Wapenzi wa Simba Sports Club nao wasusie IPP Media? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wapenzi wa Simba Sports Club nao wasusie IPP Media?

Discussion in 'Sports' started by Chakaza, Mar 20, 2010.

 1. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #1
  Mar 20, 2010
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,684
  Likes Received: 21,946
  Trophy Points: 280
  Nimefadhaishwa sana kuona lile jambo lililokuwa likisemwa kuwa Vyombo vya habari vya IPP vimesusa kutoa habari za timu ya Simba hata pale inapo peperusha bendera ya Taifa nje kuwa ni la kweli.
  Jana Simba imefanya jambo ambalo kila Mtanzania anapaswa kujivunia, lakini kwa namna ya ajabu sio ITV, magazeti yake wala Radio One ambao wamelipa hata kwa uzito mdogo jambo hilo. Jee hii ni kuwatendea haki wasikilizaji,watazamaji na wasomaji wenye kutaka kupata habari za Simba?
  Jee wakati sasa umefika kwa wapemzi wa Simba nao ku Pay Back hujuma hizi za IPP kwa kususia kununua bidhaa zao,kutosikiliza au kusoma habari zinazotolewa nao? kutokupeleka matangazo ya biashara kwenye vyombo vyao?
  Hatua hii inaweza kuwapa fundisho kuwa ugomvi wa mtu mmoja mmoja usiwe unaihusisha jamii nzima.
  Imagine kama wapenzi wa Simba katika mechi yao ya marudiano wakija uwanjani na mabango yasemayo " KAMA UNAIPENDA SIMBA USINUNUE CHOCHOTE CHA IPP AU KUTANGAZA KTK VYOMBO VYAO" hali itakuwaje. Wadau mnasemaje kuhusu hili?
   
 2. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #2
  Mar 20, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,856
  Likes Received: 2,019
  Trophy Points: 280
  Nakuunga mkono Chakaza, ni jambo la kushangaza sana kuona kuna bifu za ajabu sana nchi hii. Waweke wazi watu wajue tatizo ni nini? Mimi nilikuwa nanunua sana NIPASHE lakini toka nisikie kuna bifu hiyo nanunua gazeti jingine kabisa. Simba juuuuuu bila ITV na RADIO ONE
   
 3. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #3
  Mar 20, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Mnacheza nyie ilikuja kampeni ya kususia mtandao wa VODA matokeo yake mpaka leo watu wanatumia ndo wanazidi kuongezeka kisa ni wa fisadi RA hapo mnacheza tu mtu asinywe maji ya kilimanjaro anywe maji ya Uhai au ya 50/= duh.
   
 4. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #4
  Mar 20, 2010
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,684
  Likes Received: 21,946
  Trophy Points: 280
  Fidel80, tusaidie mawazo jee ni sahihi kwa IPP kususia habari kama za jana?
   
 5. senator

  senator JF-Expert Member

  #5
  Mar 20, 2010
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 1,927
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Huenda hakuwa na reliable source ya information..tusubirie leo kama hawatangaza...Tunajua kuwa mengi ni Yanga damu ila kwa vyombo kama TV/Radio kutotangaza kitu cha timu kwa ubaguzi nadhan kuna haja hili swala kupelekwa kwenye baraza la sanaa kujadiliwa..Kwanza ni upotofu wa maadili ya vyombo vya habari..madhara uhuru wa utangazaji kupita mipaka
   
 6. M

  MzeePunch JF-Expert Member

  #6
  Mar 20, 2010
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 1,412
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Mimi ni mwana-Simba. Nilisusia kuangalia ITV baada ya siku ile kuacha kutangaza kuwa timu yetu imetwaa ubingwa, tena kwa rekodi ya aina yake - kwa kutopoteza mchezo. Hata hivyo, kwa habari murua za michezo Star Tv na TBC1 wako juu kuliko hao wababaishaji wa ITV. Kwa upande wa radio, Clouds 'Sports Extra' ndio wenyewe, hakuna haja ya kusikiliza kipindi cha michezo cha Radio One.
   
