Mada maalum kwa wapenzi wa Tamthilia ya Isidingo

f578bf8d321af38c8ad09725a5cf2413.jpg
 
Jaman hivi Isidingo, NAYO ni ya kulumbania!?? Au kutoana povu!?? Kama na we we unapenda kuhadithia, adithia tuuu au mpeane zamu, mbona mi sijaona kigum hapo!?? Tatizo wabongo kila kitu mnaona in siasaaa hadi MNABOA.
 
Kama hujui kitu uliza povu lote la nn hamna anaegombania kutoa update hapa, mkurupuko on fleek.
Jaman hivi Isidingo, NAYO ni ya kulumbania!?? Au kutoana povu!?? Kama na we we unapenda kuhadithia, adithia tuuu au mpeane zamu, mbona mi sijaona kigum hapo!?? Tatizo wabongo kila kitu mnaona in siasaaa hadi MNABOA.
 
Asubuh na mapema morogwa anamfata gabriel kujua kama kuna machafuko zaid,gabr anamtoa wasiwasi kuwa papa g keshasawazisha kila kitu,morogwa anaona ndio muda muafaka wa kuwa partners ila gabr anamchenga.

Hosp nina yupo busy wodin kuhakikisha obakeng yupo sawa kwa kumuuliza ampatie uji ila papa g anamwambia huyo ni mwanaume hivyo anahitaji pombe huku akimpa obakeng chupa ya pombe kuwa ni dawa tosha,nina anakataa. Dokta beth anaingia na kuwaambia mgonjwa hana tatizo kubwa,pia anahitaji kuongea nae alone.

Obakeng anakiri kuwa na ugonjwa wa kulipuka na hajawahi kutibiwa kwa tatizo hilo.

Eddie anamfata shebeen nina waongee vizuri ila nina hataki maongez nae na kumwambia lazima wamshtaki kwa kitendo alichokifanya.

Skhu,sechaba na parsons wapo katika maongezi kuhusu harusi ya sechaba na utani wa hapa na pale huku wakijikumbushia vituko vya familia ya lerato

Jana kamo aliiba shuka jipya chban kwa lerato, saloon lerato akiwa busy kuchagua mapambo wanaingia sechaba na parson na kuwaomba wamsaidie kuchagua ila wanaishia kumchanganya. Baada ya muda lerato analipata shuka jipya saloon ila kamo anasingizia ni la mteja alilisahau,lerato anabaki anashangaa

Gabriel anaenda omba kutoka out na nikiwe ila bidada anamtolea nje na kumtaka wawe na uhusiano wa kikazi pekee

Aphiwe anamtembelea obakeng hosp akimpelekea maua kama pole.

Eddie anajiandaa kwenda hosp,Yvette anatoa ofa ya kumsindikiza ila eddie anamtaka abaki maana anaweza sababisha matatizo mengine.

Kamo anamtembelea obakeng hosp na kumpa pole ya shuka(la lerato)

Nikiwe anazinguana na skhu kwa tabia yake ya kumficha mambo kwa uhusiano walionao.

Eddie akiwa anaulizia hali ya obakeng nina anawakuta na hapendezwi na kitendo hicho.

Nina anamfata brad duncan ofisin na kumtaka aombe msamaha kwa kitendo alichokifanya ila brad anampuuzia.

Nikiwe anagundua kuna kikao cha board kimeitishwa bila yeye kujua,anamfata baba yake na kumuuliza sababu ila wanaishia kulumbana na vitisho juu.

Lerato anagundua lile shuka saloon ni lake anamfata kamo sebulen na kumu expose mbele ya sechaba,aunt tilly,parson na kumuita mwizi,kamo anajitetea hakua na kitu cha kumpa obakeng,lerato anakasirika shuka lake kupewa huyo kijana na kumwonya kamo aache kulala nje ovyo,lerato anasema kachoka mambo ya kamo hivyo afunge mizigo kesho yake arud kwao na akina sechaba(wanaenda malizia mahari)
 
Asante Numbisa na pole kwa kuandamwa. Mpuuzie tu maana mwenyewe keshaomba poo. Gabriel baada ya kukataliwa out na Nikiwe,anaambiwa cheki yake iko tayari hivyo aichukue kwa secretary.(kumbuka sg wanadhamini kampeini ya zama zama.) Gabi anasema secretary hayupo kwani alimwambia anaenda kwenye kikao cha bodi. Niki anashangaa. Hivyo Gabriel ndie aliemshitua Niki kuhusu kikao cha bodi. Baada ya Niki kuonana na Linc na kukwaruzana kuhusu kuitishwa kwa kikao cha bodi bila kuhusishwa,Niki anaonekana kukasirika. Na nahisi atatoboa siri kuhusu baba yake kumuua Kat.(hii ni hisia yangu tu). Ni hayo tu kwa nyongeza.
 
Shukran mkuu upo vizuri. Nilicheka pale gabriel anataka mkumbatia nikiwe bidada akampausha

Hayakuhusu!!! Punguza kiherehere
 
Sechaba,parson na aunt tilly wapo mezani wakipata breakfast, kabla ya aunt tilly kujiunga nao mezan,sechaba aliweka whisk ili washerehekee kumaliza salama masuala ya labola,kumuona aunt tilly parson akaificha whisky. Aunt akagusia suala la kamo,lerato akalalamika tabia za kamo na kutaka asiongelewe maana ataharibu mood yake ya sherehe.

