Wapenzi wa Club ya SIMBA wachukizwa SPIKA kualikwa kama Mgeni Rasmi Tamasha la MO Awards....

kasenene

JF-Expert Member
Jun 6, 2008
1,632
2,413
Kama ilivyo ada kwa Mabingwa wa Back to Back (B2B) Ligi kuu ya Tanzania bara na wanarobofainali pekee katika ligi ya Club bingwa Africa 2018/2019 na si wengine bali Wekundu wa Msimbazi wameandaa tena tamasha lao la " "MOSimbaawards 2019" tamasha ambalo hufanyika kila mwaka mahususi kwa ajili ya kuwaenzi/kuwapongeza na kuwazawadia wachezaji waliofanya vizuri kati ka msimu wa ligi iliyokwisha .

Tamasha hilo kwa mara ya kwanza lilifayika mwaka jana na kwa hakika pasipo na shaka lilifana saana. Tamasha la mwaka huu linafanyika 30/05/2019 na tayari maandalizi yake yakichagizwa pamoja na shamrashamra za kuchukuwa ubingwa wa mkwaka huu yalikuwa yaimepamba moto hadi pale club ilipotangaza jina la atakaye kuwa mgeni Rasmi wa tamasha hilo ambaye si mwingine bali "SPIKA" Nisingependa kuonekana "mdhaifu" au mchochezi katika jambo hili yoyote ambaye angependa kuona nini wamesema wanachama na wapenzi wa Simba akasome mwenyewe kwenye official instagram account ya club ya simba ambayo ni "simbasctanzania" ili pengine ajionee mwenyewe commnets zao. kwa ufupi wapenzi na wanachama Wa Simba wamechukizwa saana na kitendo cha kualikwa huyu mtu na wamezielezea kinagaubaga sababu za kuchukizwa kwao ni kitendo hiki
 
Back
Top Bottom