 7. senator

  senator JF-Expert Member

  #7
  Mar 20, 2010
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 1,927
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Je bidhaa tuachane na micoke cola na maji ya dasani na kilimanjaro turejee kwenye Pepsi na uhai?kwa kuwa hivi vyombo hatuna gharama tunayochangia kusikiliza wala kuangalia na hata kama hutaangalia sidhani kama wao watajua hilo..chakufanya ambacho kitaweza kuwagusa wao ni kutonunua bidhaa za kutoka kwa pande hiyo..Magazeti sana sana kutokana na habari lengwa kuwa ya michezo..
   
 8. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #8
  Mar 20, 2010
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Vipi hili likienda sambamba na kususia biashara za mafisadi kama vile Voda phone etc?
   
 9. Sinkala

  Sinkala JF-Expert Member

  #9
  Mar 20, 2010
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 1,505
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Hebu tuorodhesheeni bidhaa za IPP hapa
   
 10. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #10
  Mar 20, 2010
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Sasa hivi jina la Simba linauza, wakisusa kuandika habari zake kwenye magazeti yao hasara wanapata wao na hakuna mwanaSimba atakeyeathirika.

  Naona ~IPP wanaanza kufulia, siku si nyingi huko nyuma walisusa kutangaza habari za Yanga shauri ya bifu kati ya Manji na Mengi, na kipindi hicho mauzo ya magazeti ya IPP yalishuka sana, sasa kama wanaongezea na Simba sijui wanaelekea wapi.
   
 11. senator

  senator JF-Expert Member

  #11
  Mar 20, 2010
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 1,927
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  All products from Coca cola..bitterlemon, krest club soda,Fanta family,sparleta,sprite etc
  Magazeti:nipashe, Taifa letu, The Guardian, Kulikoni,( Leteraha na Alasiri-haya nasikia yamekufa kwa sasa),etc
  Anakampuni yakutengeneza tissues,(TP) etc
  Na miradi mingine mingi wadau wanaweza kuendeleza
   
 12. Eliphaz the Temanite

  Eliphaz the Temanite JF-Expert Member

  #12
  Mar 20, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,836
  Likes Received: 362
  Trophy Points: 180
  I'm in!!! Good for the goose, good for gander.
   
 13. T

  Tizo Member

  #13
  Mar 20, 2010
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mr. Reginald Mengi is very stupid to allow this to go on at his media outlets. Part of duties its media outlets play is to inform and educate people. He is very silly. I was in shock when I came to know that they were not broadcasting or writing any thing "simba" for some lame reason.

  We are his customers and we pay him to pay his employees and for him to make profit. As consumers , we can retaliate by not buying or using anything with his trade marks even if it is for free.

  I , for one, I no longer watch ITV, Listern to Radio One and I am now drinking Pepsi. I am switching to UHAI and sensodyne for a toothpaste.

  On the day we play Yanga I will come with a big plackard telling all football fans and all who love media to boycot the childish bullshit at IPP Media.

  Mengi empire is run by mad men.

  As for cloud fm!! these are nothing better.they are the lesser evil because their snub is subbtle. But Cloud entertainment are Mafia fellas. I have read and heard what they have done to Mr. Two ( Mbilinyi) and other artists and I tell you these are also to be boycotted. First of all they have assumed a role of Campaign heard quaters of the Top Brass in CCM. They have no objectivity at all. They sell their ignorance so much. I detaste them so much, I feel vomiting. They lick the boots of JK as if they can not live without him. In the face of politicians , they are scandalous!!! Total garbage. I think they think they can bacome powerful force some day by forgetting that the neutrality they had previously is what attaracted and made people gravitate towards their station.

  I hate them because they have become banners of politicians, mostly top brass.