Papa g akiwa na morogwa na gabriel anamshaur gabr atumie chumba cheke kuwekea mizigo ili kuepusha purukushan na polisi,gabr hajapenda hilo wazo,papa g anauliza anaendeleaje na nikiwe,gabr anashtuka na kumwondoa morogwa kwa kisingizio awafatie bia(bidada haaminiki) baada ya morogwa kuondoka gabr anamwambia papa g kuwa nikiwe mgumu,papa g akamwambia atumie mbinu ya sympathy ili kumpata binti wa kitajiri, gabr anapenda ushaur huo

Lerato akiwa saloon anaongea na aphiwe aina ya maua ya siku ya sherehe,kamo anajibu bila kuulizwa na kushushuliwa,mara aunt tilly anaingia na kutaka kuongea na lerato,aunt anamwambia lerato kuwa wameshamtolea labola hivyo ameshakua matabane means abadilishe lide style ajiunge na kikundi cha wamama kanisani aende kanisani kila jumatano na asikose kipindi kama ma agness alivyokua na kuvaa uniform aache vinguo vifupi,lerato anasema jumatano ana wateja,aunt anamwambia hata ma agness alikua ana biashara,lerato anabaki speechless.

Nina kamuita aphiwe nyumban kwake kujua zaidi kilichotokea usiku kule duncan parking,bidada haongei ya maana zaidi ya kumlaum kamo kuwa ndie aliyesababisha yote yaliyotokea.

Aphiwe akiwa duncan kuchukua mtandio wake aliousahau siku ya tukio anakutana na brad,brad anajaribu kuongea na aphiwe kistaarabu ila bidada anakuwa mkali na kumlaumu zaidi.

Yvette anapokea simu inayomtaka eddie ila anaongea kwa niaba yake na kumtetea huku akionyesha dalili za kutokubaliana na kosa lililotokea.

Gabriel akiufanyia kazi ushauri wa papa g anaenda ofisin kwa nikiwe na kuanza utapel wake kwa kusingizia kuna watu wamevamia kwake na hajui wanatafuta nn,nikiwe bila kujua anadanganywa anajikuta anamhurumia na kumuuliza anaishi wap anamjibu anaishi nyumba duni,huku akisema labda kampen zinasababisha,nikiwe anajaa kwenye mtego kumuhaidi malazi mazuri zaidi maana wanamhitaji sana kwa kampen ya zama zama. Jamaa anatabasamu kwa ushindi

Nina akiwa duncan,papa g anatokea na kutaka kuongea nae ila nina hatak kuongelea masuala ya biashara,ana deal kwanza na suala la obakeng,wakiwa wanabishana anatokea barker,nina anamgaka papa g aondoke maana ana mazungumzo na barker,baada ya papa g kuondoka nina anamwambia barker kuwa brad aombe msamaha kwa kilichotokea la sivyo ataenda fungua kesi.

Brad akiwa na charlie kwa skhu wakipata vinywaji huku wanaongelea ishu ya aphiwe kumtetea obakeng,charlie anakuwa upande wa aphiwe akisema mapenzi ni upofu ukitokea kupenda hutaona mabaya ya mwenzi wako. Skhu anatokea na kuweka msimamo wake kuwa hamtaki obakeng awe na aphiwe.

Gabriel akiwa anajiandaa kuhama anahamia duncan kwa pesa za sibeko,huku chumba anachokihama watakitumia kuwekea mizigo yao,morogwa namkuta akifunga funga na kushangaa huku akitaka kujua nafasi yake maana anaefaid ni gabr pekee,wanabisha hapo bidada anaamua kuondoka

Lerato na familia yake wakiwa mezani,aunt tilly anakumbushia mazungumzo ya kumtaka lerato ajiunge kanisan na kuvaa uniform,sechaba na parson wanashangaa na kumtetea lerato. Parson anaaga kuwa kesho yake asubuh anaondoka,lerato anafurahi akijua na aunt nae atasepa ila aunt anasema haondoki kuna mambo anataka kuyaweka sawa

Kamo anamkuta nina duncan na kwenda kumsalimia ila nina anaishia kumlaum kamo kwa kuanzisha fujo zilizosababisha obakeng alazwe,lerato anatokea na kum taunt nina kwa kumtelekeza mtotowake tangu utoton kisha anakuja kumjali ukubwa,yanaibuka malumbano hapo mpaka brad anatokea kusuluhisha ila nae anaishia kuchambwa na lerato kuhusu style yake ya nywele

Eddie yupo hosp mara nesi anatokea na kumwambia anaweza kwwnda kumuona mgonjwa,eddie anasita kwanza kisha anaingia wodini.

Wodin obakeng anamtaka dokta asiandike kama ana tatizo kuzimia maana utotoni wwnzake walimsimanga sana na kumcheka,dokta anampa ushauri kisha kuondoka, eddie anaingia wodini,obakeng anamuuliza kama ameenda hapo kummaliza kabisa,eddie anajitetea ila obakeng hakubali na kuuliza kwann alikamatwa yeye pekee na brad akaachwa,wanalumbana hapo na obakeng anatishia kumshtaki eddie kwa yaliyomtokea.
 
33 Reactions
Reply
Back
Top Bottom