidi yake.

Jody na brad wakiwa the rec wakiongelea sehemu nyingine ya kufanyia party,mara skhu anatokea,jody anamwomba ushauri wa sehemu ya kufanyia party .skhu anawaambia shebeen,jody anafurahia ila brad anapinga wazo hilo

Calvin ananunua cd kwa mtu shebeen,wakati anaondoka anakutana na obakeng wanaishia kubishana kuhusu aphiwe

Gabriel kwa mbwembwe anampelekea mawe machache ya dhahabu papa g. Papa g anamwonya gab kwa kumpelekea mzigo mdogo na kumtaka safari nyingine ampelekee mzigo kubwa.

Jody na brad wanakubaliana na nina kukodi shebeen pia wateja wa kila siku wanakaribishwa pia. Brad anatoa advance

Sechaba anamshangaa skhu kwa kuitupulia bingo ya akina jody,skhu anasema hawezi dili na party za kumchosha

Gabriel anamgombeza matlala kuwa anamletea mzigo mdogo na kwamba aongeze bidii ili asimuone papa g akikasirika

Skhu anampelekea geto morogwa bidhaa nyingi za bei mbaya akisema zimetoka kwa tyson na barker. Morogwa anafurahia sana

Calvin anamkabidhi aphiwe cd na kumtaka waangalie pamoja usiku huo,ila aphiwe anakataa na kusema hana muda labda weekend,calvin anakubali kinyonge. Aphiwe anakuta ua kwenye ndoo ya uchafu ambalo obakeng alileta meng akayagawa,analichukua na kuliweka kwenye glass ila anaona haifai kukaa hapo na kuamua kuondoka nalo
 
33 Reactions
Reply
Back
Top Bottom