  If you listern to Jahazi, Gadner keeps on playing his wife's songs.... even though there hundreds of artists in the country, forget about the world. He keeps on playing his wife's choir songs. We know he is the manager of his wife. But for goodnes's sake, kick out the biaseness
   
 14. leseiyo

  leseiyo Senior Member

  #14
  Mar 22, 2010
  Joined: Oct 25, 2007
  Messages: 116
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hakuna haja ya kusumbua kichwa kufikiria vyombo vya IPP na coverage ya Simba,after all kuna media nyingi zenye akili kama Star TV ambao nao walifanyiwa vurugu na Simba lakini wakamaintain profession.Tabia za kususa zimezoeleka IPP si unakumbuka waliwahi kuisusa Yanga kisa Manji kuwa mfadhili wa klabu hiyo?Hakuna cha kupoteza IPP waendelee na ukanjanja wao Simba tuendeleze mapambano hakuna wanachoathiri kwetu.
   
 15. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #15
  Mar 22, 2010
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Hakuna haja ya kususia jambo lolote. Hii si mara ya kwanzakwa IPP kufanya hivyo kwa vilabu vy soka. Kama kunamtu anakumbukumbu siku ambayo Yusuf Maji alipopatanisha makundi ya Yanga Asili na Yanga Kampuni na kutia saini mkataba wa kampuni yake na Yanga, Mengi alikasirika sana na hakuna habari yeyote iliyotolewa na vyombo vyake. Sasa hili la Yanga na Simba linaweza kuonekana kwa urahisi je kwa yale ambayo hayaonekani inakuwa?
  Itafika wakati wataandika tu habari za Simba wanataka wasitake!!!!
   
 16. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #16
  Mar 22, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,171
  Likes Received: 1,256
  Trophy Points: 280
  Mi naacha kununua maji ya kilimanjaro kuanzia sasa
   
 17. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #17
  Mar 22, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Wakuu... mimi nilishasusia hawa jamaa miezi kadhaa iliyopita na kwakweli ndio njia pekee!! enough with their acts
   
 18. Masaki

  Masaki JF-Expert Member

  #18
  Mar 22, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,465
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 160
  Sikumbuki ni lini mara ya mwisho nimewahi kukosa habari za Simba kwenye vyombo vya habari. Hii ni kwa sababu sisomi magazeti ya IPP wala kusikiliza Radio One wala kuangalia ITV. Ni zaidi ya miaka miwili sasa! Hawana kipya!

  Tanzania ni moja ya nchi zinazoongoza Afrika kwa kuwa vyombo vingi vya habari. Kama TV zote zinaonyesha habari za Simba kasoro TV za IPP, na kama magazeti yote yaana andika habari za Simba kasoro magazeti ya IPP, why should we bother about them? Achaneni nao! Ila ipo siku watakuja kupiga magoti wanaomba kutangaza mechi ya Simba laivu siku tutakapokuwa tunacheza fainali ya Kombe la Shirikisho, nasi tutawakalia LAIVU!
   
 19. N

  Nanu JF-Expert Member

  #19
  Mar 22, 2010
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,224
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Waandike wasiandike shauri yao, simba tuko juu!!! kwani lazima usikilize radio one au uangalie IT au usome Nipashe au Guardian? Magazeti mengine yameandika na redio zingine zimesema na tv zingine zimesema.
  Kama IPP Media wameiogomea Simba, hata Simba wakiwa wamecheza na timu za nje bado ni Simba tu na wala haiwi Yanga wala Azam wala Taifa Stars, wala Twiga Stars, Wala Serengeti boys, Wala Ngorongoro heroes. hivyo malalamiko ya kutokutangaza simba imeshinda Zimbabwe wala hayana maana. tatizo lililopo litatuliwe na uongozi wa Simba na wa IPP. Kama wewe shabiki wa Simba waulize viongozi wa Simba kulikoni????
   
 20. K

  Kijiweni Member

  #20
  Mar 22, 2010
  Joined: Feb 23, 2010
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Msusieni na JK,yeye si ndie mlezi la mafisadi.
   
Loading...